Mwenye HIV ajitangaze kwa wapenzi wake, vinginevyo Lupango?

Mwenye HIV ajitangaze kwa wapenzi wake, vinginevyo Lupango?

nilivyosisimkwa na hiyo habari, imenipasa nifikishe maamuzi yafuatayo...............!
i. kila mtu atakae gundulika anangoma, HIV, adungwe sindano ya sumu, ajifie kimya kimya, hii itakua sheria katili na mbaya sana, lakini miaka kumi mbele TANZANIA itakua taifa huru dhidi ya UKIMWI. najua nitapingwa lakini hakuna jambo zuri lisilo na gharama zake.

ii. Sheria ya juu..[proposed law] itafanikiwa ikiwa tu , kwenye bandari zetu, mipaka yetu yote, viwanja vya ndege tutaweka sheria kali na ngumu ya kupima HIV, ikigundulika Muhamiaji amenasa , ana uchaguzi adungwe sindano yetu ile ya Sumu kali sana ajifie ama ageuke na kurejea nnchini kwake haraka sana.

iii. Guest house zote zivunjwe na zifungwe....maana zaidi ya 40% ya waliopata hili janga wamelipatia katika nyumba za kulala wageni....hebu jiulize mgeni atoke Ubunge akapange chumba kule Kigamboni ama kijichi, jamani hizi nyumba ni danguro tu.

Kuna watoto wamezaliwa na huu ugonjwa na wamefika mbali sana kielimu, ungeshauri na wao wachomwe sindano wafe? Kila mtu anao uhuru wa kuishi, kama hutaki kuambukizwa Ukimwi pima mtu kabla hujatembea naye.
 
, Mh. Shabiby ni muathirika muda mrefu sana na anatembea na mabinti zetu wa chuo hawa mamiss na huwezi jua huko ndani anatumia kinga au la na hawa mabinti nao wanakuja kutembea na vijana wenzao na hawa vijana wana wapenzi wao wengine......the network goes on.....
Mh yetu macho twende kazi!!
 
Kama alivyosema mwenztu hapo juu sheria hii ipo na imeshaanza kufanya kazi toka Tarehe 1 januari 2009 ilipotangazwa na waziri kuanza kutumika. Hata hivo sheria hii inahitaji kanuni za kufanyia kazi na kanuni hizi bado zinaandaliwa.

Sheria ipi unazungumzia? Hii ya kudunga watu sindano ya sumu kama anavyopendekeza mwenzetu nguvumali sijaiona bado (-to be precise, haipo!).
 
Imefika wakati nazani jamii lazima iwe na mkakati wa kutambua wale wenye maambukizo, na watambulike katika jamii yao, huwezi kupambana na adui usiyemuona? na kama tumetangaza ukimwi ni janga la kitaifa na ukimwi upo kwenye miili ya watu bila kujua nani ameubeba basi huwezi kupambana nao.
suala la kuufanya ukimwi ni siri ya mtu tutakuja kugundua watu wote wameambukizwa.....mimi nitatoa mfano, Mh. Shabiby ni muathirika muda mrefu sana na anatembea na mabinti zetu wa chuo hawa mamiss na huwezi jua huko ndani anatumia kinga au la na hawa mabinti nao wanakuja kutembea na vijana wenzao na hawa vijana wana wapenzi wao wengine......the network goes on.....yupo bwana mmoja alikuwa na mpenzi wake ambaye alishawishiwa na shabiby wakawa wapenzi yule binti baada ya muda na starehe za muda akagundua ameathirika ila kizuri akamuambia jamaa yake kilichotokea na kumuomba amsamehe ila wasiwe na mahusiano tena....ni wachache watakao kuwa na busara ya namna hii.....zipo taarifa zisizo rasmi kuhusu hali za afya za viongozi wetu wengi....na mambo yanayofanyika kwa mfano dodoma wakati wa bunge ni ya aibu, yupo msichana mmoja pale CBE dodoma alitembea na wabunge watano kwa siku moja.....kwa wakati tofauti, na kuna waheshimiwa wengine ukisikia taarifa zao utashangaa!!!!
mimi kama ningepewa nafasi ya kupendekeza sheria kuhusu mapambano juu ya ukimwi, ningeshauri basi huu usiri wa waathirika uondolewe na hata mtu aliyekufa kwa ukimwi haijawahi kutangazwa rasmi sababu ya kifo chake....wanaficha nini?

Imetokea style moja ya wanaume siku hizi kujipima ukimwi kupitia kwa wake zao, wengi wakiwapa mimba wake zao wakazaa salama basi wanajua wapo safi lakini watu ni waoga sana kwenda kupima hali za afya yao.....

Unadhani kwa nini matangazo mengi sana siku hizi yanahusu watu kwenda kupima na kutumia Condom? Ni ili kila mtu akapime/ampime mwenzi wake au ajikinge. Sasa unamlaumia nini huyo Shabiby? Na kwani wewe ndio ulikuwa counselor wake wakati anapima ukimwi ili uwe na facts kuwa kaathirika? Huyo dada wa CBE/mabinti zenu wa chuo na hao mamiss wanaotembea na wakubwa wamebakwa???? si uamuzi wao wa kupenda shortcuts? Kwa nini wasilazimishe kuwapima au kutumia condom?
 
Tusifanye ngono zembe. Tumia condom kila mara unapofanya tendo la kujamiiana period!!
 
Basi kama ndio hivyo kuna umuhimu mkubwa sana katika sheria zetu kutunga sheria kama hiyo bila kujali anaumwa au la. ila suala ni kullinda jamii ya watu wazima na wengine
 
nilivyosisimkwa na hiyo habari, imenipasa nifikishe maamuzi yafuatayo...............!
i. kila mtu atakae gundulika anangoma, HIV, adungwe sindano ya sumu, ajifie kimya kimya, hii itakua sheria katili na mbaya sana, lakini miaka kumi mbele TANZANIA itakua taifa huru dhidi ya UKIMWI. najua nitapingwa lakini hakuna jambo zuri lisilo na gharama zake.

kama ni mwanao, mkeo au mzazi wako au wewe mwenyewe utajipa hukumu hiyo ya kudungwa sindano ujifie kimya kimya? Au unafikiria adhabu hii kwa watu wengine tu wasiohusiana na wewe? Just for your thoughts.

ii. Sheria ya juu..[proposed law] itafanikiwa ikiwa tu , kwenye bandari zetu, mipaka yetu yote, viwanja vya ndege tutaweka sheria kali na ngumu ya kupima HIV, ikigundulika Muhamiaji amenasa , ana uchaguzi adungwe sindano yetu ile ya Sumu kali sana ajifie ama ageuke na kurejea nnchini kwake haraka sana.

Itakuwaje na yule mwenye kudunga wenzake sindano naye anao?

iii. Guest house zote zivunjwe na zifungwe....maana zaidi ya 40% ya waliopata hili janga wamelipatia katika nyumba za kulala wageni....hebu jiulize mgeni atoke Ubunge akapange chumba kule Kigamboni ama kijichi, jamani hizi nyumba ni danguro tu.

mmh nadhani liko kwenye kujamiiana siyo kwenye nyumba; maana watu wanajimiiana hadi kwenye vichaka, kona za nyumba, kwenye magari, n.k
 
Wanachofanya hapa ni kuwa kila mtu ambaye ana HIV yuko kwenye database na anajijua kuwa anayo na anapewa angalizo kuwa kuanzia sasa ni lazima amwambie mtu yeyote atakayepanga kukutana naye kimwili (yaani full disclosure); kushindwa kufanya hivyo na kumuambikiza mtu mwingine ni kosa la jinai.

Hivyo, kama nimeambukizwa na ninajua kuwa nimeambukizwa (maana data zipo) halafu nikaenda kukutana na x naye akaambukizwa halafu anakuja kuuliza kama nilikuwa najua nimeambukizwa nami nasema hapana lakini wakienda kwenye taarifa za hospitali wanaona kuwa ndiyo nilikuwa najua basi yule dada anaweza kufungua mashtaka ya kushambuliwa na silaha ya mauaji (HIV).
 
Hii nzuri nadhani nivema Tz tukaiadapti.Itasaidi kupunguza maambukizi yanayoepukika.
 
Wanachofanya hapa ni kuwa kila mtu ambaye ana HIV yuko kwenye database na anajijua kuwa anayo na anapewa angalizo kuwa kuanzia sasa ni lazima amwambie mtu yeyote atakayepanga kukutana naye kimwili (yaani full disclosure); kushindwa kufanya hivyo na kumuambikiza mtu mwingine ni kosa la jinai.

Hivyo, kama nimeambukizwa na ninajua kuwa nimeambukizwa (maana data zipo) halafu nikaenda kukutana na x naye akaambukizwa halafu anakuja kuuliza kama nilikuwa najua nimeambukizwa nami nasema hapana lakini wakienda kwenye taarifa za hospitali wanaona kuwa ndiyo nilikuwa najua basi yule dada anaweza kufungua mashtaka ya kushambuliwa na silaha ya mauaji (HIV).
Nimekupata vizuri sana Mzee Mwanakijiji.ila tatizo kubwa tulilonalo Tanzania ni record na control ya watu wetu..kwakweli Serikari isipolitilia mkazo suala hili hatutapiga hatua yoyote kimaendeleo na itakuwa kama mchezo wa kuigiza. kwa mantiki hiyo basi,ni kweli watu wengi wanaitikia wito wa kupima na kujijua hali yao, ila asilimia 98 ya watu hao wanapoenda kupima wanatoa information fake yani majina ya uongo ilimradi kuogopa majibu yake kusambaa mtaani.

Vitu kama hivi vinaifanya sheria hiyo iliyosiniwa na rais kufail kwa mfano leo nimeenda mabibo nimepima na nimepata majibu yangu kama nimeathirika,na wakati napima nimeacha infos si za kweli na wala sijaacha picha yangu. kesho keshokutwa kwakuwa nimeshajijua hali yangu naendelea kuusambaza..Je mahakama itaitumia vipi sheria hiyo kunifunga wakati haina uthibitisho wowote kama nilikuwa najijua kama nimeathirika na nimeendelea kuambukiza wengine???

Kwa sasa mi nafikiri suala la database na control ya watanzania ndiyo lingekuwa jambo la kwanza kwa serikali kulifanyia kazi kikamilifu,na baada ya hapo basi matunda yake yataanza kuonekana,Maajali yatapungua matendo ya uvunjaji sheria yatapungua,umasikini utapungua na mengineyo mengi.

Nchi zilizoendele sheria hiyo ipo na inafanya kazi vizuri sana. na ukibainika umemuambukiza mtu wakati unajijua utamlipa muathilika huyo fedha nyingi sana na utatumikia kifungo kwa mujibu wa sheria..sheria kama hii tunaihitaji sana Tanzania..
 
Hivi bongo tuna database za kitu chochote kweli?

Na hapa sizungumzii Dar tu peke yake...nazungumzia Peramiho, Ikwiriri, Meadu, Kanadi, Ibinzamata, Tukuyu, nk.
 
Julius.. database zipo.. nyingi tu na karibu za kila kitu; tatizo lake ni kuziaccess..
 
Julius.. database zipo.. nyingi tu na karibu za kila kitu; tatizo lake ni kuziaccess..

Zipo wapi na za aina gani? Electronic? Kwa mfano wewe sasa hivi hapo kijijini ukiwa na arrest warrant halafu ukimbilie Marietta kwa yule mdosho halafu itokee siku uwe pulled over, najua unajua utakuwa kwenye deep trouble maana jamaa hawatakuachia. Utapigwa pingi kama zile za Muro halafu utarudishwa kijijini kujibu mashitaka. Tena siku hizi wakikusikia una ka accent wataangalia na immigration status yako papo hapo kwenye gari zao.

Kama ulikuwa na credit cards zilizotolewa na BoA halafu zimekuwa charged off....miaka mitano baadae unakwenda Wells Fargo kuomba mkopo wa nyumba (mortgage loan) utatoswa kwa sababu una deliquent credit. Taarifa zote zipo kwenye database.

Almost kila kitu huko kijijini kipo kwenye database....hata medical na dental records...na kama ingawa kuna patient/doctor confidentiality lakini mbele y subpaena hiyo confientiality haina nguvu.

Sasa bongo zipo wapi? Tuna miuondo mbinu kweli inayowezesha hizo database kufanya kazi vizuri?
 
Inatakiwa ifikie wakati serikali kupitia bunge lake, lipitishe sheria ya kupima UKIMWI kwa kila Mtanzania na wageni wote wanaotembelea Tanzania kuwa ni lazima na si jambo la hiyari... Serikali ikisha pitisha hiyo sheria ndio kuwe na kifungu kidogo cha sheria kitakacho mlazimisha muhathirika kujitambulisha kwa partner wake... Vile vile kuwe na kipengere cha kuwabana wale wote watakao wanyanyapaa waathirika kwenye shughuli za kikazi na za kijamii.
 
Yafuatayo naamini yatatusaidia

1. Iwe ni marufuku kwa mwanamke na mwanamme kuruhusiwa kuingia gesti au katika hoteli bila cheti cha ndoa.

2. Ifanyike kampeni ya nguvu kitaifa kuwa hata ukitumia Kondomu kwa tendo la Kujamiana jua kuwa Ukimwi utaupata tuu---Kwa kweli matangazo ya Kondomu kimsingi ndiyo yanachangia kwa kiasi kikubwa sana watu kuona kuwa ni salama kufanya tendo la ndoa na mtu yeyote ili mradi unazo Kondomu.

3. Kila mmoja wetu ajichukulie kuwa ni muathirika.

4. Ukifanya Tendo la Ndoa na Mtu Yeyote yule ambaye si Mkeo/Mmeo iwe ni jela miaka 15.
 
campaign za condom zimekaa kibiashara zaidi, maana tangia hayo matangazo yaanze ndio kwanza maambukizo yameongezeka.... kama moto na nyika.
 
Yafuatayo naamini yatatusaidia

1. Iwe ni marufuku kwa mwanamke na mwanamme kuruhusiwa kuingia gesti au katika hoteli bila cheti cha ndoa.

itakuwaje kama ni mtu na dadake; mtu na binti yake (vyumba tofauti)? Na itakuwaje ni watu wazima ambao hawataki kufunga ndoa lakini ni wapenzi? Itakuwa ni kinyume cha Katiba kwani huwezi kumshurutisha mtu kuoa na huwezi kutunga sheria ambayo inalenga kuwabagua watu fulani kwa sababu ya hali yao ya ndoa (marital status)

2. Ifanyike kampeni ya nguvu kitaifa kuwa hata ukitumia Kondomu kwa tendo la Kujamiana jua kuwa Ukimwi utaupata tuu-

kuna ushahidi gani wa kauli hii?

3. Kila mmoja wetu ajichukulie kuwa ni muathirika.

kama kila mmoja akichukulia kuwa ni muathirika huoni kuwa kunahalalisha kujamiiana? kuna ubaya gani waathirika kwa waathirika wakijamiiana?
 
Tatizo la ukimwi ni kwamba mtu haogopi tena sheria yoyote.

Tatizo la pili ni tamaduni zetu. Sheria haitasaidia kitu, labda kama kuwe na udikiteta fulani wa kwamba majibu ya ukimwi siyo siri tena.

Na ili upewe huduma fulani lazima uende na cheti kuonyesha umepima ukimwi, kila mwezi lazima uki renew cheti.
 
Sasa bongo zipo wapi? Tuna miuondo mbinu kweli inayowezesha hizo database kufanya kazi vizuri?

Julius.. umechanganya mambo mawili lakini swali lako la mwisho ndilo la msingi. Taarifa zote ambazo zingeweza kutumika kama zinavyotumika kijijini hapa zipo Tanzania. Kuanzia taarifa za kuzaliwa, uhalifu, immigration, afya n.k Tatizo liko kwenye organization, availability, accessibility n.k

Kina JK wanataka kujenga mabarabara ya kwenda juu kwa juu wakati kama wangetoa ajira ya watu wachache kukaa chini na kuanza data entry ya taarifa mbalimabli kwenye somesort of national database (najua wanafanya hivyo sehemu chache) wangeweza kuhakikisha within few years taarifa zote muhimu zinapatikana kwa kutumia mtandao.

Ningekuwa mimi ningetengeneza kwanza National Database and Statistics Clearing House ambayo itakusanya taarifa zote ambazo ni za public zinazoingia kutokana na kuzaliwa na vifo, ajira, n.k na kuweka makao yake makuu somewhere in Dodoma na vitengo vyake mbalimbali huku unaweka backup yake Kigoma na Mtwara na labda moja digitally somewhere outside the country.

Unaweka taarifa zinazotakiwa kuwa updated daily, weekly, monthly na zile ambazo zinakuwa archived n.k Hii inaitwa miundombinu ya kisasa (modern infrastructure).

Kilichopo sasa hivi ni fragmentation ya taarifa mbalimbali kitu ambcho hata Wamarekani bado kinawasumbua sana (as we have seen in the attempted X'mass bombing). But we have to start somewhere with something small and increase progressively.
 
Back
Top Bottom