Mwenye Nyumba ameleta mganga wa kienyeji anatulazimisha tulambe unga anahisi kuna mchawi kwenye nyumba yake

Mwenye nyumba ana tabia za kuwafanya wapangaji wake chuma ulete kimazingira na inavyoonekana kuna mpangaji aliyeingia hapo na ana nguvu kinzani na huyo mzee mwenye nyumba. Kuna watu wanapangisha nyumba moja tokea umri wa ujana hadi uzee, na si kwamba hiyo nyumba ina mazingira au huduma bora.
 
Akurudishie pesa iliyobaki usepe,atakulambishaje vitu huvijui!?
 
SERIKALI INAZUIA MATUMIZI YA UNGA MGANGA ANAWALAMBISHA WATU UNGA😂😂😂
 
Nenda ofisi za ustawi wa jamii,hizo ndo kazi zao .Kwanza lazima awe na kibali cha kufanya kazi ya uganga,pili lazima apitie serikali ya mtaa husika.Je yote yamegfanyika?Kama hayajafanyika karipoti ustawi wa jamii watakaupa msaada.
Mwisho jipange kuhama
 
Toa taarifa kwa mwenyekiti wa mtaa halafu polisi. Hawezi kukufukuza kirahisi.
 
Dah! Balaa hii
 
Kama unatoka, si atakurudishia kodi? Utahangaika kupata sehemu nyingine, ila hutashiriki uchawi wake. Haya mambo yafaa yapigwe marufuku Tz.
 
Umesoma nilicho jb lkn? Wapi nimesema alambe unga!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…