Mwanzo nilijua ukiwa tajiri basi umejiepusha na kero ndogo za serikali kumbe tabu iko palepale

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Unaweza kusema labda kwa vile mtu umepambana umetajirika basi utakuwa mbali na kero za serikali kumbe tabu iko palepale

  • Unakimbia kero ya kupanda mwendokasi kwa kununua magari binafsi lakini unakutana na kero ya barabara mbovu, mashimo na foleni
  • Unakimbia kero ya kupanga unaamua kujenga nyumba eneo zuri la makazi unakutana na kero ya mtu kafungua kanisa linapiga kelele usiku kucha na serikali iko kimya
  • Unaamua kufungua biashara unakutana na wasimamizi wa sheria ambao hawafuati sheria kabisa
  • Unaamua kugombea unakutana na wagombea wenzio ambao hawategemei ushindi kupitia sanduku la kura
  • Unaamua kuchangia mfuko wa hifadhi ya jamii ili ukistaafu upate mafao, lakini ukistaafu wanakwambia watakupa kidogo kidogo mafao yako
  • Unaamua kwenda kutafta haki mahakamani unakutana na DPP ambaye hana nia ya kuendelea na kesi anaifuta na huna cha kumfanya
  • Unaamua haya basi ngoja nitulie nyumbani tu unakutana tena na wakata umeme, kata washa kata washa yaani kero extremely
Yaani unawaza sijui shida iko wapi, tulikosea wapi! Ibada kama zote lakini viongozi hawabadiliki!

Miundombinu inajengwa leo kesho inafumuliwa tena ili ijengwe tena keshokutwa almradi tu mtukere watumiaji wa barabara kwa ujenji usio isha
 
Rev Hananja anakuambia kama hutaki changamoto nenda Kinondoni Makaburini
 
Ndio maana nimemwambia jamaa ila kagoma
Ila kina rostam ,mo ,GSM , bakhresa hao wote wanasafishiwa njia
 
Duniani ni mateso
 
Shida ni kuwa Ngozi Nyeusi haijiwezi yenyewe, hasa katika Uongozi na usimamizi (Management)

Ili Mbantu aendelee anamhitaji Mtu mweupe amzibue akili na kumsimamia kwa ukaribu ili asiharibu tena

Kwa Mfano hizo kero ulizoziorodhesha kwa serikali sio tatizo kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…