KERO Responded MWAUWASA imekuwa jipu lisilotumbulika, Nyamagana - Mwanza ni mwezi sasa hatuna maji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

ANT DRUGS

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2013
Posts
5,578
Reaction score
7,055
Ni mwezi sasa Wilaya ya Nyamagana, maeneo ya Igoma, Machinjioni, Muhandu-Kisiwani, hatuna maji. Binafsi nimechukua hatua ya kuwapigia simu, wanasema machine ya ku-pump maji ya Mabatini imeharibika.

Nikawauliza mna mpango gani? Wakasema hiyo ni changamoto. Yaani kiufupi na wao wanaonekana hawana cha kufanya. Hii MWAUWASA imekuwa jipu lisilotumbulika.

Wanafanya business as usual, Wananchi mitaani wanabaki kumlaumu Rais, ilhali viongozi wangetatua hilo tatizo wenyewe. Juma Aweso, ulikuja ukabadili viongozi wa MWAUWASA, uliowaweka nao ni sifuri bin sifuri, nothing they are doing.

Ufafanuzi wa MWAUWASA ~ Hoja ya maji Nyamagana kukosa, MWAUSAWA yasema "Huduma inaendelea kila wiki kadri migao inavyotekelezwa"
 
Ni mwezi sasa Wilaya ya Nyamagana, maeneo ya Igoma, Machinjioni, Muhandu-Kisiwani, hatuna maji. Binafsi nimechukua hatua ya kuwapigia simu, wanasema machine ya ku-pump maji ya Mabatini imeharibika.

Nikawauliza mna mpango gani? Wakasema hiyo ni changamoto. Yaani kiufupi na wao wanaonekana hawana cha kufanya. Hii MWAUWASA imekuwa jipu lisilotumbulika.

Wanafanya business as usual, Wananchi mitaani wanabaki kumlaumu Rais, ilhali viongozi wangetatua hilo tatizo wenyewe. Juma Aweso, ulikuja ukabadili viongozi wa MWAUWASA, uliowaweka nao ni sifuri bin sifuri, nothing they are doing.
Tanki kubwa la maji ya kutoka victoria lipo Tabora halijajaa. Likijaa yataachiwa kuja Mwanza.
 
Hii mamlaka bora ifutwe kabisa, haina tija yoyote, hayo maeneo uliyotaja yamekuwa sugu kwa ukosefu wa maji,tunateseka sana sisi watumiaji wa maji
 
Bora hata igoma mgao upo ila si mkali ukilinganisha na hapo machinjion..kuna muda hadi machinjio yanasimama kwa ukosefu wa maji
 
Mimi huwa sielewi kabisa mwanza kila kikianza kiangazi tu, maji yanakuwa ya shida sasa unashindwa kuelewa kabisa
 
Yan hata mimi imefikia kipindi nawaza kuhama huu mkoa sababu ya tatizo la maji lisiloisha na ufumbuzi haupo mpaka sasa mamlaka hawana majibu
 
Back
Top Bottom