kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Usafiri wa mwendo wa haraka ni jambo jema kwa uchumi kwakuwa unapunguza muda wa kukaa njiani na kuongeza muda wa kufanya kazi kwa siku, wiki, mwezi na mwaka.
Pamoja na kazi na kasi hii ya kujenga usafiri wa haraka lakini lazima ujenzi huu uzingatie pia kujenga vituo vikubwa vya kuegesha magari ya watu binafsi kutoka pembezoni mwa mji yasifike katikati ya mji sambamba na mabasi yenu ya BRT.
Hivi ni vituo ambavyo magari madogo ya watu binafsi kutoka maeneo yasiyofikiwa na mradi yataegeshwa hapo kwa malipo kidogo wakati mwenye gari hilo anabadilisha usafiri kutoka gari lake binafsi kwenda kwenye BRT kuendelea na safari yake kuelekea city center.
Hii itapunguza msongamano, moshi wa magari, kelele za magari na magereji katikati ya mji. Pili magari ya mwendo wa haraka yawe na ratiba inayofahamika kwa muda na siku.
Tatu, magari ya mradi wa BRT yote yatumie gesi ili kutunza mazingira kwa kupunguza Moshi katikati ya mji na kupunguza gharama za uendeshaji wa mradi kwa kuwa gesi ni rahisi lakini haibiwi na madereva wa magari kama ilivyo kwa mafuta ya magari.
Ndugu zangu kujenga nchi sio lazima uteuliwe na Rais na kupewa maagizo. Tujiongeze.