Mwenye kujua asili ya utawala wa Saudi Arabia anijuze

Mwenye kujua asili ya utawala wa Saudi Arabia anijuze

Mikitaka ajira huku Saudi Arabia njooni mujiandikishe mapema kama wenzenu wa Kenya na wa West Afrika wapo kibao!!!

mengine mtajifunzia hukuuku
 
duh sasa mbona saudi arabia haitaki kusaidia waislamu wenzake watu wa siria kuwapa makazi ya muda , kweli na historia yote hiyo inashindwa kutoa msaada mpaka inafikia waislamu wanaenda kupewa hifadhi na nchi za wagalatia kama ujerumani duh kweli sometime dini izi noma sana , muislam yupo lazi apigane kwa mtu kuchona kitabu chao ila kumsaidia muislamu mwenzake ni ngum
ule utawala wa pale haupo kwa ajili ya maslahi ya waislam na waislam ,japo uwepo wao pale umejifunika kwa joho ya kiislam
 
ule utawala wa pale haupo kwa ajili ya maslahi ya waislam na waislam ,japo uwepo wao pale umejifunika kwa joho ya kiislam
Zama za mwisho kabisa hizi,ndugu zanguni tunaelekea kwenye mass extinction dalili zote zinaonyesha.
 
Mji wa Madina uko ukanda wa Magharibi ya pwani ya ghuba ya Arabuni ndani ya Mkoa uitwao Hijaz, takribani maili 90 mashariki mwa fukwe za Bahari Nyekundu, na maili 290 kaskazini mwa Maka. Madina, mji alioishi Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, ina nafasi adhimu ndani ya moyo wa kila Muislamu
Al-Madina al-Munawwarah, al-Barrah, al-Jabirah na Taiba ni majina machache tu miongoni mwa majina 100 au zaidi ambayo Waislamu wameupa mji huu unaopendwa ambao unasimama kama mji wa pili mtukufu na muhimu katika Uislamu baada ya Maka. Historia yake ni tajiri mno, na nafasi yake ni kubwa mno katika Uislamu kiasi kwamba hakuna mji mwingine ulioweza kukaribiana nao.
Madina ndiko uliko Msikiti wa Mtume, swallallahu alayhi wa sallam. Pia ndiko uliko Msikiti wa kwanza kabisa kujengwa katika Uislamu, Masjid Quba, ambao Mtume binafsi, alisaidia kuusanifu na kuujenga. Madina ndio mji wa Ansar (wasaidizi au masapota), ambao walitoa kila kilichokuwa chao kumsaidia Mtume wa Mwenyezi Mungu.
Madini ndio mji Mkuu wa serikali ya kwanza ya Kiislamu iliyoongozwa na Makhalifa, ndio mji uliohifadhi Uislamu, na kuusambaza ujumbe wake ulimwenguni kote, na hadi leo unafanya hivyo.
Ama kwa hakika imani ya Kiislamu inarudi tena kutafuta hifadhi Madina kama nyoka anavyorudi shimoni mwake kujihifadhi.” (Bukhari na Muslim).
Madina ndio mji ilimofanyika Hijra, na ndio mji unaojitokeza kifua mbele katika zama na kumbukumbu za Uislamu. Ndio mji ambao tende zake zinatibu maradhi, na ndio mji ambao watu wake wana nyoyo laini kwelikweli na wana khulka njema kabisa. Hizi ni baadhi ya sababu ambazo kwazo Waislamu wanaipenda Madina, wale ambao hawajafika Madina, wanaiotea ndoto ya kuizuru siku moja inshaAllah.
Lengo kuu la ziara hiyo, bila shaka, litakuwa ni kuuzuru Msikiti wa Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, kwani Mtume amesema, “msifanye safari katika msikiti wowote (kwa nia ya kupata fadhila au jazaa maalum ya Swala) isipokuwa Misikiti mitatu, nayo ni al-Masjid al-Haram, al-Masjid al-Aqsa, na katika msikiti wangu.” (Bukhari).
Lakini punde tunapokuwa Madina, tuzidishe fadhila zetu kwa kutembelea maeneo mengine maalum ya Kiislamu, kupata maarifa ya dini yetu, na kuimarisha imani zetu juu ya Mwenyezi Mungu.
Na japokuwa Waislamu wengi watazuru Madina kama sehemu ya Hija yao lakini ziara hiyo si sehemu ya hukumu za Hija wala Umra. Ni wema na heshima tu maalum ambayo inahusishwa na Mji huu wenye Nuru ya kipekee inayowavutia na kuwatia Waislamu hamasa ya kutenga muda na kuja kwa vipando kutoka pembe zote za dunia kupata fadhila zote wanazoweza kuzipata.
Kumbe we ni muoga na mnafiki,umeulizwa swali ujibiwe huku ukijua wazi kuwa na wewe wajua pengine zaidi ya watakao kujibu ili update sababu ya kuyaongea hitoria yako,kumbe ungeweza kusimulia uyajuayo kwa manufaa ya wengi wanaopenda kujua historia uijuayo.
 
inawezekana nikawa mnafki kwako na muoga kwenye macho yako ,ila nisiwe muoga wala mnafki wa nafsi yangu...
Naww ambaye unajionyesha si muoga au mnafki ,na ukawa ninafki wa na muoga wa nafsi yako mwenyewe...

Swali nililouliza ni utawala na si miji ya maka au madina ,

Nilitaka kujua zaidi asili ya utawala huu ,na kwanini tawala huu umeendelea kuwepo madarakani mpaka sasa ,kuliko tawala zingine zote na huwa hauguswi kuna sili gani nyuma yake,

Ndicho nilichotaka kujua ,

Nikusaidie kitu ,usipende kutosheka na unachojua ,heri ujifanye mjinga ili upate kujua zaidi kutoka kwa wengine ,

maana sio yote utayajua ,.

Ili uwelewe Historia ya mahali flani au watu lazima ukubali kujifunza kwa watu mbali mbali
 
Hayo yote unayajua shekhe basi tu umeamua tu haya bana.
 
Back
Top Bottom