MWAUWASA acheni kutumia mo Mirongo kupeleka maji machafu Ziwani.

MWAUWASA acheni kutumia mo Mirongo kupeleka maji machafu Ziwani.

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739

Licha ya umuhimu wa mto huo uliopo ndani ya Jiji la Mwanza, lakini ni kituko cha kila siku kuona uko hatari kwa uchafu wa mazingira na kusababisha madhara ya kiafya na kimazingira kwa watu wanaoutumia kwa shughuli mbalimbali. Hali hiyo imesababishwa na kuongezeka kwa shughuli za binadamu ikiwemo kulima pembezoni mwa mto huo na utupaji wa taka.
Mwanza-town.jpg

Wakazi wengi wa mwanza tumeshuhudia taka ngumu ikiwemo chupa za plastiki zikiwa zimetuama kando ya kingo za mto huo ambazo kama mvua ikinyesha zitasukumwa na maji kuingia ziwani. Lakini kwa watumiaji wa barabara ya kueleka mjini via njia ya kliniki jirani ya mahakama ya Mwanzo, wamekuwa wakikutana na harufu kali ya kinyesi, tumewahi kujiuliza uchafu huo umetoka wapi?
mto mirongo.jpeg

Wakazi kadhaa ndani ya Jiji la Mwanza ambao wapo jirani na mto huo mara kadhaa wamekuwa wakiona uchafu mkubwa ambao ni uchafu wa aina mbalimbali ndani ya mto huo hali inayosababisha uchafu kujikusanya na kuziba kwenye kingo za mto. Makopo, mifuko ambayo ndani ina taka, kitu hiki kinaweza kuathiri afya zao na kusababisha magonjwa kama kipindupindu.

Hatari zaidi ni kwenye kipindi cha mvua ambapo mto unapofurika huzoa taka hizo na kwenda kuzimwaga ziwani, kuwa wakati mwingine uchafu huo huingia kwenye makazi na kuhatarisha afya za watu. Wapo wengine mashimo yao ya choo yakiwa yanatazama kwenye kingo cha mito, na pale mua inaponyesha basi na wao wanafungulia uchafu wao.
mto mirongo 12.jpeg

Utakuta taka hizo zote zinaingia ziwani wakati huo wapo wanaotumia maji hayo kunywa, kupikia na kuongea hivyo kufanya afya za watu wanaotumia maji ya ziwani Nyanza kuwa hatarini. Wakazi wengi wamesema kitendo cha mto huo kuendelea kuchafuliwa kunaweza kusababisha magonjwa yakiwemo ya mlipuko kwa wana Mwanza.
Jambo la ajabu ni kuwa MWAUWASA nao badala ya kuishi kwenye maono na dira yenu ya kutoa huduma bora kwa wananchi, mnafanya vitu vya ajabu sana, Mkurugenzi Neli Msuya upo ofisini na haufahamu kama kuna sehemu mnaruhusu maji machafu kuingia kwenye mto Mirongo na kuyaelekeza kwenda Ziwani?
Mirongo-Mwanza.jpg

Kama hauamini siku inyeshe mvua basi pita maeneo ya Kemondo kama unaelekea Airport aisee kuna harufu kali sana katika daraja hili. Ni ajabu ila sio kitu kigeni kuona wanafanya haya tena bila hata aibu wala soni. Dhamira yenu ni kwamba mnatimiza azma ya Serikali ya kumpatia mwananchi huduma bora, endelevu na yenye kutosheleza, huku Mamlaka hii ya Maji ikiendelea kushirikiana kwa karibu na wadau wa Maendeleo kutoka Nchi mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha azma hiyo inafikiwa kikamilifu. 2020 timu maalumu kutoka Benki Kuu ya Dunia ya CIWA walifanya utafiti wao na kuonesha hofu kuwa uchafuzi wa mazingira mkubwa sana ndani ya Ziwa Nyanza.
mwanza-1.jpg

Ni kwamba hakuna ushirikiano baina ya mamlaka hizi au hawajui kuwa kuna makubaliano na mikataba ya kimazingira tumepata kusaini na mashirika kadhaa ya mazingira. Mradi wa Nile Cooperation for Climate Resilience (NCCR) pamoja na mfuko wa maendeleo wa Korea Green Growth Trust Fund wanafanya kazi kubwa sana kuzuia uchafuzi wa mazingira lakini ni kama tunakwenda hatua kumi mbele kisha tunarudi hatua hamsini nyuma.
large-1713336439-HUMBURG.jpg

Ni kweli kwamba mto huo unachafuliwa na watu wanaoishi kando na mto huo pamoja na wafanyabiashara, kinachofanyika hadi sasa Serikali inajitahidi kusafisha ili kudhibiti uchafu huo usiingie ziwani na kuzalisha magugu maji.
Mwanza-erial-2.jpg

Afisa Misitu na Mratibu wa shughuli za Mazingira Mkoa wa Mwanza upo wapi Mkuu!? Nikwamba hauoni yanayoendelea kwenye mto huu? Kuanzia kwa Aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispa ya Ilemela Kibamba Kiomoni, mpaka sasa Bi Ummy Wayayu Mkurugenzi wa sasa wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Je yanayoendelea hapa yanatokea mbinguni au. Mzee wangu Kiomoni Kibamba hujawahi kupita maeneo haya na kuona hili jambo? MWAUWASA acheni kuelekeza uchafu huu nje nje! Tafuteni namna nzuri ya kupeleka uchafu huu! Hayo maji yanatumika na watu wengi!​
Sio kwa ubaya! Sio kwa ubaya!
 
Back
Top Bottom