Unaweza kusema labda kwa vile mtu umepambana umetajirika basi utakuwa mbali na kero za serikali kumbe tabu iko palepale
Miundombinu inajengwa leo kesho inafumuliwa tena ili ijengwe tena keshokutwa almradi tu mtukere watumiaji wa barabara kwa ujenji usio isha
- Unakimbia kero ya kupanda mwendokasi kwa kununua magari binafsi lakini unakutana na kero ya barabara mbovu, mashimo na foleni
- Unakimbia kero ya kupanga unaamua kujenga nyumba eneo zuri la makazi unakutana na kero ya mtu kafungua kanisa linapiga kelele usiku kucha na serikali iko kimya
- Unaamua kufungua biashara unakutana na wasimamizi wa sheria ambao hawafuati sheria kabisa
- Unaamua kugombea unakutana na wagombea wenzio ambao hawategemei ushindi kupitia sanduku la kura
- Unaamua kuchangia mfuko wa hifadhi ya jamii ili ukistaafu upate mafao, lakini ukistaafu wanakwambia watakupa kidogo kidogo mafao yako
- Unaamua kwenda kutafta haki mahakamani unakutana na DPP ambaye hana nia ya kuendelea na kesi anaifuta na huna cha kumfanya
- Unaamua haya basi ngoja nitulie nyumbani tu unakutana tena na wakata umeme, kata washa kata washa yaani kero extremely
Miundombinu inajengwa leo kesho inafumuliwa tena ili ijengwe tena keshokutwa almradi tu mtukere watumiaji wa barabara kwa ujenji usio isha