Mwenye kulijua hili anisaidie haraka

Mwenye kulijua hili anisaidie haraka

ufumawicha

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
504
Reaction score
209
Mdogo wangu aliachwa na mkewe mwaka mmoja uliopita.Katika hali isiyokuwa ya kawaida akamuandikia barua kuwa hamtaki tena na akamkabidhi barua hiyo mbele ya mtendaji.
Agosti 2016 akaenda mahakamani kudai talaka.Jana hakimu katoa uamuzi huu,kuanzia leo mko huru.Wa kuoa aoe na wa kuolewa aolewe.Nendeni nyumbani na muhesabu siku 45 toka leo halafu mrudi hapa mahakamani kwa hatua ya mwisho.Ila kila mmoja wenu itabidi ajigharamikie kwa gharama hizo ndogo.

Ninachoomba mnieleweshe hizo gharama ni za nini?Au ndoa ikivunjwa mahakama inatoa hati za talaka?
 
Mdogo wangu aliachwa na mkewe mwaka mmoja uliopita.Katika hali isiyokuwa ya kawaida akamuandikia barua kuwa hamtaki tena na akamkabidhi barua hiyo mbele ya mtendaji.Agosti 2016 akaenda mahakamani kudai talaka.Jana hakimu katoa uamuzi huu,kuanzia leo mko huru.Wa kuoa aoe na wa kuolewa aolewe.Nendeni nyumbani na muhesabu siku 45 toka leo halafu mrudi hapa mahakamani kwa hatua ya mwisho.Ila kila mmoja wenu itabidi ajigharamikie kwa gharama hizo ndogo.Ninachoomba mnieleweshe hizo gharama ni za nini?Au ndoa ikivunjwa mahakama inatoa hati za talaka?
Kesi inapofunguliwa huwa inakuwa na gharama kwa wahusika kulipia ufunguaji wa shauri, gharama za mawakili, nauli za kuhudhuria mahakamani nk, hivyo mtu katika maombi yake huwa anaomba iwapo akishinda hizi gharama alizotumia zilipwe na yule alieshindwa...
Sasa kwenye kesi za ndoa huwa mahakama haitoi gharama kwa upande wowote ndio maana hakimu alisema hao watu kila mmoja ajigharamie.
 
Sajo,nashukuru kwa ufafanuzi!
Lakini hii kesi imefunguliwa na shemeji yangu akidai talaka sasa hizo gharama zinaingiaje?Yeye si ndiyo anatakiwa alipie?
 
Kila kilichofanyika kina thamani, yaani muda alioutumia kaka yako na shemeji yako pia una thamani maana muda huo wangeweza kuutumia katika shughuli za kuzalisha mali, kufika mahakamani lazima kuna ghrama ziliingiwa (nauli, mafuta ya gari kama ni binafsi nk), kama kulikua na mawakili pia lazima walilipwa ili wafanye kazi yao..sasa kwa ujumla hivi vyote ndio vinavyoleta kitu kinachoitwa gharama ambazo mahakama ikiona inafaa huwa zinatolewa kwa mshindi wa kesi kuwa itabidi alipwe gharama zote alizoingia...
Hivyo hizo gharama unazouliza zimetokea wapi, jibu ni kuwa zimetoka katika hivyo vitu nilivyoviainisha
 
Asante sana,sajo!
Sasa,kwa uzoefu wako na kwa kuwa hakukuwa na wakili maana ni mahakama ya mwanzo,gharama inaweza kuwa shilingi ngapi?
 
Kwa melezo uliyotoa ni kuwa mahakama haikutoa gharama kwa mtu yeyote ndio maana ikasema kila mtu atajigharamikia ambapo tafsiri yake ni kuwa hakutakua na mtu kudai alipwe gharama..kwa maana rahisi ni kuwa gharama zilizotumika wakati wa kesi hazitaombwa kufidiwa kwa mtu yeyote katika kesi hiyo..ninaamini kesi hii ilikuwa mahakama ya mwanzo.
kwani kaka yako amedaiwa gharama za kesi na huyo shemeji yako?
 
Hapana shemeji hakudai gharama yoyote!
Lakini mbona hakimu kasema wahesabu siku 45 toka alipotoa uamuzi halafu warudi tena?Inamaana wanarudi kufanya nini tena na wakati kishawaambia waende na mwenye kuoa aoe na wa kuolewa aolewe?
 
inawzekana siku 45 zilizotajwa hapo ni za kukata rufaa kama mtu hajaridhika na hukumu iliyotolewa na pia walipoambiwa warudi baada ya siku 45 labda ni kwa ajili ya kuja kusikiliza shauri la kugawana mali.. hujafafanua vyema hukumu ilisema nini, ila kimsingi mamombi ya talaka na mgawanyo wa mali zilizochumwa pamoja ni vitu viwili tofauti ambavyo vinaweza kuombwa katika shauri moja au vinaweza kuombwa tofauti tofauti, lakini vyovyote vile itakavyokuwa cha kwanza itakuwa ni mahakama kusikiliza shauri la talaka na kulitolea uamuzi. Kama mahakama itaruhusu talaka itoke basi kitakachofuata itakua ni kusikiliza shauri la mgawanyo wa mali ya pamoja, kwa hiyo inawezekana hizo siku 45 zilizotolewa ni kwa ajili ya kuangalia kama kuna rufaa kuhusu ishu ya talaka na baada ya hapo kama kutakua hakuna basi wataenda kujadili kuhusu mgawanyo wa mali.
isome vizuri hukumu ujue shemeji yako aliomba nini mbele ya mahakama na hukumu iliyotolewa ilieleza nini utaweza kuona kama haya niliyoyaeleza yapo humo.
 
Yeye hakimu aliwaambia kuwa kulingana na ushahidi wenu mliotoa ni wazi ndoa yenu iliishavunjika muda mrefu kwa hiyo mikia gharama zote!
Sasa kuhusu nakala ya hukumu nakala ya hukumu naweza kuipataje?Iko katika lugha gani?
 
mwambie kaka yako aandike barua kwenye mahakama iliyotoa uamuzi akiomba hiyo nakala ya hukumu, kama ni mahakama ya mwanzo itakua imeandikwa kiswahili, lakini hata ikiwa ya kiingereza unaweza omba mtu anaejua lugha ya kisheria akutafsirie ingawa mahakimu wengi siku hizi wanaandika katika kiingereza chepesi kinachoweza kueleweka na kila anaefahamu kiingereza.
 
Nashukuru sajo,hukumu imetolewa mahakama ya mwanzo ujiji!
Samahani naomba muundo wa hiyo barua ili niiandike haraka kuomba hiyo nakala ya hukumu.
 
hii ni barua ya kawaida tu ya kikazi, haina muundo wowote (sio document ya kisheria), ila ni muhimu anayeomba awe ni party wa kesi iliyoisha 9kaka yako au shemeji yako) ndio maana nikasema kaka yako ndie aandike barua hiyo..unataja namba ya shauri na tarehe uamuzi ulipotoka na sababu ya kuomba nakala hiyo (labda kwa rufaa au kwa mambo yako tu mengine), utapata nakala yako hiyo.
 
Asante ndugu,ngja nifanye hivyo nitakupa mrejesho.
 
Back
Top Bottom