Mwanza: watoto waliotekwa wapatikana, watekaji wauawa kwa kupigwa risasi

Beira Boy

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2016
Posts
19,976
Reaction score
32,195
Amani iwe nanyi wapendwa

Wale watoto waliotekwa hatimaye wamepatikana lakini watekaji wameuliwa.

=====

Wanafunzi wawili wa Shule ya Blessing Model School waliokuwa wametekwa na watu wasiojulikana Februari 5, 2025 jijini Mwanza wamepatikana huku watekaji wakipigwa risasi na kupoteza maisha baada ya kuonesha nia ya kutaka kuwashambulia maaskari wakiwa na silaha.

Akizungumza katika eneo la tukio Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema watoto hao wamepatikana wakiwa wamefichwa katika nyumba namba 8 iliyopo katika Mtaa wa Nyagoloboya Kata ya Nyegezi huku watekaji wakiwa humo.

Pia soa > Mwanza: Watoto wawili wa Shule ya Blessing Model watekwa, wengine Wanne wanusurika

Hata hivyo Kamanda Mutafungwa amesema baada ya maofisa wa jeshi hilo kuzingira nyumba na kuwataka watekaji watii amri walitoka wakiwa na silaha kama mapanga na rungu hali iliyopelekea kutumia risasi.
 
Serikali haijaweka wazi.

Ila naamini IPO AMRI ya chini Kwa chini ya kuwapiga vyuma WAHALIFU WAZOEFU NA WAHALIFU watukutu,hasa hawa WA kutumia silaha.

NI idea nzuri sn,
Maana zaman hawakuogopa jela, sahivi nao wanaogopa Sana kifo.

UJAMBAZI UMEPUNGUA SANA👍
 
Kipindi wenda zao wakimiminiwa vyuma hao watoto walikuwa wapi ili wao wasiathirike?
Maana ni lazima wangewafanya watoto kama kinga, au askari wetu waokozi walizama humohumo ndani ya nyumba au majamaa yalitimua mbio baada ya kubainika na hukohuko yakamiminiwa njugu?
 
Hongereni Polisi kwa kuokoa roho za hawa watoto. Watu wabaya wanaodhulumu uhai wa jamii yetu hawapaswi kuchekewa. Matukio kama lile la kibaha wanaofanya kwa njia yoyote inapaswa waondolewe kwenye jamii yetu kwa njia yoyote ile police watakayoona inafaa.

Katika matukio mengine Mtu anafanya uhalifu anaua mzazi anaacha watoto yatima. Yani hawa watu hawana huruma kabisa hawapaswi huonewa huru.
 
Amani iwe nanyi wapendwa

Wale watoto waliotekwa hatimaye wamepatikana lakini watekaji wameuliwa.

=====

View attachment 3229443

Wanafunzi wawili wa Shule ya Blessing Model School waliokuwa wametekwa na watu wasiojulikana Februari 5, 2025 jijini Mwanza wamepatikana huku watekaji wakipigwa risasi na kupoteza maisha baada ya kuonesha nia ya kutaka kuwashambulia maaskari wakiwa na silaha.

Akizungumza katika eneo la tukio Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema watoto hao wamepatikana wakiwa wamefichwa katika nyumba namba 8 iliyopo katika Mtaa wa Nyagoloboya Kata ya Nyegezi huku watekaji wakiwa humo.

Hata hivyo Kamanda Mutafungwa amesema baada ya maofisa wa jeshi hilo kuzingira nyumba na kuwataka watekaji watii amri walitoka wakiwa na silaha kama mapanga na rungu hali iliyopelekea kutumia risasi.
Roho mbaya tu kutoa uhai wa mwanadamu mwenzako. Wameua baba za watu, watoto wa watu waume za watu na kuacha familia zao zikibaki na huzuni na mateso.

Hii haikubaliki kabisa Serikali iwachukulie hao polisi hatua kali sana kwa umwagaji huu wa damu.

Wahalifu nao wana haki ya kuishi na kufarahia matunda ya maendeleo CCM imeiletea taifa letu.

R.I.P watekaji.

Nyau de adriz
 
Amani iwe nanyi wapendwa

Wale watoto waliotekwa hatimaye wamepatikana lakini watekaji wameuliwa.

=====

View attachment 3229443

Wanafunzi wawili wa Shule ya Blessing Model School waliokuwa wametekwa na watu wasiojulikana Februari 5, 2025 jijini Mwanza wamepatikana huku watekaji wakipigwa risasi na kupoteza maisha baada ya kuonesha nia ya kutaka kuwashambulia maaskari wakiwa na silaha.

Akizungumza katika eneo la tukio Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema watoto hao wamepatikana wakiwa wamefichwa katika nyumba namba 8 iliyopo katika Mtaa wa Nyagoloboya Kata ya Nyegezi huku watekaji wakiwa humo.

Pia soa > Mwanza: Watoto wawili wa Shule ya Blessing Model watekwa, wengine Wanne wanusurika

Hata hivyo Kamanda Mutafungwa amesema baada ya maofisa wa jeshi hilo kuzingira nyumba na kuwataka watekaji watii amri walitoka wakiwa na silaha kama mapanga na rungu hali iliyopelekea kutumia risasi.
Safi,polisi wamefanya la maana kuwaua, maana wangepelekwa mahakamani Wangeanza kutetewa na kuonewa huruma humuhumu Jf
 
Back
Top Bottom