Mwenge - Morocco: Stendi za Daladala 6 na Traffic lights maeneo 10 kama mapambo, Panachosha lakini salama

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Ukitokea Mwenge kuelekea Morocco

Traffic lights
1. Mwenge
2. Njia panda ya ITV
3. Bamaga
4. Sayansi
5. Millenium tower
6. Makumbusho
7. Njia panda ya Mwananyamala
8. Njia panda ya Kairuki hospital
9. Njia panda ya Chato ( Vodacom)
10. Morocco

Vituo vya Daladala
1. ITV
2. Bamaga
3. Sayansi
4. Makumbusho
5. Victoria
6 Vodacom

Nawasalimu kwa jina la JMT.
 
Kulikua Hamna haja kabisa ya taa zote hizo na kwa kweli hii imekua nchi ya Jenga Bomoa Jenga Bomoa.

Barabara kama hiyo Mwenge Morocco ingewekwa njia 8 kabisa Ili angalau kwa Muda iweze kutumika sasa Bado Wanajenga kwa style ile ile Njia 4 wakati wanajua mji umekua sana huu. NJIA 2 ZIMEPITWA WAKATI.
 
Ulizia taa 1 Bei Yake ndio utajua watu wametumwa pesa
 
Ila naona wamekewa na sehemu ya mwendokasi......sio njia nane zile ?
 
Jo zinakuruka ujue
 
wataweka overpass kwenye makutano zote hapo baadae hizo taa ni suluhisho la mda mfupi tu.
 
Ni kwa sababu ya maungio nadhani... Ila zina chelewesha sana...
 
Utapitia wapi ukiwa watoka bamaga kwenda sheki ambapo hakutokuwa na mataa.......tupe hizo chocho maana taa nazo ni kero
 
Ina maana wameongeza taa tena hawa watu ni wapuuzi sana aisee😅😅😅! Mataa mengine hayana maana wangeacha za Bamaga tu na za Sayansi zile junction kama ya Victoria sio muhimu sana sababu kuna matuta
 
Badala kuondoa foleni tumeongeza. Angalia hata Barabara ya Shekilango na Sam Nujoma kutokea Mlimani City sasa kuna mi foleni ya haja
Hapa naskia harufu ya upigaji kwenye uwekaji wa hizi Taa imekuwa kama mradi wa Mtu! Njia ya Shekilango to Bamaga imejaa taa kila baada ya kilometre moja!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…