Usiku wa kuamkia leo jijini Mwanza, kata ya Buhongwa kumetokea mauaji ya kinyama. Mauaji hayo yamefanywa leo saa kumi usiku. Watu wa tatu wa familia moja akiwemo Mtoto wa miezi saba (7) waliuwawa kikatili, kwa kunyongwa, ndani ya nyumba yao na watu wasiojulikana. Kwa habari za awali ni kwamba, watekelezaji wa mauji hayo walifanikiwa kuingia ndani ya nyumba hiyo pasi na kuvunja mlango. Licha ya nyumba ya marehemu hao kuzungukwa na nyumba zingine. Hata hivyo hakuna aliyefanikiwa kutoka ama kusikia wakati unyama huo ukiendelea. Kila aliyeulizwa alisema hajui chochote juu ya tukio hilo. Mama na mtoto wa miezi 7 walinyongwa, baba akachinjwa! Miili ya marehemu hao bado ipo ndani ya nyumba ikisubiri uchunguzi zaidi. Askari nao wamefika eneo la tukio na uchunguzi unaendelea.
Source: ITV Breaking News
My concern: Je, mtoto wa miezi 7 alikuwa na ugomvi na nani hadi na yeye kunyongwa?