Mwenye kujua mbinu za kusevu pesa aniambukize jamani,

Mwenye kujua mbinu za kusevu pesa aniambukize jamani,

Bora nile bata mda huu sina majukumu mengi zaidi ya kujilisha kujivika na kujilaza..

Nikiwa na majukumu zaidi ya haya nita save.. Saizi nakula bata kwanza baadae huko Mungu akijalia uhai kitaeleweka tu.

Saivi nahitaji uhakika wa kunywa walau beer tatu kwa siku na kula vizuri kila siku. Hayo mengine kwangu bado naona itakuwa too much
Hahaha...una Miaka mingapi kazini?
 
hobby ya kwanza napenda soccer

hobby ya pili napenda kusikiliza music

hobby ya tatu kwa sasa ni kubet [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16]
hapa nachaniwa mikeka kishenz [emoji16] [emoji16] [emoji16]
Hiyo ya kubeti asee...hahaha..Jaribu kuiacha, mi mwenyewe ni muhanga wa kubeti....asee, Tangu nianze kubeti ndo mwanzo wa kuishiwa hela, Zamani nilikuwa na ziada ya hela...ila siku hizi hela mifukoni sizioni, kidogo tu kubeti.

Nimejiamulia kuacha kubeti, Nikishindwa sana nitapunguza.

Ila Kubeti Big NO.
 
Kusave pesa haijawahi kuwa kazi rahisi mkuu, hata kama mshahara ni mkubwa, utajitahidi kuzitunza lakini zitaisha tu bila hata kutegemea na ukijiuliza cha maana ulichofanyia wakati mwingine hukioni.

Nakushauri kama umeona umeshindwa kabisa fanya haya yafuatayo:

1. Tafuta project ya kufanya halafu kakope pesa benki utakuwa unarejesha polepole kulingana na utaratibu utakowekwa.
2. Nasikia kuna account zinaitwa malengo account kwenye mabenki kadhaa, kaziweke huko kwa muda utakaokuwa umeridhia mwenyewe kulingana na utaratibu wa benki husika.( japo hii siiafiki sana ).

Nimezungumzia kwa wale waajiriwa na pesa yao inakatwa moja kwa moja kwenye mshahara, kitakachokuwa kimebaki naamini utakitumia kwa nidhamu ya hali ya juu.

Kwa waliojiajiri wenyewe nawashauri waongeze mtaji kutoka kwenye faida wanayopata, kuwa na pesa nyingi zilizotunzwa ni kukaribisha ibilisi hatari sana wa matumizi.

Kwa wale walioweza kutunza pesa kwa muda mrefu niwapongeze sana maana ni kipaji na uvumilivu wa hali ya juu sana.

Kwa sasa ni hayo tu mkuu.

Huu uzi ulenivutia kwasababu nimejaribu kutunza fedha kwa ajili ya projects na mara nyingi bila ya sababu ya msingi Nimekua nikizitumia au kumsaidia mtu na kuanza upya.

Hiyo mbinu namba 1 ndiyo imekua mkombozi kwenye projects zangu nyingi japo ni muhimu sana kuiangalia Riba ya mkopo....
 
Tengeneza buget...cut unnecessary spending. Nununua vitu vya jumla mwazoni mwa mwezi....alafu hela ya matumizi madogo madogo kama nauli weka home. Kila siku unaandika matumizi yako hata kama ni sh. 100. Living within a budget inanisaidia sana kusave
Kweli kabisa.... Pia achana na simu banking nikimaanisha usiwe access ya haraka ya kutoa pesa.Mimi ATM kadi yangu ili expire, sija renew ,pesa ikiingia huko mpaka niitoe nipange mstari so uwa naiachaga tu nategemea mishe zingine
 
Tafuta kitabu changu nilicho andika mwaka jana kinachosema "HOFU YA NINI: Matumizi bora ya kipato kwa maendeleo ya jamii au binafsi. kitakusaidia kuwa na mpangilio mzuri wa mapato yako. vipo Bookshop nyingi labda viwe vimeisha natumai utavipata
ntakitafuta
 
Hiyo ya kubeti asee...hahaha..Jaribu kuiacha, mi mwenyewe ni muhanga wa kubeti....asee, Tangu nianze kubeti ndo mwanzo wa kuishiwa hela, Zamani nilikuwa na ziada ya hela...ila siku hizi hela mifukoni sizioni, kidogo tu kubeti.

Nimejiamulia kuacha kubeti, Nikishindwa sana nitapunguza.

Ila Kubeti Big NO.
mzee baba hii kuacha ngumu, nliwai pga milion 1, [emoji2]
 
Back
Top Bottom