SAGAI GALGANO
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 50,104
- 75,552
CCM ni genge la kigaidi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendelea kutawala.
Tukio baya ni tukio baya haijalishi lini, wapi, nani, kivipi na kwa nini?Tunajadili tukio la sasa hivi, current
Labda kuna zawadiPumbaf kabisa. Mtu apigwe awe mahututi anapelekwa kituo cha afya? Halafu hapo amepewa tu bed rest wala haonekani kama mtu aliepigwa hata kofi moja. Huyu aitwe kwenye kamati ya nidhamu aadhibiwe kulingana na katiba ya chama.
Chadema haina tofauti na Taliban!Mwenezi wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAVICHA), Siglada Mligo, ameendelea kufichua kwa undani tukio lililompelekea kupigwa na hatimaye kulazwa hospitalini akiwa katika hali mahututi.
Kwa mujibu wa Mligo, tukio hilo lilitokea wakati wa kikao cha ndani cha wanachama wa CHADEMA kilichoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, John Heche. Kikao hicho kilifanyika mara baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika siku hiyo.
Mligo anadai kuwa wakati wa kikao hicho, alimuomba Heche fursa ya kuzungumza ili kuweka wazi baadhi ya masuala kwa ajili ya mustakabali wa chama. Hata hivyo, badala ya kupokelewa kwa hoja zake, alijikuta akikaripiwa vikali na Heche, hatua iliyofikia hadi kutolewa nje ya kikao kwa nguvu.
Soma Pia: Ghasia Ndani ya CHADEMA: Mwenezi wa BAWACHA Taifa ashambuliwa na Walinzi wa Heche
Baada ya kufukuzwa kutoka kikaoni, Mligo anasema alimtumia Heche ujumbe wa simu akiomba kuruhusiwa kurejea na kutoa mchango wake. Hata hivyo, badala ya kujibiwa, alidai kuwa kundi la vijana lilitumwa kumfuata, miongoni mwao akiwa mlinzi wa Heche, ambaye alimshambulia vibaya na kumsababishia majeraha makubwa.
Kwa mujibu wa Mligo, kilio chake cha maumivu kilisababisha askari waliokuwa kwenye doria kuingilia kati na kumsaidia. Askari hao walimkimbiza katika kituo cha afya kwa ajili ya matibabu.
Ukiangalia mlolongo wa tukio hili, ni dhahiri kuwa shambulio dhidi ya Mligo lilifanywa kwa makusudi, kwa lengo la kumzuia kushiriki tena kwenye kikao hicho. Swali linabaki: Je, CHADEMA kweli ni chama cha demokrasia? Chama kinachojiita cha kidemokrasia kinaweza kumdhuru mwanachama wake, tena mwanamke, kwa sababu ya tofauti za kimtazamo?
Ni wazi sasa kwamba CHADEMA chini ya uongozi wa Tundu Lissu na John Heche kinaendeshwa kwa mkono wa chuma. Wale wote wanaoonekana kuwa wafuasi wa Freeman Mbowe au wasioonyesha utii kwa Lissu wanachukuliwa kama maadui.
Tunatoa wito kwa wanaharakati wa haki za binadamu na haki za wanawake kupaza sauti kwa niaba ya Siglada Mligo. Ni muhimu kuhakikisha anapata haki yake na pia kushinikiza CHADEMA na Heche kumuomba msamaha na kugharamia matibabu yake kikamilifu.
Ukatili huu haupaswi kufumbiwa macho. Ni muhimu kuukemea sasa kabla uongozi huu wa CHADEMA haujafikia hatua ya kuhatarisha maisha ya wanachama wao kwa sababu tu ya tofauti za kimtazamo.
View attachment 3285301
Tatizo ni kuwa wanashindwa kuwakemea wale ambao wanaona chama ni chao kwa sababu waliyemuunga mkono alishinda uchaguzi. Huyu dada ni kiongozi na Heche alitakiwa kufuatilia hali yake mara baada ya tukio. Sasa hivi wamewapa CCM mtaji wa bure kabisa.Sema hili suala lina ukakasi mwingi. Na ifikie wakati CHADEMA wayavunje haraka makundi yao yaliyosababishwa na uchaguzi wao wa ndani, ili chama chao kipige hatua ya kwenda mbele.
Kwa hiyo Noel asitafutwe kwa sababu Ndugai hakuchukuliwa hatua yeyote? CDM nao wanataka kuwa na culture ya impunity kama ilivyo kwa CCM? Kuwa ruksa kumpiga mwanachama anaetofautiana na uongozi wa sasa? Hii ilikuwa nafasi nzuri ya kuitofautisha na CCM kama walivyofanya katika uchaguzi wao.Halafu Ndugai alimtandika mtu viboko hadharani, na akaachwa tu! Ila mlinzi wa CHADEMA, anatafutwa na polisi!