Mwekezaji wa Kitanzania Edha Nahdi ainunua Oryx Energies

Mwekezaji wa Kitanzania Edha Nahdi ainunua Oryx Energies

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Amsons Group, kampuni kubwa ya Kitanzania yenye uwekezaji katika sekta mbalimbali, imeingia makubaliano ya kuinunua kampuni ya Oryx Energies nchini Tanzania, hatua inayoiweka kampuni hiyo katika nafasi ya kupanua ushawishi wake katika sekta ya nishati.

Soma Pia: Kampuni ya Amsons Group ya Tanzania inahusishwa kuinunua Oryx kwa Dola Milioni 250

Makubaliano ya kampuni hizo mbili yanahusisha miundombinu muhimu ya biashara ya mafuta ya Oryx Energies, ikiwemo bohari za kuhifadhia mafuta, vituo vya kujaza mafuta na mtandao wa usambazaji wa bidhaa za mafuta nchini Tanzania.

Hatua hiyo inaashiria mabadiliko muhimu katika umiliki wa miundombinu ya nishati nchini, huku kampuni ya Kitanzania ikipata fursa ya kuendeleza biashara iliyojengwa na Oryx Energies na kutafuta fursa zaidi za ukuaji katika soko la ndani na ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Mkurugenzi Mtendaji wa Amsons Group, Bw. Edha Nahdi amesema makubaliano hayo yanaendana na azma ya kampuni hiyo ya kupanua shughuli zake katika sekta ya nishati na usafirishaji.

Amesema kuunganishwa kwa mtandao wa usambazaji na uwezo wa kuhifadhi mafuta wa Oryx Energies kutasaidia kuimarisha nafasi ya Tanzania katika biashara ya nishati na kuifanya Tanzania kuwa kituo muhimu cha vifaa na usafirishaji katika ukanda huo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Energies, Bw. Moussa Diao, amesema wamechagua kuingia makubaliano hayo kutokana na imani waliyonayo kwa uwezo wa Amsons Group kuendeleza biashara hiyo na kuibua fursa mpya kwa wafanyakazi, wateja na washirika.


images (59).jpg
Oryx Energies imeeleza kuwa uamuzi wa kuuza biashara hiyo ni sehemu ya tathmini yake ya kimkakati kuhusu uwekezaji wake katika usambazaji wa mafuta barani Afrika, huku ikilenga kuelekeza rasilimali zake katika kuendeleza miundombinu ya nishati na kuimarisha shughuli zake katika masoko mengine.
 
Tunapita mule mule mpaka tutafika. Hii ni baada ya kesi fulani hapo zamani za kale kumalizika
 
Hivi hawa Amsons Group sio ni kampuni Mama ndani ya zile kampuni za RA?
 
Back
Top Bottom