Mwenye kujua, nje ya Medical Doctor (MD), course gani nyingine ipo kwenye soko miaka 3 hadi 4 ijayo?

Mwenye kujua, nje ya Medical Doctor (MD), course gani nyingine ipo kwenye soko miaka 3 hadi 4 ijayo?

Cheki kozi nyingine usipende kulazimisha mambo..mbona kuna maisha yanaendelea tena vzr zaidi hata ya walio na MD acha kasumba..tena baada ya miaka 5 MD wa tz wataanza kubeba bahasha kitaa.

Kapige famasi..medical lab..Environmental health Sciences..biomedical n.k

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Msaada wenu ndugu zangu wa dharura

Nina mdogo wangu amechaguliwa mipango tu kwenye 1st round aka confirme, ilipotangazwa 2nd round akaomba tena akapata aridhi university, ila aridhi wamekataa kumtumia code kwaajili ya ku confirme kwa kuwa wanasema ameshapata chuo kingine,

otherwise aombe mipango wamuondoe kwenye selection, moyo wake wote upo aridhi na iyo course aliochaguliwa chuo cha aridhi ndio ilikuwa ndoto yake kusoma, na kesho ndio mwisho wa ku confirme chuo naombeni msaada wenu kwenye ili afanyaje ili aweze kupata chuo cha aridhi.

Msaada wenu ndugu zangu wa haraka.
 
Nilikuwa naipenda hii kozi lakini ghafla ilinitoka aisee..kwanza waombaji ni wengiii mno afu maisha ya kazini ni kujitoa sana yaani unaanzia kuteseka ukiwa unasoma hadi unafanya kazi...
Mhh labda ulikua tu kilaza mkuu, neurosurgeon anaweza mwezi akaona mgonjwa mmoja tu, ila akavuta mpunga mara kumi ya huko ulipokimbilia
 
kuna wale wanao soma vikoz vya kawaiwa tu wanamaisha bomba kinyama
Wachache sana, ni ngumu sana kumkuta MD analipwa chini ya Milioni ila ni rahisi sana kuwakuta wahasibu hawana hata hizo ajira zenyewe, ingawa wenzao wengine wanakula milioni 6+ B. O. T.
[emoji28][emoji28]
 
Yah..kuna vikozi vya kawaida lakini ukipata kazi umetoboa..sasa Hiyo MD dah!.. Kinachoniuma zaidi kila aliyesoma PCB anang'ang'ania iyo iyo ushindani mkubwa..hata ukimshauri mtu aombe kozi ingine ya afya hataki...yaani sasaivi round 2 kuna watu wataomba tena iyo iyo na wakati round 1 walikosa..
MD dunia nzima ina ushindani sio tu Tanzania, kua kilaza ama kushindwa kusoma MD hakuifanyi sociology, ama marketing kua na thamani kuliko MD? [emoji38][emoji38]
 
Mkuu believe me, unapohitimu udaktari na ukajua kutibu hata siku moja hutoona uzito kwenye majukumu yako.. Hivyo usifikiri wale wanaotibu watu wanateseka kwenye majukumu yao.

Unasema hivyo kwa kuwa labda hukuipata hiyo nafasi ila amini ninachokuambia.

Kuhusu kupata nafasi ya kusomea MD, of coarse competition ni kubwa.. Ila ukipata nafasi hutojutia.

Zipo course ndogo ndogo ambazo watu wanapiga pesa sana, nakubali.. Lakini omba uwe na bahati!

Mimi nina rafiki yangu alisoma PCM akapata kozi ndogo tu ya science pale CBE ya 3 years inaitwa Metrology (kama sikosei) - inahusika na masuala ya vipimo (ni mpya mpya), mwaka aliomaliza ndio mwaka huo huo wanaajiriwa mawakala wa vipimo wa serikali pale bandari.

Sasa hivi ninavyoongea jamaa anamalizia nyuma yake ya pili, moja ikiwa ya ghorofa. Ni bahati sometimes!
Umeelezea Kisomo sana, kwa **** mtu kasoma Archeology akabatika kubaki chuo apige pindi, basi kila akikutana na madogo anawashauri wapige mapindi
 
Ni kweli lakini..ukubali ukatae...kazi ya udaktari ya kujitoa sanaa...afu kingine hiyo kozi sasaivi ina competition kubwa kuliko zamanii...tena sio kitoto...hata vyuo vya private kupata nafasi bila div 2 ya kwanza hupati... Kuna rafiki yangu ana divi 2/12 ameachwa palee st fransis...
Shida sio kazi ya udaktari, shida ni kupata hio nafasi ya kusoma huo udaktari, acha basi kufananisha hizo concept mbili tofauti
 
Kasome Dental ukijiajiri baadae hutajuta.
 
Dental we unakua unadeal na meno tu..... Yaani meno tu hadi unazeeka....... MD, unaweza kua neuro, cardio, nephro etc
We jamaa unareply tu comments bila hata kusoma... Mshakji amesema akasome dental baadae ajiajiri...wewe unaanza kusema MD anaouwezo wa kuwa neuro, cardio...
 
MD dunia nzima ina ushindani sio tu Tanzania, kua kilaza ama kushindwa kusoma MD hakuifanyi sociology, ama marketing kua na thamani kuliko MD? [emoji38][emoji38]
Jamaa kusoma MD unajiona genius sana na kuita wenzako vilaza..anyway nimetoa sababu zangu binafsi..na nikweli mimi kilaza lakini hatakama nisingekuwa kilaza nisingesoma MD...wewe baki unapoamini...madaktari wenyewe ukiwaambia unaenda kusomea udaktari wanakwambia bora ukasome phamarcy kuliko hiyo...sasa nani anataka apoteze miaka 6
 
Back
Top Bottom