Mwendokasi hali ni mbaya

Mwendokasi hali ni mbaya

Na aliyeruhusu bajaj kuja mjini ndiyo kaharibu kabisa. Angalia zinavyopaki ovyo na kusababisha msongamano barabarani. Hizi zilitakiwa ziishie bara bara za mitaani tu siyo trunk roads. Ukizingatia ukosefu wa ustarabu kwa madereva wa hivyo vibajaj huwezi kuelewa kwa nini vinaruhusiwa kuingia mjini kati
Mimi watu walioruhusu hiz bajaji na Bodaboda ndo walikosea kabisa.
Siku hiz Dar haina tofauti na dhaka na india huko.
Yaani kuua mradi wa mabasi, basi linaloweza kubeba watu 100+ na kuruhusu bajaji/bodaboda inayobeba watu maximum wanne. Halafu utegemee umalize foleni Dar?
 
We ni mbuzi kweli aliekwanbia wanaopanda mwendokasi hawana hela ni nani

Mwendokasi ndio usafiri umewafanya watu kuacha magari kukimbia foleni na uchovu usijidanganye
kwa taarifa yako daldala kwa sasa ni more comforatble kuliko hayo ma mwendo kasi yenu mnajaza kama samaki kwenye tenga, and this has been done strategically
 
Kama kuna abiria aliyetoka na treni ya saa kumi namoja jioni kwenda Moro kashafika na kaoga kapumzika huwezi amini hapa kivukoni watu wapo tokea saa 10 hamna magari

Yaani abiria wa Moro kafika na kashalala mtu wa kimara haelewi hadi sasa ataondoka saa ngapi

Sijui Serikali mna mpango gani na huu usafiri mnajinadi kila siku mmefanya makubwa mbona hali tete sana huku
Ngoja kwanza tuwahudumie chawa, hawa jambo lao muhimu sana ni mwishoni mwa mwaka huu.
 
Back
Top Bottom