SI KWELI Mwenye Seli Mundu (Sickle Cell Disease) hawezi kuishi kwa zaidi ya miaka 30

SI KWELI Mwenye Seli Mundu (Sickle Cell Disease) hawezi kuishi kwa zaidi ya miaka 30

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Hii imekaa vipi kitaalam, Mwenye Selimundu (Sickle Cell Disease) hawezi kuishi kwa zaidi ya miaka 30?

IMG_6741.jpeg
 
Tunachokijua
Sickle Cell Disease (SCD) ama Selimundu ni ugonjwa wa kurithi unao athiri chembe nyekundu za damu.

Kwa muundo wake, chembe nyekundu za damu huundwa na aina moja ya protini inayoitwa hemoglobin.

Protini hii hufanya kazi ya hubeba hewa na kuisafirisha kwenda sehemu mbalimbali za mwili.

Kwa watu wenye afya nzuri, hemoglobin huwa ni laini, ina umbo la duara na huwa inaweza kubadilika umbo lake kirahisi. Tabia hizi ndizo huruhusu iweze kupenya kirahisi na kusafiri kila sehemu ya mwili pasipo uwepo wa pingamizi lolote.

Kwa watu wenye ugonjwa huu hali haipo hivyo. Hemoglobin huwa ngumu, ina umbo la mwezi mchanga au herufi C na huwa haibadiliki kirahisi.

Takwimu
Takriban watu Milioni 20 duniani wanakabiliwa na changamoto hii huku Tanzania ikiwa na wastani mkubwa wa kuzaliwa kwa watoto takriban 11,000 kila mwaka walio na ugonjwa huu.

Dalili za ugonjwa
SCD ama ugonjwa wa Selimundu huwa na dalili nyingi ikiwemo kusababisha udumavu wa watoto, upungufu wa mara kwa mara wa damu, umanjano, maumivu makali ya mwili, kupungua kwa uoni wa macho pamoja na kusumbuliwa na maambukizi ya mara kwa mara.

Umri wa kuishi kwa wagonjwa
JamiiForums imezungumza na wataalam wa afya pamoja na kurejea tafiti mbalimbali za afya zinazotoa maelezo ya kitabibu kuhusu ugonjwa huu na uhusiano wake na umri wa kuishi.

Katika rejea zetu, tumebaini mambo yafuatayo;
  1. Mtu mwenye ugonjwa wa Selimundu anaweza kuishi umri mrefu unaozidi miaka 30.
  2. Utafiti wa Orah S. Platt et al (Mortality In Sickle Cell Disease-Life Expectancy and Risk Factors for Early Death), watoto waliozaliwa na taarifa kamili za ugonjwa walikuwa na wastani wa kuishi wa miaka 42 kwa wanaume na miaka 48 kwa wanawake. Pia, wale wenye haemoglobin ya seli mundu aina C waliishi kwa wastani wa miaka 60 kwa wanaume na 68 kwa wanawake. Kwa ujumla wake, takriba 50% ya wagonjwa wote 3764 waliofanyiwa utafiti huu waliweza kuishi zaidi ya miongo 5.
  3. Watu hawa wanaweza kuishi maisha bora huku wakifuraha haki zao za msingi kama binadamu wengine pasipo uwepo wa changamoto kubwa za kudhoofisha afya zao.
Kwa kuwa ugonjwa huu huambatana na changamoto na maudhi mengi, wazazi wenye watoto walio na ugonjwa huu hushauriwa kuwatunza vizuri, kuwapeleka hospitalini mara kwa mara pamoja na kuhakikisha kuwa wanafuata taratibu sahihi za kimatibabu.

Aidha, inashauriwa pia kutumia maji ya kutosha kila siku, walau glasi 8 ili kupunguza ukubwa wa maudhi yake.

Baadhi ya tiba za ugonjwa huu ni kutumia dawa za Hydroxyurea, kuongezewa damu pamoja na kufanya pandikizi la uroto (uboho).
Mnatutia presha tu na hizi tafiti zenu uchwara
 
Ni kweli hapo awali ilikuwa hivyo..tena hata 30 yrs hufiki lakini juhudi kubwa za Wanasayansi wetu zimewezesha na wao kuishi angalau umri uliosogea kiasi.Wameleta dawa nzuri za kuongeza damu na elimu namna ya kujikinga na magonjwa nyemelezi ambayo ndio triger kuu ya ugongwa wa seli mundu
 
Back
Top Bottom