Mwendazake alitumia muda mwingi kuwatukana wengine, sasa ni malipo yake

Mwendazake alitumia muda mwingi kuwatukana wengine, sasa ni malipo yake

Moja kati ya engagements zake za mwisho na wananchi, alimwambia mtu abaki na mav* yake nyumbani.
Aisee,ila jamaa sijui alikuwa anaipeleka wapi hii nchi daa!!!sad enough kumbe muda wote alikuwa anaumwa kwa nini alikuwa anajiongezea stress badala ya kuishi kwa amani na uchaji Mungu.
 
Heshima yenu wakuu

Kinachotokea kwa sasa mitandaoni, bungeni na mitaani ni matokeo yaliyopandwa na mwendazake.

Bungeni kuna mmyukano mkali, mitandaoni ndio hakufai.

Wapo wanaomponda mwendazake na wapo wanaomsifia.

Jambo moja la kuweka kichwani ni kuwa mwendazake alipokuwa hai wasifiaji na waimba mapambio ndio walikuwa wengi zaidi hivyo ilizoeleka hivyo.

Wakosoaji walikuwa wachache sana kutokana na vitisho na matukio yaliyokuwanyanaendelea.

Sasa mwendazake hayupo jambo ambalo linaibua kila kukicha idadi ya wapondani na wakosoaji wa mwendazake huku idadi ya waimba mapambio ikishuka kwa Kasi kubwa.

Waimba mapambio watakaobaki wanafahamika kwani ni wale waliopewa nafasi kwa upendeleo kama vile baadhi ya wabunge ambao wanajua Kabisa bila ya mwendazake wasingekuwa bungeni.

Mwendazake alishawakashfu baadhi ya watangulizi wake kwa maneno ya dhihaka na kejeli.

Mwendazake ndiye aliyeanzisha Tabia ya kudhalilisha viongozi wa Umma na kuwatusi.

Wapo walioitwa WAPUMBAVU mbele za halaiki.

Wapo walioitwa VILAZA mbele za Umma.

Wapo walioitwa MAJIZI na Majambazi mbele za watu

Wapo walioitwa VIBARAKA mbele ya Kamera

Wapo walioambiwa WANANJAA akiwepo Kaka Pascal Mayalla humu

Wapo aliosema kuwa hawapaswi kuishi mbele za watu na kweli walijeruhiwa na wengine kupotea

Sasa ni zamu yake na ashukuru hayupo maana kama angekuwa hai huo mwaka 2026 + ndio ungekuwa mbaya kwake zaidi

Kweli Karma is real
Malipo ni hapa hapa duniani

Watered I wake jambo moja wasilolielea ni kuwa Kadiri wanavyomtetea hakika madhara Hayat’s waache salama, wanajiwekea alama kwenye nyuso zao ili iwe rahisi kupewa stahiki zao, na watapewa tuu mpaka mwaka 2023 kila mtu atakuwa amepokea kamisheni yake

Ni bora Hawa raia wa kawaida na wanaharakati mitandaoni ndio wawe mstari wa mbele kujibu mashambulizi lakini kama unacheo iwe mbunge au mkuu wa mmoja au Wilaya au cheo chochote ni Bora ujikalie kimya tuu

Vinginevyo uzi huu utaukumbuka 2023 ukiwa na familia yako baada ya kupokea kamisheni ya malipo ya mwendazake

Endeleeni Kudemka
Kuna Yule Mwananchi Alimwambia Aende na Mavi yake
 
Nakumbuka alimdhalikisha jk nadhani pale UDSM au UDOM hadi mzee JK alihamaki kwa mshangao, alimwambia mzee umeniachia mzigo kweli kweli kila kitu hewaaa
🤣🤣🤣🤣
 
Nimesema Mimi ndio rais sasa tunaomba ajitete sasa ye kama raisi
 
Back
Top Bottom