Nimekosea, Prophet Muhammad wrote Medina Constitution not Mecca constitution
Evidences are everywhere...u can search for yourself hata ukigoogle
Kama ambavyo wewe bibi huwa unawaambia members hapa wajisomee...nawewe jisomee kuhusu katika ya medina aliyoiandika Muhammad
Muhammad ndiye binadamu wa kwanza kuanzisha Pure Islamic secular state.
Mji wa Madina uko ukanda wa Magharibi ya pwani ya ghuba ya Arabuni ndani ya Mkoa uitwao Hijaz, takribani maili 90 mashariki mwa fukwe za Bahari Nyekundu, na maili 290 kaskazini mwa Maka. Madina, mji alioishi Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, ina nafasi adhimu ndani ya moyo wa kila Muislamu
Al-Madina al-Munawwarah, al-Barrah, al-Jabirah na Taiba ni majina machache tu miongoni mwa majina 100 au zaidi ambayo Waislamu wameupa mji huu unaopendwa ambao unasimama kama mji wa pili mtukufu na muhimu katika Uislamu baada ya Maka. Historia yake ni tajiri mno, na nafasi yake ni kubwa mno katika Uislamu kiasi kwamba hakuna mji mwingine ulioweza kukaribiana nao.
Madina ndiko uliko Msikiti wa Mtume, swallallahu alayhi wa sallam. Pia ndiko uliko Msikiti wa kwanza kabisa kujengwa katika Uislamu, Masjid Quba, ambao Mtume binafsi, alisaidia kuusanifu na kuujenga. Madina ndio mji wa Ansar (wasaidizi au masapota), ambao walitoa kila kilichokuwa chao kumsaidia Mtume wa Mwenyezi Mungu.
Madini ndio mji Mkuu wa serikali ya kwanza ya Kiislamu iliyoongozwa na Makhalifa, ndio mji uliohifadhi Uislamu, na kuusambaza ujumbe wake ulimwenguni kote, na hadi leo unafanya hivyo.
Ama kwa hakika imani ya Kiislamu inarudi tena kutafuta hifadhi Madina kama nyoka anavyorudi shimoni mwake kujihifadhi.” (Bukhari na Muslim).
Madina ndio mji ilimofanyika Hijra, na ndio mji unaojitokeza kifua mbele katika zama na kumbukumbu za Uislamu. Ndio mji ambao tende zake zinatibu maradhi, na ndio mji ambao watu wake wana nyoyo laini kwelikweli na wana khulka njema kabisa. Hizi ni baadhi ya sababu ambazo kwazo Waislamu wanaipenda Madina, wale ambao hawajafika Madina, wanaiotea ndoto ya kuizuru siku moja inshaAllah.
Lengo kuu la ziara hiyo, bila shaka, litakuwa ni kuuzuru Msikiti wa Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, kwani Mtume amesema, “msifanye safari katika msikiti wowote (kwa nia ya kupata fadhila au jazaa maalum ya Swala) isipokuwa Misikiti mitatu, nayo ni al-Masjid al-Haram, al-Masjid al-Aqsa, na katika msikiti wangu.” (Bukhari).
Lakini punde tunapokuwa Madina, tuzidishe fadhila zetu kwa kutembelea maeneo mengine maalum ya Kiislamu, kupata maarifa ya dini yetu, na kuimarisha imani zetu juu ya Mwenyezi Mungu.
Na japokuwa Waislamu wengi watazuru Madina kama sehemu ya Hija yao lakini ziara hiyo si sehemu ya hukumu za Hija wala Umra. Ni wema na heshima tu maalum ambayo inahusishwa na Mji huu wenye Nuru ya kipekee inayowavutia na kuwatia Waislamu hamasa ya kutenga muda na kuja kwa vipando kutoka pembe zote za dunia kupata fadhila zote wanazoweza kuzipata.
Nimekosea, Prophet Muhammad wrote Medina Constitution not Mecca constitution
Evidences are everywhere...u can search for yourself hata ukigoogle
Kama ambavyo wewe bibi huwa unawaambia members hapa wajisomee...nawewe jisomee kuhusu katika ya medina aliyoiandika Muhammad
Muhammad ndiye binadamu wa kwanza kuanzisha Pure Islamic secular state.