Mkuu Rakims
Kwanza nashukuru kwa somo lako
hasa kuhusu Meditation. Nimeelewa na leo nimefanya meditation ya kukagua mwili wangu na yafuatayo ni matokeo yake.
Nilikuwa nimelala kama pozi langu la
kumeditate. Wakati nameditate nilikuwa nataja jina la Mungu kwa mujibu wa iman yangu baadae
nikajikuta nageuza kichwa changu upande wa kulia. Kisha mkono wangu wa kulia ukaanza kunyanyuka ukapanda hadi kifuani kisha ukarudi nilipokuwa nimeuweka baada ya kama sekunde tatu kichwa kikageukia upande wa kushoto nikajikuta nainua mkono wa kushoto hadi kifuani na kuurudisha ulipokuwa. Baada ya kama sekunde kumi nilikigeuza kichwa
kilipokuwa na kuanza kutingisha kama mtu mwenye pepo. Kilipotulia mikono
yote ikaanza kuinuka hadi kifuani ukitangulia mkono wa kushoto na wakulia juu yake. Baadae nikajikuta natoa mkono wa kulia kifuani na kuupeleka kama mtu anayetaka
kupokea kitu kisha mikono yote ikarudi
mahali ilipokuwa.
Naomba muongozo wako hapo je niko
sahihi kwa mtokeo hayo?