Mwanzo wa meditation

Mwanzo wa meditation

Hongera kwako mkuu Rakims kwa somo zuri, kwani kupitia uzi huu nimejikuta navutiwa ku meditate.
Shida ni kwamba nimejaribu kufuatilia mwanzo hadi mwisho ktk maelekezo na hata kupitia maswali walio uliza wadau lkn sijaona sehemu ulio fafanua kuhusiana na hicho kidole ambacho unatumia pindi utaamua kutoka.
Unagonga wapi chini au unagonga sehemu yoyote ya mwili wako?
Na unagonga mara ngapi?
 
unaliza kama vile unaita au kustua mtu mkuu,
 
Lete aya ya hayo mambo unayoandika.
Imeandikwa wapi katika vitabu vya Mungu ?
Au ndo umetoa kwa huyo unayemwita mungu wako ?
Unajua kutofautisha maana ya Mungu na mungu ?
Maana sehemu zote umemwandika mungu unayemfahamu wewe.
Tutajie hapa huyo mungu wako unayekutana naye wakati wa meditation ni nani ?
Anaitwa nani ?
Andiko lako linamtaja mungu badala ya Mungu sisi wenye udadisi tunapata wasiwasi kuwa, huandiki kwa bahati mbaya na unataka kuwapeleka watu kusikotakiwa.
 
Mmoja wenu atakuja apotelee humo..mi nawashauri mtumie rucids dream ni afadhali kuliko iyo iyo imepoteza watu kibao.
 
Eti kwa wakristo meditation ni dhambi au LA? Naombeni maandiko
Meditation ya kutafari Neno la Mungu lililoko kwenye Biblia ya Kikristo sio dhambi.

Ila hiyo meditation nyingine ni DHAMBI KUBWA.
Inahusisha utawala wa GIZA moja kwa moja.
Inamshirikisha Shetani katika kuifanikisha, na mtu unaondoka Kiroho kutembelea himaya yake, wakati wa kumeditate, wengi wanafia huko huko wakati wana Meditate.
Siri hiyo hamwezi kuambiwa kwani ni mpango maalum wa hila wa Shetani.

Mimi nakusaidieni tu, msijaribu mazoezi msiyoyajua undani wake.
Mungu aliyekuumba hajawahi kukuambia ufanye hivyo alijua hasara yake kwako.
Mambo yote mazuri ya kufanya, Mungu ame ruhusu kuyafanya.
 
Back
Top Bottom