Mwenye Kujua channel inayoonesha SportPesa supercup

Rejea kichwa Habari hapo juu
Naomba kujuzwa iwapo Mashindano hayo yataoneshwa live na channel hiyo

Nilimsikia Mtangazaji Bernard James asubuhi ya leo akiwa anatusomea Vichwa vya Habari vya Magazeti na akasema kwamba Michuano hiyo itaonyeshwa na Channels za Startv na Starsports. Hivyo nami pia nasubiria hiyo Saa 10 ifike ili nione Sahara Media ni Waongo au Wakweli!
 
Ngoma IPO live mkuu sasa hivi
 
Startv mbona matangazo yenu yana katakata sana? Tatizo ni nini? Na kwani hamkujiandaa mapema kwa changamoto?
 
Nafuatilia matangazo ya moja kwa moja ya mechi ya mpira wa miguu kati ya Yanga na Kakamega Home Boyz ya Kenya kupitia channel yetu hii ya hapo Mwanza (Star Tv)
Kiukweli Tv hii bado sana, yani bado mno kiteknolojia maana hata kama wanapokea matangazo kutoka kituo kingine lkn ni dhahiri kabisa tatizo hili la kukatikakatika na kukwama kwa picha si la kituo wanachopokea ila ni lao. Ubora wa picha na utulivu ni mbovu mno kiasi kwamba hakuna maana yoyote kwa kituo hiki kurusha live mtanange huu wa SportsPesa.
Bongo ni Azam tu wengine miyeyusho, nimezima Tv.
 
Usikasirike mkuu nenda kbc
 
Hizi ndizo sababu Kuu za Yanga SC kufungwa ambazo Kocha wao Mwandila amesema muda mfupi baada ya kutoka kufanya ' post match interview ' Uwanjani...
  1. Schoolboys mistakes na hapa amewalaumu sana Mabeki wake kwa uzembe usiovumilika
  2. Injuries akisisitiza kwamba Timu imeenda huko ikiwa na Wachezaji wagonjwa huku wengine wakiwa bado hawa ' match fitness '
KINACHONISHANGAZA

Katika Interview yake jana huyu huyu Kocha Mwandila pamoja na Nahodha wake Thabani Scara Kamusoko walijinasibu kabisa kwamba Yanga SC haitorudia makosa na kwamba katika michuano hii watafika hadi Fainali na kuchukua Kombe ili wakacheze na Everton ya nchini Uingereza na wakaahidi kwamba leo watawafunga hawa Kakamega Homeboys goli nyingi tu lakini nashangaa katika mahojiano yake ya leo kabadili maneno yake.

Poleni sana Yanga SC na sasa subirini Wanamume Simba SC tuwafutieni ' aibu ' Kesho kwa kushinda ili tulichukue hili Kombe tukaitangaze vyema huko kwa Mama Theresa May na Queen Elizabeth.
 
Ndo maana Mkuu wangu.Kwakweli hawa Jamaa wa Star TV wajirekebishe.Kwani walishikiwa Kiboko wakubali kuonyesha hiyo Mitinange??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…