Mwendokasi nahisi ni mradi wa mtu ambaye hawezi kuguswa. Ukitafuta nyuzi za kero za mwendokasi na ushauri wa kuboresha mwendokasi hazipungui hamsini humu JF lakini hakuna hatua zozote zimewahi kuchukuliwa walau hata kupunguza kero. Hivi inshindikana nini :-
- Kuwa angalau na ofisa mmoja kila kituo ambao watakuwa na mawasiliano ya redio call wakawa na mawasiliano na incharge mabasi yanapoanzia yaani gerezani, kivukoni, kimara, moroco na mbezi. Wawe wanasiliana muda wote kujua kila wakati wapi kuna abairia wengi ili mabasi mengi yaelekezwe huko kwa muda husika.
- Kila kituo kuwe angalau na wasimamizi wa kutosha kuhakikisha abiria wanapanada kwa foleni badala ya kusukumana, kukanyagana na kuibiana.
-Wasimamizi hao hao wahakikishe kuwa mabasi yanapakia abiria kwa kiwango fulani kiasi abiria waweze kupumua vizuri na mama/dada/binti zetu wasiwe wanadhalilishwa na dunga dunga ndani ya mabasi.
- Wasimamizi hao hao waweze kuhakikisha kuwa wajawazito, watoto, wazee, wagonjwa na wasijiweza wanapanda bila bugudha na wanakaa kwenye viti vyao husika ndani ya basi tofauti na sasa amabao viti hivyo vinakaliwa na watu wasistahili.
Mwisho ni ombi kwa serikali kwanini wasiruhusu wawekezaji wengine wenye uwezo katika sekta ya usafiri kama Azam waingie wapewe baadhi ya ruti na waruhusiwe walete idadi fulani ya mabasi ambayo itakuwa luxury na nauli waruhusiwe kuongeza kidogo. Kwa mfano unampa Azam ruti ya Mbezi - Kivukoni au Abood unampa ruti ya Gerezani Kimara. Naamini siku serikali ikifanya hivi ndio utakuwa mwisho wa foleni mjini kwani hawa jamaa lazima wataleta mabasi yenye viyoyozi na kuboresha usafiri kwa ujumla kiasi watu wengi watapaki magari yao majumbani na kuanza kutumia usafiri wa umma.