DOKEZO MWENDOKASI: Madereva na watumishi wanavyopakiza ndugu zao nje ya utaratibu

DOKEZO MWENDOKASI: Madereva na watumishi wanavyopakiza ndugu zao nje ya utaratibu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Bongo kwa lawama.

Kama ulikua hujui ndgu hii nchi ni nchi ya janjajanja.
Ukizubaa wenzao wanatumia uzubavu wako kama daraja.

Hapo ungeanzisha vurumai hapohapo stendi hao jamaa wangeshuka wakapanga foleni, ila kwakua nyie ni wazubavu, unaacha kupambana hapo kwanza unaleta huku jf acha waendelee kupendeleana.
 
usafiri huo ulishakuwa maji taka siku nyingiiii yani kimsingi nunua gari tu maana ukikimbilia kwenye daladala ndiobalaa kabisaaaaa Bongo hamna kitu kinakwenda smoothly
Kumiliki gari sidhani kama ndio kutafanya usiwahi kutumia tena usafiri mwingine kuna dharura za hapa na pale, watu wengi wanamiliki magari lakini siku moja moja kwa sababu mbalimbali huwa wanapanda usafiri wa umma, kuna mahali daladala huwa hazijazi sana na siyo za kugombania
 
acha kupanic kwa mambo madogo madogo kama hivi haya mambo yapo katika taasisi zote hospital, TRA, Bandarini, Mashuleni. I bet hata wewe ungekuwa na nafasi sehemu huwezi acha damu tako iteseke.

siungi mkono lakini
Tatizo la watanzania! Huoni tatizo siyo? Pole!
 
Kwa wenzetu, unakuta basi tena la gorofa, ndani kuna watu wanne au watano, na nje mko wanne; bado watu hujali foleni, aliyetangulia kufika ndiye atakayetangulia kuingia!

Shame on us, ndo maana hatutakaa tuendelee! Afu watu na akili zao timamu, eti anatetea huu ujinga! Shame!
 
Zungumzia na suala la ticket fake.

Leo pale Mbezi nimekata tikiti 07:06 nikapewa inayosoma time 07:49 tarahe ya leo nilikuwa na jamaa yangu tukaangalia ya kwake inasema muda iliotolewa ni 06:51 ambayo kwa uzoefu wangu inaweza kuwa kweli.

Mimi nimejiuliza hii imewezekanaje?yumkini kuna muda hawa jamaa huchanganya na kanjanja zao muda fulani ukifika.
 
Huoujinga umeshika hatamu sana safari hii
Hasa kivukoni pale

Gari lishaenea siti z mbele za dirishani
Watu wanapandishana kindugu.
 
Serikali ilivyo na akili zake zisizojulikana, muda mfupi ujao utaona vibao vya kukataza kupiga picha vituo vya mwendokasi vimebandikwa.

Mashine za kukagua ticket hazijaharibika lakini zimesimamishwa mwaka wa 6 huu.

Nchi imejaa walaanifu hii kha
Hawaruhusu kupiga picha hata hivyo.
 
Mmh Africa hatari San, mtu anatetea usawa na haki lakin anaonekana snitch...ivi Africa matendo haya mnaona ya kawaida kweli, mtu kunyimwa haki yko
Lakini ijulikane wazi utaratibu upo wazi na nchi nyingine mtu anawajibishwa kufanya kinyume na utaratibu. Siku hizi smartphone lakini watu wanashindwa kurekodi ikiwa hivyo hakuna mfanyakazi wa huduma ya serikali atafanya kinyume na wakati anajua wananchi wanamrekodi hapo kukiwa na ushahidi mtu hawezi kutoa favours au ujinga wakati yeye ndie atakaye jibu malalamiko. Sio kwamba nchi nyingine ni malaika eti wanafanya kila kitu vizuri lakini wananchi wanajua ukishakuwa na ushahidi sana sana was video huyo mfanyakazi au kampuni inawajibishwa kisheria ambazo hata Tanzania na nchi za Africa zipo. How many times serikali inaingilia kati kitu kwasababu kuna ushahidi wa wazi(video evidence) sio tu tetesi lakini watu bado wanashindwa kujua kuwa sasa simu ni kitu muhimu kupata haki.
 
acha kupanic kwa mambo madogo madogo kama hivi haya mambo yapo katika taasisi zote hospital, TRA, Bandarini, Mashuleni. I bet hata wewe ungekuwa na nafasi sehemu huwezi acha damu tako iteseke.

siungi mkono lakini
Hii si kweli. Sanasana ungemshauri asingekuja kulalamika hapa. Kwa umoja wao wangemaliza hiyo kesi hapohapo. Wanawapiga ngumi hao wahudumu na hao ndugu zao.

Shida yetu watz ni maboya. Unakuta wengi wao wanaumia chinichini. Hawawezi kuondoa uovu kwa mkono wao.

Hii hoja ya kuita hilo ni jambo dogo halina nafasi kwenye utawala wa sheria. Hata mimi nikifanya hivyo kitengoni kwangu nipigwe hadi nitoke meno.
 
Hii si kweli. Sanasana ungemshauri asingekuja kulalamika hapa. Kwa umoja wao wangemaliza hiyo kesi hapohapo. Wanawapiga ngumi hao wahudumu na hao ndugu zao.

Shida yetu watz ni maboya. Unakuta wengi wao wanaumia chinichini. Hawawezi kuondoa uovu kwa mkono wao.

Hii hoja ya kuita hilo ni jambo dogo halina nafasi kwenye utawala wa sheria. Hata mimi nikifanya hivyo kitengoni kwangu nipigwe hadi nitoke meno.
unazungumzia utawala na sheria ktk nchi gani? kama mambo makubwa hayafati utawala bora na sheria yatakuwa haya ya UDA??

tunachekesha
 
Uwepo wa uholela hakufanyi tusizungumze. Na wananchi tukiwa na ujasiri wa kukemea ndiyo tutaweza walau kuwastua hao watekelezaji. Kusema hakuna utawala wa sheria na kuruhusu hata kile kidogo mnachoweza kukiondoa ni upumbavu. Kero nyingi mitaani tunaweza kuziondoa wenyewe. Kuna vijiji mpaka leo bado wanachapa viboko wakosefu. Watu wananyooka. Na sisi hatushindwi kujisimamia kwenye foleni za daladala. Abiria wakiamua kesho tu kero hiyo kwisha. Hakuna yeyoye atakaeleta shida.
 
Maboresho yanayotakiwa kufanyika katika mradi wa mabasi yaendayo haraka Bus rapid transit (BRT) jijini Dar es Salaam.


Nimebaini changamoto kadhaa zinazotakiwa kutatuliwa katika mradi huu.


Hivyo nimemshauri juu ya maboresho yanayotakiwa kufanywa katika mradi huu. Pitia katika link hii kusoma ushauri wote: Kwako Mkurugenzi mpya wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART): Katatue changamoto zifuatazo….


Pia michango mbalimbali imetolewa na wadau wengine na wameshauri jinsi ambavyo mfumo wa uendeshaji wa haya mabasi unapaswa kuwa ili kwendana na ukuaji wa teknolojia:


Ushauri wote tumeuandika hapa: Kwako Mkurugenzi mpya wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART): Katatue changamoto zifuatazo….
 
Back
Top Bottom