KERO Mwekezaji kachukua viwanja vyangu vinne Kijiji Cha Msufini Kidete – Mkuranga, Pwani, kila ninapoenda hakuna msaada

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mnamo Desemba 7, 2022, nilifanya uamuzi wa kuwekeza kwenye ardhi kwa kununua shamba lililopo Kijiji cha Msufini Kidete, Kata ya Mbezi, Wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani.

Ununuzi huu haukuwa wa mitaani tu; nilifuata taratibu zote za kisheria na za kiserikali. Nilisaini mkataba halali mbele ya Serikali ya Mtaa, tukiwa na mashahidi wote wanaotakiwa, na picha za tukio zikachukuliwa kama ushahidi. Mpaka leo, nyaraka zote, mikataba, na ushahidi wa picha ninao mikononi mwangu.

Hata hivyo, miaka miwili baadaye (mwaka 2024), mambo yalianza kubadilika. Mwekezaji mmoja kutoka nje aliwasili eneo hilo na kuanza kununua eneo kubwa la ardhi kwa ajili ya mradi wa ujenzi. Kwa masikitiko makubwa, eneo alilopewa linajumuisha na viwanja vyangu vinne vilivyopo ndani ya shamba langu la awali.

Mwekezaji huyo aliuziwa maeneo yangu bila ridhaa yangu wala taarifa yoyote kwangu! Sijawahi kuuza kiwanja hata kimoja. Kinachoshangaza zaidi, mikataba anayotumia mwekezaji huyo inaonyesha viwanja vyangu vilikuwa vinamilikiwa na watu wengine kabisa ambao walijitokeza na kumwuzia. Katika mikataba hiyo ya mwaka 2024:

Hakuna hata shahidi mmoja aliyeshiriki wakati mimi nanunua ardhi hiyo mwaka 2022 na hakuna kiongozi wa mtaa aliyenishuhudia nikinunua aliyewahi kuhusishwa.

Swali langu kuu linabaki kuwa: Inakuwaje mtu anauziwa kiwanja na watu ambao siyo wamiliki halali wa eneo hilo?

Nilipojaribu kufuata sheria na kuwasilisha malalamiko yangu katika ngazi husika za Serikali, badala ya kupata haki, nimekutana na ukuta. Viongozi na mamlaka nilizozitegemea zinaonekana "kucheka vizuri" na mwekezaji huyo na kunigeuka kabisa. Mkataba wangu halali ni wa mwaka 2022, huku wa mwekezaji na matapeli hao ukiwa wa mwaka 2024, lakini bado haki yangu inakanyagwa.

Nimepambana kila kona kutafuta msaada bila mafanikio. Inasikitisha sana kuwa katika nchi yetu, unapokuwa huna nguvu ya kiuchumi, walioshika fedha ndio wanaopewa kipaoumbele na kupendelewa. Sikatai maendeleo wala uwekezaji lakini hivi maendeleo lazima yaje kwa kutukandamiza na kutudhulumu sisi wananchi wanyonge?

Mimi nimeamua kujitokeza na kupaza sauti yangu leo, lakini nyuma yangu kuna wananchi wengi wanyonge waliodhulumiwa na kuumizwa, lakini hawana pa kusemea wala kuhemea. Naomba mamlaka za juu zitazame swala hili na kurejesha haki yangu.

​
 
Huko Mkuranga kuna changamoto sana kuhusu migogoro ya ardhi hasa ya Wawekezaji wanaowadanganya wananchi wa hali ya chini.
 
Serekali yetu, ifanye juu chini iwape viwanja wananchi hao sehemu zingine kwa ukubwa ule ule wa maeneo yao!.....
N.b,iwafidie endapo kama kulikuwa na mazao.
 
wenzako wananiungisha mapanga yaliyonolewa kabisa kwa bei chee sana,...karibu ujipatie nawe pia
 
Kwa akili yangu, ningetafuta nauli niende sumbawanga nikanunue radi tu. Ni kugonga radi hadi washtuke.
 
Back
Top Bottom