Mwenye ndoa salama ajitokeze hapa

Mwenye ndoa salama ajitokeze hapa

Nimekuwa nikisikiliza washauri wa masuala ya ndoa Jinsi wanavyoelezea changamoto za na namna ya kukabiliana nazo yaani kama wao wapo sahihi kwenye ndoa zao, badala yake hao motivation speaker ndio vinara wa kuchepuka katika ndoa zao.

Ndio maana nasema kama una ndoa salama jitokeze.
Usalama kwa namna ipi ?

Uwazi ama uaminifu ?

au uwazi na uaminifu ?..

NB: Tusi haliwi tusi mpaka alietukanwa aseme ni tusi.
 
Nimekuwa nikisikiliza washauri wa masuala ya ndoa Jinsi wanavyoelezea changamoto za na namna ya kukabiliana nazo yaani kama wao wapo sahihi kwenye ndoa zao, badala yake hao motivation speaker ndio vinara wa kuchepuka katika ndoa zao.

Ndio maana nasema kama una ndoa salama jitokeze.
Ndoa ni mkataba wa mahusiano baina ya mwanamme na mwanamke ambao ndiyo hupelekea kutengeneza familia. Ili uingie kwenye mkataba huo wa ndoa ni lazima ujue haki yako juu ya mwenza wako, kwani kuna sababu nyingi zinatokea za kuvunjika kwa mkataba huo wa ndoa na chanzo ni watu kutojua nini haki yake kwa mwenza wake na nini haki ya mwenza wake kwake. Kama binadamu tulivyo hakuna aliyekamilika tofauti za hapa na pale zipo, lakini tusijaalie hizo tofauti ndiyo chanzo cha kuvunja mikataba yetu ya ndoa. Ustahamilivu kwa baadhi yetu haupo, hekima na heshima nazo hazipo ndiyo maana leo tupo kwenye mjadala mfano wa huu.
Nashukuru nina mwaka wa 24 sijapatapo kuwa na tatizo katika ndoa, si kwa uhodari wangu bali ni taufiki ya Mungu na mwenza wangu kuwa ameelewa darasa la ndoa na ameridhika na kutosheka kwa kile anachokipata katika maisha yake.
 
Ndoa yangu ni salama, occasionally hua tunazozana, but that normal part of human being.

All in all we are good and love each other insanely.
Nani kakuambia kuzozona ni sehemu salama ya maisha ya binaadamu, some time ni ku-surender na ku-ignore mambo mengine ila sio kua salama, Ndoa yako ina mda gani mkuu?
 
Ndoa ni mkataba wa mahusiano baina ya mwanamme na mwanamke ambao ndiyo hupelekea kutengeneza familia. Ili uingie kwenye mkataba huo wa ndoa ni lazima ujue haki yako juu ya mwenza wako, kwani kuna sababu nyingi zinatokea za kuvunjika kwa mkataba huo wa ndoa na chanzo ni watu kutojua nini haki yake kwa mwenza wake na nini haki ya mwenza wake kwake. Kama binadamu tulivyo hakuna aliyekamilika tofauti za hapa na pale zipo, lakini tusijaalie hizo tofauti ndiyo chanzo cha kuvunja mikataba yetu ya ndoa. Ustahamilivu kwa baadhi yetu haupo, hekima na heshima nazo hazipo ndiyo maana leo tupo kwenye mjadala mfano wa huu.
Nashukuru nina mwaka wa 24 sijapatapo kuwa na tatizo katika ndoa, si kwa uhodari wangu bali ni taufiki ya Mungu na mwenza wangu kuwa ameelewa darasa la ndoa na ameridhika na kutosheka kwa kile anachokipata katika maisha yake.
Mkuu omba sana mungu muendelee hivo unaweza kua una timing bomb itapasuka mda wowote miaka 24 sio haba ila bado maisha na binaadamu hubadilika ghafra.
 
Nilichojifunza ni kwamba ndoa wala hazifanani. Kila ndoa Ina staili ya utofauti ambao unaweza usifanane na ndoa nyingine. Kunakuwa na vitu vichache sana vya kufanana.

Kuna wengine hata wamfumanie mwenza wake utakuta wanaweza vumilia na kusamehe, lakini kuna wengine wakikuta tu umemtumia mtu mwingine meseji ya ya kimahaba unapata kibuti hapohapo, hakuna No uvumilivu.

Wengine wanaishi kwa kupigana kilasiku. wegine hata ile kuongozana tu kutembea pamoja huwezi kuwaona ili mladi kila ndoa ina staili yake na kunakuwa na tabia za utofauti
 
Back
Top Bottom