Mwenye mwangaza wa kutumia boom

Mwenye mwangaza wa kutumia boom

Wenzako wanatumia boom kumalizia tution fee cjui umenisoma????

tuchukulie anategemea ndugu wamsaidie hiyo ada iliyobaki.

Kwani hata hao wanao lipwa asilimia miamoja lkn bado mwisho wa siku wanalalamika nyumbani na kwa ndugu baki wawatumie fedha ya matumizi, wanadai imeisha, hususani pale kipindi kigumu cha boom kukalibia kutoka.

Siku hizi wazazi hata kama mwanafunzi anapata mkopo wanajua kuwa lazima atapewa kiasi kidogo kwa hiyo wanajiandaa kwa kitakachohitajika.
 
Jamani naomben mnisaidie manake mimi sijui kutumia vizuri pesa,, naombeni mnisaidie kwa aliye na wazo jinsi ya kupangilia boom anisaidie,, nitawaelewa wote bila kujali matumizi yangu binafsi.Nimefanya hivi kwa imani kuwa mkopo utatoka siku si nyingi, wadau tusaidiane, naogopa kukopa

Lipa bili ya chakula ya semista nzima, nunua madesa yote muhimu. Inayobaki ni akiba yako, unaweza kuwa unatumia kulingana na mahitaji. Cha msingi hakikisha unakuwa na uhakika wa chakula. Kama sio mnywaji na sio mhongaji, uta survive but kama ni mnywaji na mhongaji,itakuwa ngumu sana kwako. Kutunza hela ni changamoto kubwa sana hususani kwa wanaume.
 
Kuna jambo la madesa nalo linamaliza pesa sana hapo UDSM, mkakati mzuri kwa uzoefu wangu pale CoNAS ni vyema umiliki laptop ndogo tu, then jibane ununue HP printer inauzwa around 100,000TZS hiyo utatumia muda mrefu na ikiwezekana utaifanyia business kama utakua na muda. Ikiwa utapenda idea ya kua na printer utanitafuta nikuelekeze jinsi ya kuendesha hiyo business bila hasara
 
duu aisee hii wala haina ushauri ni jinsi wewe mwenyewe utakavosoma mazingira, mimi nilikuwa napata bum 100% ila nilikuwa namaliza ndani ya two weeks, lakini met wangu alikuwa anapata 60% na alikuwa anasomesha mpaka mdogo wake kwa bum lake.

Nadhani umechanganya madesa hapa kati ya bum na pesa ya tuition fee..

Boom huwa ni flat, yani linapewa sawa kwa wanafunzi wote watakaofanikiwa kupata.. 7500/= per day..

I stand to be corrected..
 
Ukipata boom,achana na kampani za pombe ata kama unatumia pombe,achana na malavidavi ya kuleteana zawadi na trip za viwanja,acha kujifanya mambo safi kila saa cafeteria,maji ya kilimanjaro kama bonite ni ya mdogo wako... wewe la sivyo utakula piza(ukoko) na kushindia fegi mchana,wakati uo course work hazisomi!.
 
Ndugu yangu TIASSA Twende taratibu,
kama ni siku 240 @7500=1,800,000 hii ni ya chakula kwa mwaka mzima unayopewa na bodi.

chukua 1,800,000-720,000=1,080,000/=

Sasa hii 1,080,000/= ndiyo niliyosema unaibana kwa ajili ya chakula kama nilivyochanganua hapo juu.

Kuhusu usafiri amesema yupo chuo cha NIT ndiyo maana nimetoa nauli kwani pale ni karibu na hostel au vyumba vya kupanga na mkashare chumba na nimeeleza kwenye maelezo yangu ya hapo juu.Labda safari za mjini kuzunguka kulijua jiji la DAR, ndugu yangu TIASSA unajibana tu unaachana nazo au unapiga pass ndefu ya msosi siku mojamoja ili upate pesa ya kufanyia safari zako, lakini pesa uliyo ipanga kuipeleka bank huigusi.

Inawezekana ni ugumu wa kudhubutu tu.

nimekukubali,wengi huwa hawawezi,ndio maana ata kutoboa maisha huwa hawawezi,wanafikiri watakapo pata kazi mambo yatakaa sawa,wakati fedha boom kuna raia ni mshahara na wana watoto,kuna baadhi kwao wako njema ila boom wanaitafuna usiwaige utajuta
 
Utajuta ukilitumia boom kujipatia umaarufu na kuishi kama super star! Kama mdau alivyokushauri, make sure hauvuki limit uliyopangiwa kwa mwezi. Ila sio mbaya siku moja moja ukajitoa out then the next week ukala wali maharage ku cover the gap...
 
Nadhani umechanganya madesa hapa kati ya bum na pesa ya tuition fee..

Boom huwa ni flat, yani linapewa sawa kwa wanafunzi wote watakaofanikiwa kupata.. 7500/= per day..

I stand to be corrected..
Ni kweli unachosema, lakin watoto wa wakulima wengi huwa wanagawa hela ya bum kuongezea katika tuition fee. thats why nikawa namshangaa jamaa anagawa bum na kuongezea ada huku anasomesha mdogo mdogo wake.
 
7500/= kwa siku

Bajeti yako ni

Breakfast 1000
Lunch 1500
Drinks uhai maji 1200
Dinner 1500
Vocha 1000

Jumla kuu 6200/= per day

Zinazobaki weka akiba

hajanunua pamba hapo,yote 9,10 madesaaa kununua na copy na kama ni wakuonga ndo kaisha
 
wao wenyewe wakupao bumu washakwambia matumizi yake ukifuata pia inasaidia maana kwa siku ni shingapi? ni siku ngapi? na ni kwanini umepewa hicho kiasi,, japo kiuhalisia lazima utumie chini ya kiasi unachopewa kwa siku maana kuna matumizi mengine yanakuja automatic kutakana na masha ya binadamu, ili yaweze kubalance lazima ubane matumizi.
 
Kuna jambo la madesa nalo linamaliza pesa sana hapo UDSM, mkakati mzuri kwa uzoefu wangu pale CoNAS ni vyema umiliki laptop ndogo tu, then jibane ununue HP printer inauzwa around 100,000TZS hiyo utatumia muda mrefu na ikiwezekana utaifanyia business kama utakua na muda. Ikiwa utapenda idea ya kua na printer utanitafuta nikuelekeze jinsi ya kuendesha hiyo business bila hasara

mkuu naomba unipe namba yako ya simu tuuongee zaidi
 
-Chai tumia 600(yaani chai rangi 200,maandazi 2 @200)
-Lunch 1200(Ugali au wali maharage,mchuzi na mboga za majani)
-Dinner 1200 as lunch
-maji 2 @500=1000
-vocha 500
-hutokuwa na gharama ya nauli kwani pale NIT hostel za kupanga zipo karibu sana na chuo yaani mabibo kwa hiyo utatembea tu.

Jumla 4500
7500-4500=3000

Ukiweka 3000 kila siku kwa mwezi utakuwa na sh.90000/=
Hiyo elfu90 ipeleke bank kila mwezi ufungue fixed account ambayo kwa mwaka
Utaweka 720,000/=

Kwa miaka mitatu utaweka 2,160,000/=

Kwa hiyo ukijumlisha riba ya fixed account itafika kwenye million tatu na zaidi.

Sasa baada ya kumaliza chuo wewe unaingia kwenye biashara yamtaji Wa milion tatu au unaenda kwenye kilimo kwa miaka miwili tu hutaitaji kuajiliwa tena.

Usishangae inawezekana sema vijana tunapenda starehe sana hatujui kuwa nmafanikio yanaanza na shida, sisi tunataka tuanze na raha ndipo tupate mafanikio, nikitu ambacho hakiwezekani.

Ndio maana mchaga anaanza na kimeza cha pipi, sigara na biskuti lkn baadae unamkuta ana duka kubwa sana.

Thanks my friend try it.

Ebana eeeh… Bonge la akili. Nimeielewa hii. Uko vizuri mkuu. Much respect.
 
hakuna mtu wa kukuelekeza wewe jinsi ya kutumia BOOM...unatakiwa kutumia boom kwa matumizi yako yote muhimu kama kwa bahati mbaya likielekea kuisha piga pasi ndefu au kopa....utajifunza tu!!
 
Back
Top Bottom