Salaam, Shalom!!
Usishangazwe na salamu, Kuna Wana wa Mungu wamenitoroka, nawatafuta niwarudishe nyumbani. Turudi kwenye mada.
Katika kuishi kwangu nimewahi kuona aina mbalimbali za walevi, Kwa nje unaweza kudhani wanapendana sana,
Mlevi mmoja alisafiri Kwa pikipiki karibia kilometa Tano, alipofika nyumbani Kwa Rafiki yake , aligonga hodi, siku hiyo ilikuwa jumapili, alipofunguliwa mlango na shemeji yake, alimsalimia Kwa bashasha na kumuuliza ikiwa rafikiye yumo ndani,
Shemeji mtu alisema yumo ndani, aliomba aitiwe, shemeji mtu kuona mgeni amebeba mfuko mdogo ameukunja kushika mikononi, alidhani ni zawadi imeletwa, akamwambia, shemeji nikupokee,
Ndugu yule akagoma kupokelewa mfuko Ule na kudai, ameleta chakula kidogo ambacho angependa ashiriki na Rafiki yake pekee wakiwa wawili,
Basi shemeji mtu akamuitia rafikiye, alipotoka wakasalimiana, ndugu yule akadai waende pembeni kidogo wakae, Kuna chakula kidogo angependa ashiriki na Rafiki yake, ndugu yule akaona Leo imekuwaje, Rafiki yangu atoke kwake zaidi ya kilometa 5 aje asubuhi yote hii,kitakuwa chakula kizuri,
Mtu yule alipofungua mfuko Ule ,kuangalia ndani, kumbe Kuna POMBE kwenye chupa nyeupee kubwa kama maji, alipoulizwa chakula Kiko wapi, akadai pombe ndiyo hicho chakula kizuri,
Mke yule Kwa ndani alibaki anacheka mbavu Hana akishangazwa na aina hii ya urafiki.😀
KWANINI URAFIKI WA WALEVI NI WA MASHAKA!!
1. Ukitaka kujua urafiki wa walevi ni WA mashaka,
Mwambie mlevi mwenzio saizi, kwamba umefukuzwa na mwenye nyumba, Kodi imeisha, waombe wakusaidie unambie wamekujibu nini!!
2. Washirikishe walevi wenzio kuwa Leo hujapata chochote kazini, waombe wakupe angalau 20,000/ Ili familia Yako ikale, uniambie wamekujibu nini!!
3. Wambie hivi, mtoto wangu amefukuzwa shule Hana ada, waombe wakukopeshe pesa kidogo uone ikiwa watakukopesha.
4. Wambie hivi, nyumba Yako zimepungua bati mbili tu, wakukopeshe pesa Ili upaue, uhamie Kwako uone watakujibuje!!
Sasa ikiwa urafiki wa WALEVI ni katika ulevi kuteketeza pesa katika anasa pekee, urafiki huo wa nini sasa!!!
Ikiwa unapenda uachane na marafiki zako walevi wanaokutoa kwenye njia ya mafanikio na kukupoteza,
Fuatisha Sala hii,
EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, ULEVI USINISHINDE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. AMEN
Karibuni 🙏