Mwenye mwangaza wa kutumia boom

Joined
Sep 25, 2014
Posts
30
Reaction score
1
Jamani naomben mnisaidie manake mimi sijui kutumia vizuri pesa,, naombeni mnisaidie kwa aliye na wazo jinsi ya kupangilia boom anisaidie,, nitawaelewa wote bila kujali matumizi yangu binafsi.Nimefanya hivi kwa imani kuwa mkopo utatoka siku si nyingi, wadau tusaidiane, naogopa kukopa
 


Mkuu ushajihakikishia kuwa utapata?
 

Ni bora ungetaja chuo ulichochaguliwa, ili wadau tujue tunakushauri vipi. Ushauri unategemea na mazingira uliko.
 
Boom mwanaharamu halkai sana lnakata. Usjsunbue tumia uwezavyo
 
duu aisee hii wala haina ushauri ni jinsi wewe mwenyewe utakavosoma mazingira, mimi nilikuwa napata bum 100% ila nilikuwa namaliza ndani ya two weeks, lakini met wangu alikuwa anapata 60% na alikuwa anasomesha mpaka mdogo wake kwa bum lake.
 

7500/= kwa siku

Bajeti yako ni

Breakfast 1000
Lunch 1500
Drinks uhai maji 1200
Dinner 1500
Vocha 1000

Jumla kuu 6200/= per day

Zinazobaki weka akiba
 
ishi na kula kama ulivyokuw unakula sekondari...pia voom sio la kununulia smartphone...la kugongea na la kuzurulia mjin wakuone watotoz kitaa...jua boom si msaada..balini part ya mshahara wako wa baadae utakao katwa.....usivuke kima kilichowekwa cha elf 7...ACHANA NA MIKUMBO NA POMBE...TOA ZAKA..MUNGU AWE MLINZI WA hela zako..na akuongoz kutumia kimalengo na kufanya yalio mema..usije juta...maana weng hutumia boom kuhongea..automatically huisha na waliohongwa hupita pemben....likija lingine kutokn na habit uliojiwekea...lazna litaishs tena
tabia ni kma ngozi
 
Kwa sababu hela ya kula ni 7500tsh uwe unachukua hyo kila siku unatumia zinazobaki unaweka kwenye kibubu,kesho tena unachukua kiasi hchohcho then kinachobak unahifadh
 
Itategemea malengo yako - yaani unataka kubana au kujiachia. Hayo yatakupa muelekeo wa matumizi yako.
 

Jibane uwezavyo, kama utakua UDSM nenda pale caf 1 weka bili ya kula hata miezi miwili
Kingine usinunue maji ya kunywa cha msingi tafuta jagi la kuchemshia maji kwa tuliopita pale tunaita ku-google maji,
Usipende matumizi yasiyo na maana kama kula kula, kunywa soda za pale k/koo kila unapojiskia eti umetoka kusoma usiku unaenda kununua soda/juice na keki wakati ulikua umeshakula chakula cha jioni.
Epuka kula vitu vya bei kubwa kwa kufuata mkumbo kisa umeona mwenzio anakunywa supu na chapata pale caf 2 nawewe unajipima ubavu? Thubutuuu!!!
Punguza outing zako sio kila muda uko mwenge, mara mjini, kingine sehemu kama ubungo ikiwa hauna haraka ni vizuri uende kwa miguu maana utafanya mazoezi na utaepusha gharama.
Control matumizi ya vocha, tumia university promotion ndugu vinginevyo utakula 001 au 101et al.
Chunga sana style yako ya kula sio unakula wali juice na matunda pembeni.
Akili za kuambiwa changanya na za kwako.
Hiyo ni experience yangu wakati nikipiga miaka yangu hapo JK Nyerere Mlimani Campus.
 

hahaha safi sana unanikumbusha mbali sana enzi za shato pori,kudownload maji, na pasi ndefu na jioni rb.. Ila boom likitoka watu wanajisahau tena wanajichia pande za abc. Namshauri kama yupo mabibo aweke bili kwa mama kifusi,
 
-Chai tumia 600(yaani chai rangi 200,maandazi 2 @200)
-Lunch 1200(Ugali au wali maharage,mchuzi na mboga za majani)
-Dinner 1200 as lunch
-maji 2 @500=1000
-vocha 500
-hutokuwa na gharama ya nauli kwani pale NIT hostel za kupanga zipo karibu sana na chuo yaani mabibo kwa hiyo utatembea tu.

Jumla 4500
7500-4500=3000

Ukiweka 3000 kila siku kwa mwezi utakuwa na sh.90000/=
Hiyo elfu90 ipeleke bank kila mwezi ufungue fixed account ambayo kwa mwaka
Utaweka 720,000/=

Kwa miaka mitatu utaweka 2,160,000/=

Kwa hiyo ukijumlisha riba ya fixed account itafika kwenye million tatu na zaidi.

Sasa baada ya kumaliza chuo wewe unaingia kwenye biashara yamtaji Wa milion tatu au unaenda kwenye kilimo kwa miaka miwili tu hutaitaji kuajiliwa tena.

Usishangae inawezekana sema vijana tunapenda starehe sana hatujui kuwa nmafanikio yanaanza na shida, sisi tunataka tuanze na raha ndipo tupate mafanikio, nikitu ambacho hakiwezekani.

Ndio maana mchaga anaanza na kimeza cha pipi, sigara na biskuti lkn baadae unamkuta ana duka kubwa sana.

Thanks my friend try it.
 

acha uwongo wewe inamaana matumizi ni kula tu na usafiri na mwaka wa chuo ni siku kama 240 tu yaani kwa mwaka upewe 900 wewe huifazi 720 kichwa yako inafanya kazi vizuri kweli?
 
acha uwongo wewe inamaana matumizi ni kula tu na usafiri na mwaka wa chuo ni siku kama 240 tu yaani kwa mwaka upewe 900 wewe huifazi 720 kichwa yako inafanya kazi vizuri kweli?

Ndugu yangu TIASSA Twende taratibu,
kama ni siku 240 @7500=1,800,000 hii ni ya chakula kwa mwaka mzima unayopewa na bodi.

chukua 1,800,000-720,000=1,080,000/=

Sasa hii 1,080,000/= ndiyo niliyosema unaibana kwa ajili ya chakula kama nilivyochanganua hapo juu.

Kuhusu usafiri amesema yupo chuo cha NIT ndiyo maana nimetoa nauli kwani pale ni karibu na hostel au vyumba vya kupanga na mkashare chumba na nimeeleza kwenye maelezo yangu ya hapo juu.Labda safari za mjini kuzunguka kulijua jiji la DAR, ndugu yangu TIASSA unajibana tu unaachana nazo au unapiga pass ndefu ya msosi siku mojamoja ili upate pesa ya kufanyia safari zako, lakini pesa uliyo ipanga kuipeleka bank huigusi.

Inawezekana ni ugumu wa kudhubutu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…