Habari wadau. Katika njia za kufanya meditation (tunaambiwa tuseme concentration)Kuna mojawapo ya kutumia ukuta.
Yaani unatulia katika chumba chenye mwanga then unau-face ukuta kwa kuusogelea ukiwa umekaa kwenye kiti.(relaxing).
Unaanza kuutazama kwa kumakinika(concentrating)huku ukipumua taratibu.
Baada ya muda utaanza kuona body in vibrate kwa mbali,kijasho hivi then zinatokea rangi rangi..Kama zinakuja na kuondoka. Ukianza kuzifikiria tu zinapotea.
Nilifanya hivyo usiku wa kuamkia leo,kwenye ukuta mweupe ila Cha ajabu nilikuwa naziona rangi ya njano na zambarau,hasa hasa njano znakuja Kama rainbow vile,,,zinamove na kupotea then zinarudi tena....raha sana. Baadae nikawa sizioni(nafikiri baada ya kuanza kuzifikiria-zinavutia ujue Kama tv hivi).
Nililianza zoezi saa 9:55 za usiku,nikamaliza saa 5:12. Baada ya kumaliza nilijiskia fresh sana,,nasisitiza nilijiskia poa sana kimwili na kiakili. Japo sikwenda mbali zaidi.
Swali....nini changamoto za hii style ya kuangalia ukuta hasa hasa kwa beginners?
Nawasilisha