Mwekezaji abaomoa nyumba ya Mzee wa miaka 90, familia yalala nje

Mwekezaji abaomoa nyumba ya Mzee wa miaka 90, familia yalala nje

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Familia ya Mzee wa Mila afahamikae kwa jina la Chacha Wasinyo Changu (90), Mkazi wa Kitongoji cha Mirimisi, kijiji cha Mrito, Wilaya ya Tarime, inalazimika kulala nje kwa siku ya 5 mfululizo baada ya makazi yao kubomolewa.

Tukio hilo linadaiwa kufanywa na Samweli Ngocho, Mkazi wa Kijiji cha Kerende, Nyamongo, anayetajwa kuwa ni mwekezaji wa uchimbaji wa madini ya marumaru aliyeingia katika eneo hilo.

Familia hiyo imelalamikia tukio hilo na kuiomba Serikali iingilie kati, ikiwemo Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele, wakisema ubomoaji huo umeacha maumivu, mshangao na maswali mengi si kwa familia pekee bali pia kwa Wanakijiji na viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Mrito.

Akizungumza na Jambo TV, Mzee Wasinyo amesema siku ya tukio alifika nyumbani na kukuta zoezi la ubomoaji likiendelea, ambapo mifugo yake ikiwemo Kuku (na maya), pamoja na Vyombo vya ndani, vilifukiwa bila nafasi ya kuokoa chochote.

Mzee Wasinyo, ambaye ni Mume wa wake Watatu na Baba wa Watoto zaidi ya 20, amesema amekaa katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka 32, akieleza kuwa hapo awali eneo hilo lilikuwa pori lililotumika kujificha wezi wa mifugo, bila kuwa na mtu yeyote.

Jambo TV imezungumza pia na Viongozi wa Kijiji waliokuwepo wakati wa tukio hilo, wakiwemo mwenyekiti wa zamani aliyehudumu kuanzia mwaka 2009 hadi 2014 pamoja na mwenyekiti wa sasa aliyeingia madarakani mwaka 2024.

Viongozi hao kwa pamoja wamesema hawamtambui Samweli Ngocho, wakidai kuwa aliingia kijijini hapo kwa njia za ulaghai na vibali vya kughushi bila kushirikisha uongozi wa kijiji.





Chanzo: Jambo TV
 
Ndiyo MAANA mbunge msukuma alimpiga ngumu yule mwekezaji kanjanja.
 
Watu wana mambo ya kipumbavu huyo jamaa atoe fidia na ajengee familia upya
 
Hao wenyekiti wa kijiji wachapwe viboko wanatoaje majibu ya hovyo namna hiyo yasiyokuwa na mantiki.
 
"Mzee Wasinyo, ambaye ni Mume wa wake Watatu na Baba wa Watoto zaidi ya 20, amesema amekaa katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka 32, akieleza kuwa hapo awali eneo hilo lilikuwa pori lililotumika kujificha wezi wa mifugo, bila kuwa na mtu yeyote".

Huyu mzee ana uhakika gani kuwa eneo halikuwa la mtu? Ninashauri usiingie sehemu kwa sababu umeona tu ni pori ukajidanganya kuwa halina mtu. Huyo mzee alitakiwa apite ofisi ya kijiji ili apewe eneo kwa kufuata utaratibu. Hivyo alivyoingia alikuwa tu mvamizi.
 
Watoto ishirini. Na wajukuu hapo wanashindwa kulinda nyumba ya mzee wao? Zamani ukiwa na watoto kibao ilikuwa ni ulinzi.
 
Back
Top Bottom