Mbunge Wakimataifa
Member
- Jan 3, 2024
- 26
- 25
Mfumo wa demokrasia hapa nchini ulianzishwa rasmi mwaka 1992 chini ya Rais Mwinyi akiwa ndiye mwenyekiti wa chama mapinduzi CCM, na ndio kilikuwa chama pekee cha siasa kabla ya hapo kutokana na mfumo wa siasa wa wakati huo.
Najua suala la maamuzi ya kuruhusu mfumo wa mabadiliko ya kisiasa kutoka ujamaa hadi demokrasia haukufanywa na Mwinyi pekee kama Rais bali ni maamuzi ya chama kizima cha CCM ambacho kwa wakati ule kilikuwa ndio serikali yenyewe ukiondoa suala la chama. Najua waliwaza mengi na kujiridhisha kuwa ni sahihi nchi kubadili mfumo wake wa kisiasa huku CCM ikijua wazi inaruhisu wapinzani dhidi yake,hilo lilikuwa ni jambo jema sana kwa nchi kupata watu wenye mitazamo tofauti ili kupata mwenye mawazo bora kwa wakati husika kuongoza nchi pamoja na chama chake.
Sasa swali langu ni hili; kama ccm ilijua wasi kwamba inaruhusu upinzani dhidi yake kama chama tawala na ikaruhusu, sasa kwanini leo inatumia nguvu nyingi kukandamiza upinzani tena bila hata sababu? Au ilitegemea licha ya kuruhusu upinzani ya kwamba wasingetokea watu wa kuwapinga kihija na mitazamo? Au walikurupuka bila kujua athari zake kwa upande wao? Kama walijua ni kwanini sasa watu wenye mawazo tofauti na wao wanatendewa mambo mabaya ili hali wako sahihi kufanya hivyo na hawajavunja sheria? Leo tunasikia habari za watu wengi kutekwa na ukifiatilia wengi wao ni watu wa vyama vya upinzani haijawahi kutokea katekwa mtu wa CCM. Kumeshuhudiwa mara nyingi shughuli za vyama vya upinzani zikizuiwa na vyombo vya dola na shughuli hizo ziko kihalali na hawavunji sheria yoyote, mambo kama hayo hawajawahi fanyiwa watu wa CCM, je hii ni halali?
Mawazo yangu; kama CCM inaona iliruhusu mfumo wa demokrasia hapa nchini kimakosa basi ni vizuri wakae tena chini waamue upya kuufuta mfumo huo kama hauwafai kulikoni kuwanyanyasa watu ambao wanafanya shughuli zao kihalali. Ikifuta demokrasia sisi tusio kuwa na vyama ikitokea mtu anaikosoa serikali na akakamatwa tutajua wazi kavunja sheria kwasababu sheria za nchi haziruhusu mtu kuikosoa serikali kwa namna yoyote ile na tutajua ni stahili yake. Na kama watu watajitolea kudai haki zao kwa nguvu punde serikali inakuwa haiwajibiki vema kwa wananchi basi iwe wazi wanaamua kwa kujitoa muhanga kwa maana sheria hairuhusu watu kufanya hivyo, hapo inakuwa inaeleweka wazi ni kufa au kupona kuliko ilivyo sasa kwamba mtu anaruhusiwa halafu anaviziwa.
Mwenye uelewa sababu za CCM kuruhusu mfumo wa vyama vingi huku yenyewe inauchukia mfumo aniambie waliruhusu ili iweje?