Mwenye jengo akamatwe, eneo liuzwe, mali zake zifilisiwe, halafu hela zote wapewe majeruhi na waliofiwa


Kwa hivyo engineer alijiamulia kuchimba chini au alipewa maelekezo na mwenye jengo?. Mwenye jengo Hana sehemu ya kukwepa.
 
Kwa hiyo bidhaa zitakuwa zinajiweka na kujitoa zenyewe!?
 
Mkuu mwenye Jengo Hana shida.. Hapa WA kufilisi ni wale waliotia sahihi na mihuri kwenye vibali hawa wanapaswa kufilisiwa na kutaifishwa kila kitu pamoja na kuondolewa kabisa kwenye mfumo . Hii italeta uwajibikaji

Mwenye jengo pia anahusika. Amefanya kitu hatarishi
 
Akamatwe haraka Sana kwa kosa la Negligence
Afikishwe mbele ya vyombo vya sheria na wananchi wote tujue au tujulishwe namna kesi yake inavyokwenda.

Akiachwa wengine wataendelea kufanya ushenz kama huu kwa vile wanajua hawafanywi kitu.
 
Hivi matajiri unawajua kweli!?
 
Tofautisha man made calamitiea na force majeure calamities. Ajali ya kariakoo ni man made calamity sio force majeure Kama tetemeko au mafuriko. Uwe mtu mwelewa saa zingine.
ajali ya barabarani au ajali ya majini ni natural hazards sio gentleman na ndugu muerevu na muelewa sana?

kwahiyo uchome misitu, ukate miti usababishe mmomonyoko wa aridhi, ukame na njaa, uzibe mitaro usababishe mafuriko mpaka ndani ya nyumba yako halafu eti uje hapa eti ng'we ng'we ng'we sijui tofautisha nini na nini huko, alaaaa!🐒
 
Alifanya Jambo la hatari Sana. Na wote waliomruhusu inatakiwa wachukuliwe hatua.
Ikibainika kuwa jamaa ametumia njia za panya kupata vibali vya ujenzi. Basi sikata hili litaondoka na wengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…