Mwenye Nyumba ameleta mganga wa kienyeji anatulazimisha tulambe unga anahisi kuna mchawi kwenye nyumba yake

Hama haraka we mwambie nyoka halambi unga, ova
 
Mleta mada lmwenye nyumba ndie mchawi anataka kuwageuza chuma ulete

Mkilamba tu mtashangaa mnapata pesa halafu zinayeyuka hewani

Mwanga mkubwa huyo mwambieni kodi yenu ikiisha mnahama aunawarudishie chenu mkatafute nyumba ingine au awape notisi ya kuhama

Mnaishi na lichawi hilo lenye nyumba chawi lisilokuwa na haya linataka kuloga mchana kweupe wapangaji
 
huyu mzee before alikuwa fresh tu sasa alipigwa chini kazini kwao huko baada ya hapo kila mtu anamuona mchawi
Sasa masuala ya yeye kazini na wapangaji kulamba unga Inahusu nn??
Kwan huyo mganga ni tapeliiii [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Angalia vizuri mkataba wako, inaweza kuwa kuna hicho kipengele.

Kama hakipo fanya maamuzi
Sahihi aanze kwenye mkataba ambane hapo hapo wala hahitaji kusema sijui imani yangu hairuhusu vitu vya kishirikina yeye amuulize kwenye mkataba kuna kipengele.cha kulamba unga ulioletwa na mwenye nyumba?
 
Nyumba akiwa mwenye nyumba mnaishi pamoja ni shida.Nakummbuka kuna nyumba nilihama kwa ujinga kama huu wa ushirikina ulio kubuhu.
Nyumba za kupanga kienyeji mtihani. Panga kwenye nyumba ambazo mwenye nazo kaamua kuipanga kibiashara kama apartments vile.. ila hizi yeye anaishi na wewe unaishi mtatibuana tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…