TheCrocodile
JF-Expert Member
- May 31, 2021
- 1,864
- 5,254
Mgogoro mkubwa umeibuka katika jengo la biashara la Manyara Safari Lodge – Heritage Camp Lodge lililopo wilayani Karatu, mkoani Arusha, baada ya mwekezaji wa kigeni na mmiliki mwenza wa eneo hilo, Timothy Flavell, kudai kuwa anajaribiwa kutapeliwa na mpangaji wake, Erick Mashauri.
Flavell, raia wa Uingereza anayeishi Tanzania, amesema mgogoro huo umetokana na mpangaji huyo kushindwa kutekeleza masharti ya mkataba wa upangaji waliokubaliana mwaka 2022. Kwa mujibu wa Flavell, mpangaji huyo anadaiwa zaidi ya dola za Marekani milioni 26 kama kodi ya pango, hali iliyosababisha kuvunjwa rasmi kwa mkataba huo kuanzia Aprili 1, 2026.
Akizungumza kupitia kampuni yao ya Tarylin Ltd, inayomiliki pia Manyara Safari Lodge, Flavell amesema walitoa notisi kadhaa za maandishi pamoja na tangazo kwenye gazeti la serikali wakimtaka mpangaji huyo kuondoka, lakini ameendelea kukaidi na kudai kuwa yeye ni mwekezaji halali wa eneo hilo.
“Tumezingatia taratibu zote za kisheria, lakini bado anakataa kuondoka na hata anatishia usalama wetu. Tunaiomba serikali iingilie kati ili haki itendeke,” amesema Flavell.
Katika hatua nyingine, Flavell amekanusha madai ya mpangaji huyo kuwa amewekeza kwa kujenga miundombinu ya lodge hiyo, akieleza kuwa ujenzi uliodaiwa wa vyumba viwili wenye thamani ya dola 70,000 hauendani na uhalisia wa gharama halisi.
Kwa mujibu wa mkataba wa awali, mpangaji alipaswa kulipa dola 25,000 kwa mwaka pamoja na asilimia 10 ya mapato kwa kila mgeni. Hata hivyo, Flavell anadai kuwa mwaka jana mpangaji alianza kuchelewesha malipo na baadaye kulipa asilimia 5 pekee bila makubaliano.
Flavell amesema baada ya kuvunjwa kwa mkataba, walifanikiwa kumwondoa mpangaji huyo kwa msaada wa walinzi binafsi, lakini baadaye alirejeshwa kufuatia maelekezo ya Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Lameck Karanga, ili kumalizia huduma kwa wageni waliokuwa tayari wameweka nafasi.
Akizungumzia suala hilo, Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Lameck Karanga, amekiri kuufahamu mgogoro huo na kusema hatua aliyochukua ilikuwa ni ya mpito kwa lengo la kulinda amani na maslahi ya wageni.
Alieleza kuwa alimruhusu mpangaji kurejea kwa muda wa wiki mbili ili kukamilisha huduma kwa wageni waliokuwa tayari