Mwendokasi UDART mmefeli

Ukiwa unatoka morocco , kivukoni au gerezani usku , ukashukia Kimara , kama una safari ya kwenda mbezi Bora ufanye mazoezi ya kuzunguka Tu daraja ukapande bajaji zinazoenda mbezi , ukisubir mwendo kasi ya mbezi utajutaaa ..yaan mabasi yapo tuu yamesimama na abiria mmesimama zaidi ya nusu saa Magari yanazunguka zunguka tuu , madereva nao sifa kibao....

Kama huna kigari au TVS basi panda bajaji ndo usafr murua kabisa Kwa DSM
 
Hayo magari watu wanajazana mlangoni ndani kweupe sana ingekuwa wanagunguwa mlango mmoja watu wanaingia kwa mstari miwili uku na uku then kati kati, ila utaratibu mbovu na watu hawaendi bila kusimamiwa
unachoongea ni ukweli mkuu,watu wengi wanapenda kujazana pale mlangoni alafu huku mbele na katikati kunakuwa na nafasi kubwa tu ila watu hawaendi,mtoa mada akiambiwa mambo madogo kama hayo na mlinzi wa darasa la nne anaona kaonewa na Phd yake.
 
Mwendokasi nahisi ni mradi wa mtu ambaye hawezi kuguswa. Ukitafuta nyuzi za kero za mwendokasi na ushauri wa kuboresha mwendokasi hazipungui hamsini humu JF lakini hakuna hatua zozote zimewahi kuchukuliwa walau hata kupunguza kero. Hivi inshindikana nini :-
  • Kuwa angalau na ofisa mmoja kila kituo ambao watakuwa na mawasiliano ya redio call wakawa na mawasiliano na incharge mabasi yanapoanzia yaani gerezani, kivukoni, kimara, moroco na mbezi. Wawe wanasiliana muda wote kujua kila wakati wapi kuna abairia wengi ili mabasi mengi yaelekezwe huko kwa muda husika.
  • Kila kituo kuwe angalau na wasimamizi wa kutosha kuhakikisha abiria wanapanada kwa foleni badala ya kusukumana, kukanyagana na kuibiana.
-Wasimamizi hao hao wahakikishe kuwa mabasi yanapakia abiria kwa kiwango fulani kiasi abiria waweze kupumua vizuri na mama/dada/binti zetu wasiwe wanadhalilishwa na dunga dunga ndani ya mabasi.
- Wasimamizi hao hao waweze kuhakikisha kuwa wajawazito, watoto, wazee, wagonjwa na wasijiweza wanapanda bila bugudha na wanakaa kwenye viti vyao husika ndani ya basi tofauti na sasa amabao viti hivyo vinakaliwa na watu wasistahili.

Mwisho ni ombi kwa serikali kwanini wasiruhusu wawekezaji wengine wenye uwezo katika sekta ya usafiri kama Azam waingie wapewe baadhi ya ruti na waruhusiwe walete idadi fulani ya mabasi ambayo itakuwa luxury na nauli waruhusiwe kuongeza kidogo. Kwa mfano unampa Azam ruti ya Mbezi - Kivukoni au Abood unampa ruti ya Gerezani Kimara. Naamini siku serikali ikifanya hivi ndio utakuwa mwisho wa foleni mjini kwani hawa jamaa lazima wataleta mabasi yenye viyoyozi na kuboresha usafiri kwa ujumla kiasi watu wengi watapaki magari yao majumbani na kuanza kutumia usafiri wa umma.
 
Inakera sana unakuta Bus za UDART zimepark tu halafu abiria kibao...sasa sijui kama wanajua maana ya mwendo kasi ,waende ATL waone MARTA zinavyofanya kazi ili wajifunze.
 
Yaani wale madereva ukiwakuta wanabinua matako nyuki wanao tafuta maua ya kutengeneza asali.yule waziri wa utumishe nae hamna kitu pale ule usafiri ni shida
 
kiujumla Tanzania mambo mengi yenye manufaa kwa wananchi yamefeli!, taasisi za serikali tunazozitarajie zituhudumie ni rushwa na utendaji mbovu! USAFIRI - tumeshindwa hata na rwanda au kenya. public transport zipo zinawasubiri abiria wapande, watanzania tuna kuwa kama mifugo kwenye suala la usafiri. USALAMA WA CHAKULA - TBS inayomifumo ya kudhibiti usalama wa chakula lakini TBS hiyo hiyo haitekelezi mifumo yake hiyo ambayo inafanana na mifumo ya kimataifa hamna wa kuwauliza tunaoumia ni watanzania mfano mzuri juisi ya AZAM embe mwongozo unakataza CMC lakini AZAM EMBE inawekwa CMC kinyume na matakwa ya kiwango na TBS wamethibitisha usalama wake pamoja na kwamba ame declare kabisa kuitumia
 
Mimi ni sisiem na Nina smart Kadi namuomba Bimkubwa Mh Rais Samia najua Yuko bize ila siku moja tu aje pale fire just one morning weekday saa moja aone mateso ya abiria wa mwendokasi.


Good day!
Zingatia bolded.

Kulikuwa na haja gani ya kusema hivyo? Au unahisi upo kwenye kikao cha chama?
 
Fire kwenda muhimbili nayo ya kulalamika?si unatembea tu km ata moja inaweza isifike,vijana wa siku hizi nyoro nyoro sana
 
Kuna tofauti kubwa ya Tanzania na nchi nyingine zinazotuzunguka, mfano jiji la Mombasa au hata Nairobi kuna matatu za serikali, kwa sababu wana ruzuku ya serikali basi huwa zinapuyanga barabarani kila baada ya 10mins.

Unaweza kuliona matatu linakuja na ndani kuna abilia mmoja na likifika kituoni ni 30sec to minutes linaondoka haijalishi kapanda mtu au hajapanda.

Nadhani hii kitu hata ulaya ni hivyo, ila sisi UDART wanajua wanachowafanyia watanzania.
 
Kwanini tusubiri mtu kupiga simu? Hatuwezi kufahamu maslahi husika ya waliopo kituoni (wasimamizi) ingawa ni changamoto kwa watendaji kuogopa uwazi kuna haja ya kuongeza/kubadili kipengele cha mwisho wa safari kwenye stakabadhi mnaona kabisa kwamba watu wa kivukoni mpaka sasa wapo 300 kituo cha kimara, watu wa gerezani wapo 400, watu wa vituo vya kati wapo kadhaa mnatuma gari badala ya kusubiri msimamizi apige simu .. tutafika ila ...
 
Fire kwenda muhimbili nayo ya kulalamika?si unatembea tu km ata moja inaweza isifike,vijana wa siku hizi nyoro nyoro sana

Kuna wagonjwa,labda ushauri muhimbili hospital walete zile machela na vibaiskeli vya wagonjwa hapo fire.
 
Wale madereva wanaendesha kwa masaa.yale magari unayokuta yamepaki huwa madereva wake wemaliza masaa yao. Ilipaswa anayepokea awepo kabla ila ndio hivyo.sasa cha kufurahisha.akiwa kamaliza muda wake anarudisha gari kivukon kulala anapita kuanzia kimara hadi kivukon hapakii mtu.anapita kama kombora.wao hawana shida yoyote mradi kamaliza muda
Ila najiuliza kibusara kama anarudi kulaza.na abiria vituonn wapo kwa nini asirudi nao?
 
Kwanza bajaj unawah kushinda hayo.
 
Nadhan wazo zuri. Wale wale migambo wao wa kampuni ya China town sijui security wawe wanasaidia kufanya gar kwa mfano itoke level seat kwa kivukon.ili.kusudi na wa vituo vinafata wapate nafasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…