Mwekezaji Mo Dewji, Mwenyekiti Nkwabi, Bodi nzima na wana Simba SC wote tuhakikishe CEO Magori anaendelea kuwa CEO Msimbazi

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Natambua kuwa Yeye kama Yeye alishasema kuwa anang'atuka hapo kama CEO baada ya Miezi Sita ili apatikane CEO mwingine na kama Simba SC itahitaji Mchango wake basi imtumie katika mambo makubwa na mazito hasa ya Kimaamuzi ambayo Yeye kwa Hadhi yake na Uzoefu wake mkubwa anadhani ataitendea Simba SC makubwa.

Kwa muda mfupi tu ambao nimeitathmini Simba SC ikiwa chini ya Utendaji wa CEO Magori nimegundua kuna mambo mengi sana ya Kimaendeleo yametokea na Mafanikio makubwa yamepatikana hasa akishirikiana vyema kabisa na Mwekezaji Mo Dewji na Mwenyekiti Nkwabi hivyo nashawishika leo hii kusema kama si kuomba kwamba huyo CEO Magori aendelee kuwepo hapo na aongezewe Package yake Kimaslahi lakini pia ajumuishwe katika sehemu muhimu za Kimaamuzi na Kiuwekezaji ndani ya Klabu.

Simba SC tukikubali CEO Magori aondoke hapo tutakuwa tumetupa Jiwe la Thamani kubwa sana ambalo mpaka kuja kulipata tena itatuchukua muda mrefu. CEO Magori ameweza kuwa Kiungo bora kabisa kati ya Wachezaji, Benchi zima la Ufundi na Uongozi mzima wa Klabu na kitu kizuri Kwake ni kwamba ametokea Kupendwa na Kukubalika mno na Wachezaji wa Simba SC ambao amekuwa akiishi nao si tu kama Rafiki bali kama Baba kitu ambacho kimeweza kusababisha Mshikamano mkubwa ambao ulipelekea Ufanisi hadi Timu ikapata Mafanikio yale iliyoyapata.

Sina uwezo wa Kubadilisha Mawazo au Maamuzi ya CEO Magori na wala sina uwezo wa Kuupangia Uongozi mzima wa Simba SC chini ya Mwekezaji Mkuu Mo Dewji na Mwenyekiti Nkwabi pamoja na Bodi yao nzima ila nawaomba sana wafanye kila waliwezalo ili hata kama itabidi Kuundwe Cheo Kipya cha Juu ndani ya Simba SC ili CEO Magori akiongoze basi hilo lifanyike haraka au kama kuna uwezekano wa Kumpa Majukumu mengine makubwa ya Kiutendaji ili mradi tu huu Mchango wake mkubwa alioutoa Klabuni uendelee na Simba SC izidi Kufaidika nae basi hilo lifanyike upesi

Kwa Simba SC ya sasa na huku ikiwa imeanza Kujijenga Kiuwekezaji inamuhitaji sana CEO Magori hivyo tusimpoteze. Kwa wale walio karibu au jirani na Uongozi wa Juu wa Simba SC nitawashukuruni kama huu Uzi wangu mtaufowadi Kwao moja kwa moja au hata kwa Msemaji na kama Wahusika wote wako hapa JamiiForums kitu ambacho naamini wapo hivyo watautathmini na wataufanyia Kazi ila nitafurahi mno hata kama CEO Magori atamkabidhi Mtu mwingine hicho Cheo chake basi na Yeye pia aendelee kuwepo katika sehemu ya Mafanikio yajayo ya Klabu hasa Kiutendaji na katika Kipindi hiki cha Uwekezaji ambacho Simba SC imeingia rasmi.
 
Magori huyo ni mbeba mikoba ya MO, alifukuzwa NSSF kwa ufisadi, anashirikiana na MO kuitapeli simba, zile pesa za CAF hazijulikani zimeenda wapi, aondoke mapema kabla hajaishia jela!

Watu wamewekeza pesa ili faida ipatikane na wai re-invest tena,kununua wachezaji wapya na kuendeshea club,we unauliza as if ulichangia,we kazi yako ni kushabikia team acheni uswahili kwenye mpira wa kisasa inakera sana,mpira wa kisasa ni biashara,,eti wanaitapeli,simba ilikuwa na Nini kabla ya mo?
 
Magori huyo ni mbeba mikoba ya MO, alifukuzwa NSSF kwa ufisadi, anashirikiana na MO kuitapeli simba, zile pesa za CAF hazijulikani zimeenda wapi, aondoke mapema kabla hajaishia jela!

Nyie ndio mashabiki maandazi, mbona ujauliza pesa za usajili zimetoka wapi? Pesa za kambi five star hotel zinatoka wapi? Pesa ya pre season zinatoka wapi? Pesa za salary za wachezaji zinatoka wapi?
 
Natambua kuwa Yeye kama Yeye alishasema kuwa anang'atuka hapo kama CEO baada ya Miezi Sita ili apatikane CEO mwingine na kama Simba SC itahitaji Mchango wake basi imtumie katika mambo makubwa na mazito hasa ya Kimaamuzi ambayo Yeye kwa Hadhi yake na Uzoefu wake mkubwa anadhani ataitendea Simba SC makubwa.

Kwa muda mfupi tu ambao nimeitathmini Simba SC ikiwa chini ya Utendaji wa CEO Magori nimegundua kuna mambo mengi sana ya Kimaendeleo yametokea na Mafanikio makubwa yamepatikana hasa akishirikiana vyema kabisa na Mwekezaji Mo Dewji na Mwenyekiti Nkwabi hivyo nashawishika leo hii kusema kama si kuomba kwamba huyo CEO Magori aendelee kuwepo hapo na aongezewe Package yake Kimaslahi lakini pia ajumuishwe katika sehemu muhimu za Kimaamuzi na Kiuwekezaji ndani ya Klabu.

Simba SC tukikubali CEO Magori aondoke hapo tutakuwa tumetupa Jiwe la Thamani kubwa sana ambalo mpaka kuja kulipata tena itatuchukua muda mrefu. CEO Magori ameweza kuwa Kiungo bora kabisa kati ya Wachezaji, Benchi zima la Ufundi na Uongozi mzima wa Klabu na kitu kizuri Kwake ni kwamba ametokea Kupendwa na Kukubalika mno na Wachezaji wa Simba SC ambao amekuwa akiishi nao si tu kama Rafiki bali kama Baba kitu ambacho kimeweza kusababisha Mshikamano mkubwa ambao ulipelekea Ufanisi hadi Timu ikapata Mafanikio yale iliyoyapata.

Sina uwezo wa Kubadilisha Mawazo au Maamuzi ya CEO Magori na wala sina uwezo wa Kuupangia Uongozi mzima wa Simba SC chini ya Mwekezaji Mkuu Mo Dewji na Mwenyekiti Nkwabi pamoja na Bodi yao nzima ila nawaomba sana wafanye kila waliwezalo ili hata kama itabidi Kuundwe Cheo Kipya cha Juu ndani ya Simba SC ili CEO Magori akiongoze basi hilo lifanyike haraka au kama kuna uwezekano wa Kumpa Majukumu mengine makubwa ya Kiutendaji ili mradi tu huu Mchango wake mkubwa alioutoa Klabuni uendelee na Simba SC izidi Kufaidika nae basi hilo lifanyike upesi

Kwa Simba SC ya sasa na huku ikiwa imeanza Kujijenga Kiuwekezaji inamuhitaji sana CEO Magori hivyo tusimpoteze. Kwa wale walio karibu au jirani na Uongozi wa Juu wa Simba SC nitawashukuruni kama huu Uzi wangu mtaufowadi Kwao moja kwa moja au hata kwa Msemaji na kama Wahusika wote wako hapa JamiiForums kitu ambacho naamini wapo hivyo watautathmini na wataufanyia Kazi ila nitafurahi mno hata kama CEO Magori atamkabidhi Mtu mwingine hicho Cheo chake basi na Yeye pia aendelee kuwepo katika sehemu ya Mafanikio yajayo ya Klabu hasa Kiutendaji na katika Kipindi hiki cha Uwekezaji ambacho Simba SC imeingia rasmi.
Ni lini hela ya mwekezaji itaingizwa kwenye akaunti ya Simba kama ilivyokubaliwa kwenye Mkutano mkuu ?
 
Matokeo ya mchezo wa ki rafiki ( pre season)
Screenshot_2019-07-23-13-46-25.jpg
 
Magori huyo ni mbeba mikoba ya MO, alifukuzwa NSSF kwa ufisadi, anashirikiana na MO kuitapeli simba, zile pesa za CAF hazijulikani zimeenda wapi, aondoke mapema kabla hajaishia jela!

Simba inatapeliwa na Mo?

Ndio Yale yale ya Akili mali kusema Manji anaiibia Yanga na baada ya ‘Mwizi’ kujitoa, aliekuwa anaibiwa Kachoka zaid
 
Magori alikuwa mbuzi wa kafara tu, hausiki na ufisadi wowote kule, tafuteni sababu nyingine tu.

Back
Top Bottom