Baba Genovivah
JF-Expert Member
- Sep 1, 2013
- 756
- 249
Wenzako wanatumia boom kumalizia tution fee cjui umenisoma????
Jamani naomben mnisaidie manake mimi sijui kutumia vizuri pesa,, naombeni mnisaidie kwa aliye na wazo jinsi ya kupangilia boom anisaidie,, nitawaelewa wote bila kujali matumizi yangu binafsi.Nimefanya hivi kwa imani kuwa mkopo utatoka siku si nyingi, wadau tusaidiane, naogopa kukopa
duu aisee hii wala haina ushauri ni jinsi wewe mwenyewe utakavosoma mazingira, mimi nilikuwa napata bum 100% ila nilikuwa namaliza ndani ya two weeks, lakini met wangu alikuwa anapata 60% na alikuwa anasomesha mpaka mdogo wake kwa bum lake.
Ndugu yangu TIASSA Twende taratibu,
kama ni siku 240 @7500=1,800,000 hii ni ya chakula kwa mwaka mzima unayopewa na bodi.
chukua 1,800,000-720,000=1,080,000/=
Sasa hii 1,080,000/= ndiyo niliyosema unaibana kwa ajili ya chakula kama nilivyochanganua hapo juu.
Kuhusu usafiri amesema yupo chuo cha NIT ndiyo maana nimetoa nauli kwani pale ni karibu na hostel au vyumba vya kupanga na mkashare chumba na nimeeleza kwenye maelezo yangu ya hapo juu.Labda safari za mjini kuzunguka kulijua jiji la DAR, ndugu yangu TIASSA unajibana tu unaachana nazo au unapiga pass ndefu ya msosi siku mojamoja ili upate pesa ya kufanyia safari zako, lakini pesa uliyo ipanga kuipeleka bank huigusi.
Inawezekana ni ugumu wa kudhubutu tu.
Ni kweli unachosema, lakin watoto wa wakulima wengi huwa wanagawa hela ya bum kuongezea katika tuition fee. thats why nikawa namshangaa jamaa anagawa bum na kuongezea ada huku anasomesha mdogo mdogo wake.Nadhani umechanganya madesa hapa kati ya bum na pesa ya tuition fee..
Boom huwa ni flat, yani linapewa sawa kwa wanafunzi wote watakaofanikiwa kupata.. 7500/= per day..
I stand to be corrected..
7500/= kwa siku
Bajeti yako ni
Breakfast 1000
Lunch 1500
Drinks uhai maji 1200
Dinner 1500
Vocha 1000
Jumla kuu 6200/= per day
Zinazobaki weka akiba
Kuna jambo la madesa nalo linamaliza pesa sana hapo UDSM, mkakati mzuri kwa uzoefu wangu pale CoNAS ni vyema umiliki laptop ndogo tu, then jibane ununue HP printer inauzwa around 100,000TZS hiyo utatumia muda mrefu na ikiwezekana utaifanyia business kama utakua na muda. Ikiwa utapenda idea ya kua na printer utanitafuta nikuelekeze jinsi ya kuendesha hiyo business bila hasara
-Chai tumia 600(yaani chai rangi 200,maandazi 2 @200)
-Lunch 1200(Ugali au wali maharage,mchuzi na mboga za majani)
-Dinner 1200 as lunch
-maji 2 @500=1000
-vocha 500
-hutokuwa na gharama ya nauli kwani pale NIT hostel za kupanga zipo karibu sana na chuo yaani mabibo kwa hiyo utatembea tu.
Jumla 4500
7500-4500=3000
Ukiweka 3000 kila siku kwa mwezi utakuwa na sh.90000/=
Hiyo elfu90 ipeleke bank kila mwezi ufungue fixed account ambayo kwa mwaka
Utaweka 720,000/=
Kwa miaka mitatu utaweka 2,160,000/=
Kwa hiyo ukijumlisha riba ya fixed account itafika kwenye million tatu na zaidi.
Sasa baada ya kumaliza chuo wewe unaingia kwenye biashara yamtaji Wa milion tatu au unaenda kwenye kilimo kwa miaka miwili tu hutaitaji kuajiliwa tena.
Usishangae inawezekana sema vijana tunapenda starehe sana hatujui kuwa nmafanikio yanaanza na shida, sisi tunataka tuanze na raha ndipo tupate mafanikio, nikitu ambacho hakiwezekani.
Ndio maana mchaga anaanza na kimeza cha pipi, sigara na biskuti lkn baadae unamkuta ana duka kubwa sana.
Thanks my friend try it.
hahaaaa..mama mbavu zanguu..hahaaUkipata boom la semister ya kwanza kula lote kwa siku mbili: alafu angalia utaishije semester hiyo. Ndivo inavotakiwa uishi semister zinazofuata ''we learn through experience''