Jibane uwezavyo, kama utakua UDSM nenda pale caf 1 weka bili ya kula hata miezi miwili
Kingine usinunue maji ya kunywa cha msingi tafuta jagi la kuchemshia maji kwa tuliopita pale tunaita ku-google maji,
Usipende matumizi yasiyo na maana kama kula kula, kunywa soda za pale k/koo kila unapojiskia eti umetoka kusoma usiku unaenda kununua soda/juice na keki wakati ulikua umeshakula chakula cha jioni.
Epuka kula vitu vya bei kubwa kwa kufuata mkumbo kisa umeona mwenzio anakunywa supu na chapata pale caf 2 nawewe unajipima ubavu? Thubutuuu!!!
Punguza outing zako sio kila muda uko mwenge, mara mjini, kingine sehemu kama ubungo ikiwa hauna haraka ni vizuri uende kwa miguu maana utafanya mazoezi na utaepusha gharama.
Control matumizi ya vocha, tumia university promotion ndugu vinginevyo utakula 001 au 101et al.
Chunga sana style yako ya kula sio unakula wali juice na matunda pembeni.
Akili za kuambiwa changanya na za kwako.
Hiyo ni experience yangu wakati nikipiga miaka yangu hapo JK Nyerere Mlimani Campus.