Hapo umenifanya maswali yangu yote niyafute cose I thought you're against Christianity and the faith of our Lord Jesus brought to us. Kweli Mungu hakuleta dini Bali alileta Imani tu. tuko pamoja na ngoja tumsubili kahtaan maaana kuna swali nae nimemuuliza.
Mkuu nimeshakueleza hapo juu kuwa Yesu alikuwa Binaadamu km wewe na mimi.
Na andiko limesema Hivyo.
Aliyekwambia wewe kuwa yesu ni Mungu si mwingine Bali ni False Apostle PAUL.
Huyu Nabii wa Uongo ambae HAJAWAHI KUMUONA YESU wala WANAFUNZI WAKE YESU Ndio aliyeandika Kila mahala kuwa Yesu ni Mungu na Ni mwana Wa Mungu.
Lkn YESU kwa Kauli zake Mwenyewe anasema Yeye ni MTUMWA WA MUNGU (MTUME).
Soma ref zifuatazo za MANENO YA YESU MWENYEWE halafu uone je kuna Sehemu yyt amejiita Mungu?
Watu mnabadili Tafsiri na Kupotosha Nafsi zenu.
YOHANA 5:24-----
"Kweli nawaambieni, anayesikia neno langu, na kumwamini yule-aliyenituma, anao uzima wa milele. Hatahukumiwa kamwe, bali amekwisha pita kutoka kifo na kuingia katika uzima.
YOHANA 5:30
- - -"Mimi siwezi kufanya kitu kwa uwezo wangu mwenyewe. Mimi nina hukumukama-ninavyosikia kutoka kwa Baba, nayo hukumu yangu ni ya haki. Nia yangu si kufanya nipendavyo mwenyewe, bali apendavyo yule-aliyenituma.
-YOHANA 5:36
- - -Lakini mimi nina ushahidi juu yangu ambao ni mkuu zaidi kuliko ule wa Yohane. Kwa maana kazi ninazofanya, kazi alizonipa Baba nizifanye, ndizo zinazonishuhudia kwamba Baba ndiyealiyenituma.-
-YOHANA 5:37
- - -Naye Baba-aliyenituma-hunishuhudia. Ninyi hamjapata kamwe kusikia sauti yake, wala kuuona uso wake.
-------
YOHANA 7:16
- - -Hapo Yesu akawajibu, "Mafundisho ninayofundisha si yangu, bali ni yake yeyealiyenituma.
YOHANA 7:28
- - -Basi, Yesu alipokuwa anafundisha Hekaluni alipaaza sauti na kusema, "Ati mnanijua; hata nilikotoka mnakujua! Hata hivyo, sikuja kwa mamlaka yangu mwenyewe; ila yeye-aliyenituma-mimi ni wa kweli, nanyi hamumjui.
YOHANA 7:29
- - -Lakini mimi namjua kwa sababu nimetoka kwake, naye ndiye-aliyenituma."
YOHANA 7:33
- - -Yesu akasema, "Bado niko nanyi kwa muda mfupi, kisha nitamwendea yulealiyenituma.
-------
YOHANA 8:16
- - -Hata nikihukumu, hukumu yangu ni ya haki kwa sababu mimi siko peke yangu; Baba-aliyenituma-yuko pamoja nami.
YOHANA 8:18
- - -Mimi najishuhudia mwenyewe, naye Baba-aliyenituma, ananishuhudia pia."
YOHANA 8:26
- - -Ninayo mengi ya kusema na kuhukumu juu yenu. Lakini yule-aliyenituma-ni kweli; nami nauambia ulimwengu mambo yale tu niliyoyasikia kutoka kwake."
YOHANA 8:29
- - -Yule-aliyenituma-yuko pamoja nami; yeye hakuniacha peke yangu kwani nafanya daima yale yanayompendeza."
-------
YOHANA 6:38
- - -kwani nimeshuka kutoka mbinguni si kwa ajili ya kufanya matakwa yangu, ila kutimiza matakwa ya yule-aliyenituma.
YOHANA 6:39
- - -Na matakwa ya yule-aliyenituma-ndiyo haya: nisimpoteze hata mmoja kati ya wale alionipa, ila niwafufue wote Siku ya mwisho.
-------
YOHANA 12:44
- --Kisha Yesu akasema kwa sauti kubwa, "Mtu aliyeniamini, haniamini mimi tu, ila anamwamini pia yule-aliyenituma.
YOHANA 12:49
- --Mimi sikunena kwa mamlaka yangu mwenyewe, ila Baba-aliyenituma-ndiye aliyeniamuru niseme nini na niongee nini.
-------
MATAYO 10:40
- -"Anayewakaribisha ninyi, ananikaribisha mimi; na anayenikaribisha mimi, anamkaribisha yule-aliyenituma.
-------
MARKO 9:37
- - - -"Anayempokea mtoto-kama-huyu kwa jina langu, ananipokea mimi; na anayenipokea mimi, hanipokei mimi tu, bali anampokea yule-aliyenituma."
-------
LUKA 9:48
--akawaambia, "Mtu yeyote anayempokea mtoto huyu mdogo kwa jina langu, ananipokea mimi; na yeyote anayenipokea mimi, anampokea yulealiyenituma. Maana yule aliye mdogo kuliko wote kati yenu ndiye aliye mkubwa kuliko wote."
-------
LUKA 10:16
- - - --Halafu akasema, "Anayewasikiliza ninyi, ananisikiliza mimi; na anayekataa kuwapokea ninyi, anakataa kunipokea mimi. Yeyote anayekataa kunipokea, anakataa kumpokea yule-aliyenituma."
-------
YOHANA 4:34
- - -Yesu akawaambia, "Chakula changu ni kufanya anachotaka yule-aliyenituma-na kuitimiza kazi yake.
-------
YOHANA 9:4
- - - -Kukiwa bado mchana yatupasa kuendelea kufanya kazi za yulealiyenituma; maana usiku unakuja ambapo mtu hawezi kufanya kazi.
-------
YOHANA 13:20
- --Kweli nawaambieni anayempokea yule ninayemtuma anaponipokea mimi; na anayenipokea mimi, anampokea yulealiyenituma."
-------
YOHANA 14:24
- --Asiyenipenda hashiki maneno yangu. Na neno mlilosikia si langu, bali ni-lakeBaba-aliyenituma.
-------
YOHANA 15:21
- --Lakini hayo yote watawatendeeni ninyi kwa sababu ya jina langu, kwani hawamjui yeye-aliyenituma.
-------
YOHANA 16:5
- - -Lakini sasa namwendea yulealiyenituma; na hakuna hata mmoja wenu anayeniuliza: `Unakwenda wapi?`