Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, Saipulan Ramsey, amesema utamaduni wa 'uchawa' na kuteteana bila kuzingatia ukweli ni miongoni mwa mambo yanayoweza kukwamisha maendeleo na hata kuliangamiza taifa
Akizungumza leo Julai 21, 2026, ofisini kwake jijini Arusha, amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu kuwashambulia wanaohoji au kukosoa mambo mbalimbali, hususan kupitia mitandao ya kijamii, badala ya kujadili hoja zinazotolewa
"Sasa uchawa ni tatizo. Ni tatizo. Ndio maana nimesema, mtu anasema 'umepoa tajiri', 'ukifa huozi', anajenga ghorofa, ananunua gari. Hatusemi hivyo kwamba tuna wivu, lakini tunasema hivyo kwamba kuna vijana wengine wanakuangalia. Na nyinyi waandishi wa habari ndio vitu mnavyovipeleka sasa hivi vinakwenda viral. Yaani haiwezekani sasa hivi eti akitokea mtu akasema 'jamaa amemsifia fulani hapa', ndio mnaipeleka viral unakuta kwenye media zote inarushwa 'fulani amemsifia fulani'. Vijana wengine wanaona kumbe kuna hela rahisi inaweza ikapatikana kwa kusifia."