NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,925
Baada ya muda mrefu kuishi kibahili bahili licha ya kuajiriwa taasisi yenye mshahara na posho si haba, Rafiki yangu kaweza kukamilisha nyumba yake.
Hapo majuzi alienda kumuaga mwenye nyumba kwamba nae amejenga na ni muda sasa umefika nae aende kuishi kwenye nyumba yake, Lengo lilikuwa ni kuaga kwa amani, mwenye nyumba alimpokea tu vizuri, akawa anampongeza na hata alipoomba aoneshwe picha za nyumba alimpongeza sana rafiki kwa kujenga nyumba nzuri kuzidi hata pale alipopanga, wakaagana vizuri tu na kumtakia kila la kheri.
Mwenye nyumba akamwambia siku ya kuondoka ikifika amwambie ili aje achukue funguo.
Sasa rafiki alivofika tu nyumbani, mwenye nyumba akamtumia sms kuwa anataka nyumba aipake rangi yote ndio ahame, hio nyumba amekaa miaka 6 na mwenye nyumba ajawah kupaka rangi, alipaka tu wakati anahamia, mkataba ulisema haruhusiwi kufanya chochote bila idhini ya mwenye nyumba hata kama ni kitasa.