Hamna kitu kama hicho..labda Rais tu ndo hana kero..Mo Dewji tayari yule - alipotezwa akarudi yuko kimya, yule tajiri Telegram..France wamekamata juzi wakamuweka rumande kwa muda .
Matajiri wa hapa Bongo kutwa kucha kujipendekeza kwa serikali au kujiunfa CCM hata kama hawapendi ili mambo yao yaende - kero zote hizi.
Roman Abramovich - tajiri wa Chelsea - kalazimishwa kuuza timu aipendayo, wamekamata mali zake n.k.
Dangote juzi hapa alikua analalamika kama mtoto hana cha kufanya - kajenga refining kubwa Nigeria then serikali inaanza kumuhujumu.
Trump tajiri - billionaire - ex US president, current mgombea republican - walikikosa kichwa kwa risasi by milimetres, juzi hapa wamemkosakosa tena..
Mama Samia juzi kaongea kwa jazba sababu ya kero - watu wanaongea mitandaoni mpaka wanawezakupa heart attack..huyu ni Rais wa nchi, tajiri pia kw sasa.
Mifano ni mingi.
Achilia mbali kero za kuombwa bahasha, TRA.n.k
KERO ZIKO PALEPALE TU..tena ukiwa tajiri ndo hatari zaidi..