Mwanza: Watu watatu wa familia moja waliuawa kikatili, kwa kunyongwa na watu wasiojulikana

Mwanza: Watu watatu wa familia moja waliuawa kikatili, kwa kunyongwa na watu wasiojulikana

Dah! huu ni unyama wa hatari, hao wa2 inabidi watafutwe hata kwa rimote controll!, na ikibidi wanyongwe na wao!


News hii ni mbaya sana Mkuu na haya yote hayatafanikiwa kutokana na ulegelege wa serikali iliyoko madarakani.
 
Wizara ya mambo ya ndani na jeshi lake siku hizi wapo bussy na mikutano ya vyama vya upinzani na kusoma taarifa za akina masogange usalama wa raia wamewachia raia wenyewe.
 
Wapi usalama wetu?
Unaweza kuta jamaa ameshindwa kulipa deni la elfu hamsini tu ndipo mdai akaamua kumtumia kisasi kazi
 
Huu ni ukatili wa hali ya juu sana watu wamekosa hata chembe ya huruma. UTU uko wapi?

Sent from my BlackBerry - jamiiforums
 
Ooh..... . .My God! Mpaka katoto ka miezi 7 kameuawa kwa hatia gani! Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali pema peponi, amina.
 
Usiku wa kuamkia leo jijini Mwanza, kata ya Buhongwa kumetokea mauaji ya kinyama. Mauaji hayo yamefanywa leo saa kumi usiku. Watu wa tatu wa familia moja akiwemo Mtoto wa miezi saba (7) waliuwawa kikatili, kwa kunyongwa, ndani ya nyumba yao na watu wasiojulikana. Kwa habari za awali ni kwamba, watekelezaji wa mauji hayo walifanikiwa kuingia ndani ya nyumba hiyo pasi na kuvunja mlango. Licha ya nyumba ya marehemu hao kuzungukwa na nyumba zingine. Hata hivyo hakuna aliyefanikiwa kutoka ama kusikia wakati unyama huo ukiendelea. Kila aliyeulizwa alisema hajui chochote juu ya tukio hilo. Mama na mtoto wa miezi 7 walinyongwa, baba akachinjwa! Miili ya marehemu hao bado ipo ndani ya nyumba ikisubiri uchunguzi zaidi. Askari nao wamefika eneo la tukio na uchunguzi unaendelea.

Source: ITV Breaking News

My concern: Je, mtoto wa miezi 7 alikuwa na ugomvi na nani hadi na yeye kunyongwa?

Buhongwa Buhongwa Buhongwa Buhongwa Buhongwa Buhongwa Buhongwa!!!!!! Jamani!
 
(W)aliofanya unyama huo naomba mungu (w)apate maumivu makali zaidi ya hao wa3 (w)aliowauwa siku yake ikifika na malaika wamkumbushe kwamba haya maumivu ndo hayo uliyowafanyia kina flani na flani na mtoto wao.
 
Unyama mwingine hata shetani anaweza kuogopa! Mbaya sana!
 
kamati iko bize na ku arrange mapokezi ya mfanyabishara wa kimataifa wa panadol bibie masogange..hayo mengine tutajua siku ingine
 
Usiku wa kuamkia leo jijini Mwanza, kata ya Buhongwa kumetokea mauaji ya kinyama. Mauaji hayo yamefanywa leo saa kumi usiku.

Watu wa tatu wa familia moja akiwemo Mtoto wa miezi saba (7) waliuwawa kikatili, kwa kunyongwa, ndani ya nyumba yao na watu wasiojulikana. Kwa habari za awali ni kwamba, watekelezaji wa mauji hayo walifanikiwa kuingia ndani ya nyumba hiyo pasi na kuvunja mlango.

Licha ya nyumba ya marehemu hao kuzungukwa na nyumba zingine. Hata hivyo hakuna aliyefanikiwa kutoka ama kusikia wakati unyama huo ukiendelea. Kila aliyeulizwa alisema hajui chochote juu ya tukio hilo. Mama na mtoto wa miezi 7 walinyongwa, baba akachinjwa!

Miili ya marehemu hao bado ipo ndani ya nyumba ikisubiri uchunguzi zaidi. Askari nao wamefika eneo la tukio na uchunguzi unaendelea.

Source: ITV Breaking News

My concern: Je, mtoto wa miezi 7 alikuwa na ugomvi na nani hadi na yeye kunyongwa?

Habari zaidi zimeeleza kuwa muuwaji anafahamika, ni fundi wa kujenga nyumba na alishawahi kumjengea nyumba marehemu siku za nyuma sasa marehemu alimuita huyo jamaa ili kufanya mipango ya kumjengea nyumba nyingine, hivyo alikuwa ni mgeni wao.

Inasemekana binti wa marehemu akiwa amelala chumbani kwake usiku alisikia kile kichanga kikilia na baada ya muda huyo mgeni akampigia hodi huyo binti na kumkabidhi hicho kichanga ili akibembeleze, hata hivyo kiliendelea kulia kwa muda mrefu na mgeni akangongea hodi tena huyo binti na akakichukua hicho kichanga kana kwamba anaenda kukibembeleza au kukirudisha kwa wazazi wake, kumbe muda huo wazazi wote wawili walishauawa. Binti akasikia kichanga kimenyamaza nae akaendelea kulala usingizi, kumbe kichanga kilikuwa kimya baada ya kuuawa.

Huko baadae binti anataka atoke akakuta mlango kafungiwa kwa nje, akarudi kulala. asubuhi tena alipotaka kutoka mlango ukawa bado umefungwa kwa nje akaomba msaada dirishani wakaja watu na kukuta maiti zote tatu ilhali mgeni alishatokomea.

habari hii nimeisikia wapo redio asubuhi ya leo.
 
Kama huyo muuaji alikuwa ni fundi kaitwa na familia hiyo aje awajengee nyumba,kuna possibility familia ilikuwa na kahela,jamaa atakuwa amepiga kahela amesepa. #najaribukujengapicha #

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Kama huyo muuaji alikuwa ni fundi kaitwa na familia hiyo aje awajengee nyumba,kuna possibility familia ilikuwa na kahela,jamaa atakuwa amepiga kahela amesepa. #najaribukujengapicha #

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

Hijajulikana maana wakubwa wa familia ndo hao wameuawa.
 
Someone is behind this sio wizi tu hawawezi kuuwa mpaka kichanga hakina hata kosa lolote
Sometimes kwenye visasi huwa wanahakikisha hata mtoto habaki ili asije lipiza kisasi.

Hii dunia ya leo sio ya jana, unyama umezidi wema.

INATISHA SANA
 
Back
Top Bottom