Mwanziva afanya Kikao Kazi na Makatibu Hamasa Mkoa wa Dar es Salaam

Mwanziva afanya Kikao Kazi na Makatibu Hamasa Mkoa wa Dar es Salaam

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
MWANZIVA AFANYA KIKAO KAZI NA MAKATIBU HAMASA MKOA WA DAR ES SALAAM

Picha za Matukio mbalimbali wakati Katibu Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa Cde. Victoria Charles Mwanziva, akiongoza Kikao Kazi na Makatibu Hamasa wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi wa Mkoa wa Dar Es Salaam- Eng Ally Ummiy- katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya UVCCM Taifa Upanga Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Desemba, 2022.

Katika kikao hicho wamejadili mambo mbalimbali yenye kuendelea kuwa na mchango mkubwa katika Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM na Chama Cha Mapinduzi na (CCM) kwa ujumla.

Aidha Cde. Mwanziva, amewasihi makatibu hao kuwa mstari wa mbele katika kuwaunga mkono katika utekelezaji wa majukumu yao viongozi wakuu wa Jumuiya wakiongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Ndg. Mohamed Ali KAWAIDA (MCC), Makamu Mwenyekiti UVCCM Ndg. Rehema Sombi Omary (MNEC) na Katibu Mkuu UVCCM Ndg. Kenani Kihongosi (MNEC) katika kuendeleza Jumuiya Imara kwa maslahi ya Vijana wa Taifa letu pamoja na kukisaidia Chama cha Mapinduzi kwa kuendelea kusemea Utekelezaji wa Ilani ya CCM inavyotekelezwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

indexcvbgh.jpg


indexdfrtycxvfg.jpg


indexasdfg.jpg



#KaziIendelee
#AlipoMamaVijanaTupo
#2023KaziItaendelea
#2022TunavukaKwaKishindo
 
Back
Top Bottom