Mwenge, Dar: Mapambano ya Polisi na Wamachinga. Mabomu ya machozi yatembezwa

Kwanini serikali haiongei na wahusika kabla ya kuleta majanga kama haya.. tangia mwanzo!!!

Soko la wamachinga Mwenge limeshahamishwa mara mbili, mara ya mwanzo lilipelekwa Makumbusho lakini wamachinga wakarejea kinyemela then mara ya pili ulipoanza ujenzi wa majengo ya maduka mapya wamachinga wakasogezwa barabara iendayo Cocacola, lakini jamaa wakarudi kinyemela kwa kupanga vitu chini na pembezoni mwa barabara inayotokea sokoni...
 
Mwenge Kuna amanii na pisi Kali zipoo zaangaliaaa viwalio na raba za kwenda Simba daiiiii
 
Hauwezi ukatumia hekima na ukafaulu kwa wamachinga na bodaboda.
 
Bila serikali kudhibiti wafuatao, haitaweza wadhibiti

Boda boda

Machinga

Haya makundi yadhibitiwe mapema tu
 
Sipat picha kama ungelelewa na mzaz anajipatia kipato maeneo ya namna hiyo ,hii reply ungefuta tu
 
Nimepita hapo palikuwa na foleni la hatari bora ningezunguka Kawe.

Kudadek
Ni tafran

Kuna kitu kinakuwa staged nawaambia.

Polisi waache kutumia mabavu, wafanye intelejebsia na wafikirie namna ya kudeal na shida hii bila kupiga kwenzi kwenye korodani
 
Sipat picha kama ungelelewa na mzaz anajipatia kipato maeneo ya namna hiyo ,hii reply ungefuta tu
Huyo ndo taswira ya viongozi wetu.

Upumbavu mtupu walah
 
Hauwezi ukatumia hekima na ukafaulu kwa wamachinga na bodaboda.
Mimi numewahi kuwa kiongozi.

Eneo langu la utawala tuliweza kuepuka haya madhila kwa kutumia busara na hekima.

WAmachinga wanahitajika sana jamii ya uchumi wa chini.

Wafanyabiashara nao ni muhimu.

Kiongozi mwenye hekima anajua namna ya kuweka uwiano bila makundi kutafunana
 
Hakuna mmachinga anayetaka kufuata sheria, nenda Mbagala ukaone wamachinga wanavyowapa tabu wajenzi wa barabara ya mwendokasi, wajenzi wanaweka vitofali vya sehemu ya watembea kwa miguu wao wanang'oa wanavitumia! Wajenzi wanajenga mtaro wao wanatumbukiza taka za miwa, matunda na mbogamboga, ni elimu ipi uwape! Kila siku wanafukuzana na mgambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…