Mwenda Tezi na Omo marejeo Ngamani-TEC Wameelewa,Bado nani Hajaelewa?

Ndugu yangu,Kwanza hao viongozi ni wetu mimi na wewe.Swala la maridhiano sio swala utayari tu.Ni swala la kimkakati.kauli,matamko na matendo yao yana akisi kiwango cha mgogoro uliopo ambao ndio ambao unahitaji sasa maridhiano.

Labda nikuulize wewe unafikiri Maridhiano ya kweli ni yepi?
 
Ndugu yangu,Utashangaa sana ukigundua kwamba hayo maarifa,taarifa na uzoefu wa wanachohubiri na kukioambani sio ambacho mimi na wewe na watanzania wengi tunachotamani na tunachopigania.

..hakuna haja ya Cdm au Tec kubadili uongozi ili kutuliza mgogoro wa kisiasa uliopo nchini.

..jambo ambalo linaweza kutusaidia ni serikali kuomba msaada wa MSULUHISHI WA KIMATAIFA.

..nitakukumbusha ujio wa Rais Mstaafu Lazarus Chakwera, na jinsi alivyoweza kupata ushirikiano wa wadau wote wa siasa za Tanzania.

..Serikali ikubali kumrejesha Mzee Chakwera na kumpa jukumu la kutusuluhisha. Waswahili tuna msemo wetu, " mganga hajigangi. "
 
Watoke hao wa ccm kwanza ili tuone huo utayari, na sio watoke wa cdm tu.
 
Una hoja ya msingi,na ndiko tunaelekea ila kwanza lazima tuhakikishe political fall out inakuwa minimal
 
Ni yale maridhiano yasiyo na unafiki/ubinafsi ndani yake. Bahati mbaya ukija kwa viongozi wa serikali ya ccm, mara zote huvutia maridhiano yenye manufaa/maslahi kwao tu! Badala ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
 
Ni yale maridhiano yasiyo na unafiki/ubinafsi ndani yake. Bahati mbaya ukija kwa viongozi wa serikali ya ccm, mara zote huvutia maridhiano yenye manufaa/maslahi kwao tu! Badala ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Kama ndicho tunachokitaka tutachelewasana.Je unafahamu kwamba kuna issue ya National Stability and Political Fallout?Unafahamu kwamba huu mgogoro wote ni mgogoro wa maslahi kati ya watawala na wanaotawaliwa?Maslahi ya kisiasa daima ni personal na mara nyingi kila mwamba ngoma huvutia kwake?Nafikri hoja yangu bado ina mashiko.
 
Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
 
Una hoja ya msingi,na ndiko tunaelekea ila kwanza lazima tuhakikishe political fall out inakuwa minimal

..Chadema wameongea na Chakwera bila kujali kwamba Mwenyekiti wao yuko kizuizini. We should take advantage of that na kuanzisha mchakato wa maridhiano.

..Pia kila upande unapaswa kusitisha hostilities dhidi ya mwingine.

..Hii kamata kamata inatakiwa kusitishwa. Kuna hatari ya kusababisha mauaji mengine juu ya yale ya OCT 29.

..Kuunda Tume ambazo zinakataliwa na kubezwa tangu kuundwa kwake kusitishwe. Kulazimisha kuunda Tume ambazo hazizibi nyufa na mpasuko uliopo hakuna faida.

..Pia inaelekea serikali imegoma kuomba radhi, pamoja na kwamba imeuwa watu.

..Kama serikali haina mpango wa kuwaadhibu watendaji wake waliohusika na mauaji, basi haina uhalali wa kuwaadhibu waliofanya vurugu, na kuharibu mali.

..Serikali iwafidie wote waliopoteza ndugu zao, na walioharibiwa mali zao. Hatua hiyo inapaswa kufanyika bila kuchelewa.

..Serikali pia ihakikishe hatima ya watu wote waliopotea ktk mazingira ya kisiasa inajulikana. Masuala ya kina Mdude, Soka, Mlay, Polepole, na wengine, ni lazima yawekwe wazi
 
Basi kwa hali hii yaliyotokea Oktoba 29, 2025 ipo siku yatajirudia tena.
 

..You cant eat your cake and have it.

..lazima baadhi ya vigogo ktk Ccm na vyombo vya dola wabebe msalaba.

..wako waliomshauri Rais vibaya aachane na 4R huku wakimuaminisha kwamba Polisi, na Usalama, watamvusha salama ktk uchaguzi.

..matokeo ya ushauri huo yamepelekea umwagaji damu mkubwa wa kihistoria OCT 29. Lakini hata kama uchaguzi ungepita salama bado huko nyuma kuna watu wamenyimwa uhai kwasababu ya misimamo yao ya kisiasa.

..Mama hawezi kusema " never again " huko bado yuko na watu waliomtumbukiza ktk dhambi na aibu kubwa. Ili kuitendea haki kauli mbiu hiyo ni lazima awatose waliosababisha maafa na aibu kwa taifa letu.
 
Hamna jipya nyie yani uuwe raia wako afu uje ujadiliane nao,kulikuwa na ugumu gani majadiliano yangefanyika kabla ya uchaguzi.Ubinafsi na Ufisadi ndiyo unaowaangamiza nyie vilaza.
 
Si lazima kila mtu akibaliane na maoni yako. Mtu mwingine anaweza kuwa na maoni tofauti na akawa valid kuliko wewe.Pengine hata kwa namna usiyoielewa.

Siku nyingine jikite kwenye kuchambua facts zaidi ya maoni yako.
 
Mimi binafsi sina Rais anayeitwa Samiya (huyo malaya kajipachika hapo bila ridhaa yetu)
 
Unamaanisha Sacrificial Lamb?Hao watakuwepo na hata sasa hivi wanatafutwa kwa udi na uvumba shida zigo la Oct 29 ni zito sana hakuna aliyeko tayari kuyabeba akiwa hai
 
Si lazima kila mtu akibaliane na maoni yako. Mtu mwingine anaweza kuwa na maoni tofauti na akawa valid kuliko wewe.Pengine hata kwa namna usiyoielewa.

Siku nyingine jikite kwenye kuchambua facts zaidi ya maoni yako.
Si ndio uhuru wa maoni wenye mnaodai ninyi?Au uhuru wa maoni una mpaka inapokuwa no hoja tofauti ili tukikubalina na ujinga wenu ghafla tunakuwa mashujaa.Sikudhani kwamba na wewe unanyumbuka kihasi hicho.Anyway jikita kwenye kuchambua fact nilizoweka badala ya kuweka maoni yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…