Mwenye UKIMWI akitumia ARV hana tena uwezo wa kuambukiza wengine!

Basi kama ndo hivyo, ina maana mtu mwenye ukimwi aneyetumia ARV akijamiiana na akatumia condoms hawezi kuambukiza ukimwi kabisa?
wanasayansi wamejirisha kwa tafiti zaidi ya mbili katika maelezo haya, na mimi nasema haitakuwa rahisi kuambukiza mtu, stasema haiwezekani kwa kuwa uwezo wa kondomu ni 70% na ARV ni 96%, kwa harakaharaka haitawezekana kuambukiza mwingine
 
We jamaa ulikua wapi siku zotee!!!
 SANAA,
Endelea kutoa somo aka KUTUHASISHA

Taifa linahitaji vijana kama ww ili tusonge...
asante sana.
huwa nipo MMU kwa wingi, na karibia kila siku, na hata hii mada nimeweka kule ila imeletwa huku
 
Hapa mada itachangiwa kitaalamu na Siyo blah blah

nimeelewa,lakini najua kila jukwaa huwa lina watu wa aina zote,mfano mimi mwenyewe ni nimebobea zaidi katika mambo ya siasa lakini nipo MMU na siasa siendi,kwa hiyo naamini hata kule madakitari wapo.
 

hapo hapo mkuu na vipi kama ametumia ARV kwa mda alafu akaacha kutumia(let say miezi 2) hatajatumia ARV anawekwa katika kundi gani ?
 
mkuu ungerekebisha kidogo title kwani hiyo asilimia 4 ni kubwa sana!uwezekano upo lakini ni mdogo.
Misprint ya kitabu au maandishi ya kitabu cha medicine yaweza kuleta madhara makubwa mno!
 
Kuna ndugu yangu alikuwa anatumia ARV alifiwa na mke wa kwanza,akaoa mwingine nae akafu.Mwaka jana akiwa kazini akaanguka tu ghafla kupelekwa hospital pressure ilikuwa juu sana 215.Alikufa.Swali je kwa nini wengi wanaotumia ARV wanakufa kwa pressure?

kwa kifupi sana,UKIMWI unaharibu mfumo mzima wa ulinzi katika mwili,na hili linaongeza uwezekano mkubwa kwa ngonjwa wa UKIMWI kuugua magonjwa ya moyo ambayo yapo mengi na ndio maana inakuwa rahisi kwao kufa na presha zitokanazo na moyo kuugua, pia tafiti zimeonyesha watu wanaotumia ARV wanahatari kubwa zaidi ya kuugua magonjwa ya moyo kwa kuwa kunakuwa na mkusanyiko wa mafuta mengi katika mishipa mikubwa ya moyo na hata kwenye moyo wenyewe na kusababisha mishipa kuwa miembamba na hata moyo unapata tabu kutanuka na kusinyaa,matumizi ya ARV yanaripotiwa kuongeza unene japo hilo halijathibitishwa,na mwisho bado tafiti zinaendelea kubaini kwa nini ARV zinaleta ama kusababisha matatizo ya moyo
 
mkuu ungerekebisha kidogo title kwani hiyo asilimia 4 ni kubwa sana!uwezekano upo lakini ni mdogo.
Misprint ya kitabu au maandishi ya kitabu cha medicine yaweza kuleta madhara makubwa mno!

nimekuelewa japo sina uwezo wa kubadili heading mpaka niombe kwa mods, lakini niliweka makusudi baada ya approximation ili isaidie wasomaji wengi kuifungua mada, mada najua wengi wanapuuza mada zaukimwi,kwa maneno mengine huwa hazina mvuto.
 
hapo hapo mkuu na vipi kama ametumia ARV kwa mda alafu akaacha kutumia(let say miezi 2) hatajatumia ARV anawekwa katika kundi gani ?

iko hivi,mtu akiwa anatumia ARV virusi vyote vinafubazwa,yaani vinakosa uwezo wa kuzaliana na vinakosa uwezo wa kusambaa,na hivyo vinabakia kwenye eneo moja la kujihifadhi,mtu akiacha kutumia ARV virusi vinapata mwanya wa kuanza kusambaa na kuzaliana tena,na kitu kibaya zaidi ni kwamba,wakati huu hivi virusi vinaanza kujenga usugu na dawa na vinakuwa sugu zaidi kuzuilika na dawa hiyo hiyo,na huyu akiacha tu anaongeza hatari ya kuambukiza wengine maana mgonjwa anatakiwa atumie vidonge kila siku iendayo
 
asante kwa somo mkuu,japo hujasema hizo tafiti zimefanyikia wapi,kwa watu wa aina gani nk.

tafiti ni nyingi na hazijafanywa na mtu mmoja na wakati mmoja,ila mimi huwa natumiwa matokeo ya tafiti za UKIMWI katika email yangu kila wiki kutoka maeneo mbalimbali ya dunia, na wanaonitumia ni aidsmap.com ya uingereza
 

Je huyu mtu mwenye kinga imara ya mwili na tayari ameambukizwa akipima atapatikana na maambukizi? (Pamoja na kwamba hana dalili yoyote)
 
vip mkuu mtu anawezaje kuambukiza ukimwi kwa ROMANCE(de.n..da) swal ni kwamba ukimnyonya muathirika de..n..da unaweza ukakupata ? km hatumii ARV (hii kwa wale walio nao ila hawajapima na hawajijui so hawatumii ARV)
 
Je huyu mtu mwenye kinga imara ya mwili na tayari ameambukizwa akipima atapatikana na maambukizi? (Pamoja na kwamba hana dalili yoyote)
HAYA MAELEZO NILIKUWA SIJAELEWA VIZURI SWALI,LAKINI KWA KUWA NAYO NI MAELEZO MAZURI YA KUTOA ELIMU SITAYAFUTA,ILA NILIKUWA NAMUONGELEA MTU ASIYEWEZA KUAMBUKIZWA UKIMWI KUTOKANA NA KINGA YAKE IMARA YA KUWEZA KUZUIA MAAMBUKIZI,NA UTAFITI ULIOFANYIKA NA UNAOFANYIKA KUJARIBU KUTUMIA CELL ZA WATU WASIOAMBUKIZWA UKIMWI NA KUZIPANDIKIZA KWA WENGINE ILI IWE KAMA CHANJO YA KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA UKIMWI

MAJIBU YA SWALI HUSIKA NIMEYAWEKA CHINI,SAMAHANI KWA USUMBUFU WASOMAJI


hao wenye kinga dhidi ya maambukizi ya UKIMWI kamwe hawezi kuambukizwa kabisa, na wanasayansi walitaka kufanya upandikizaji wa cell za watu hawa kwa watu wengine ili nao wajikinge na maambukizi ya ukimwi,

tatizo likawa hivi, mfano mimi upandikizaji wa stem cell,T cell za hao watu wasioweza kuambukizwa inaleta shida kwa kuwa cell zangu mimi zinaona cell nilizopandikiziwa ni adui na zinaanza kuzishambulia na kuziua, na hapo ndipo walishindwa,

lakini kwa mfano yule mtu aliyepandikiziwa seli za bon marrow wa huko marekani MISSISSIP wakati wakimtibu na kansa, iliwezekana tu kwa sababu yeye ugonjwa wake ulikuwa umeua mfumo wake wote wa ulinzi(hakuwa na immune system) na hivyo hakukuwa na kizuizi ndani ya mwili wake cha kushambulia upandikizaji wa seli kutoka kwa mtu mwigine na watu wanaopandikizwa seli za wengine asilimia 20% wanakufa baada ya muda mfupi kati ya miezi na miaka 3 na ndio maana wanasayansi wakaona hii njia haifai,

hata hivyo utafiti unao-onekana kuondoa tatizo hili la mfumo wa ulinzi wa ndani kushambulia upandikizaji wa seli toka kwa mtu mwingine ni kwamba kwa sasa wanachokifanyia nikuchukua cell za mtu huyohuyo aneugua ukimwi wanazitoa na kuzifanyia mabadiliko ya kuhimili na kuzuia maambukizi,wakishazipandikiza kwa mtu yuleyule hazishambuliwi na mfumo wa ndani wa ulinzi kwa kuwa seli hizo zinafanana na za ndani japo kidogo zimebadilishwa,

lakini wakati huohuo mtu anatakiwa kuendelea kutumia ARV wakati hizi cell zinajijenga kwenye mfumo ili kuzuia zisiambukizwe wakati hazijajiimarisha na baadae hizi seli zina uwezo wa kuua vurusi vyenyewe na cell zenye virusi

lakini na hapa pia tatizo limekuwa ni kwamba hizi seli zinazopandikizwa haziwezi kuua virusi vyote na kuua cell zote zilizoambukizwa,lakini ni hatua nzuri zaidi iliyoikiwa.
NADHANI KWA MAELEZO HAYA MAFUPI UMENIELEWA.
 
vip mkuu mtu anawezaje kuambukiza ukimwi kwa ROMANCE(de.n..da) swal ni kwamba ukimnyonya muathirika de..n..da unaweza ukakupata ? km hatumii ARV (hii kwa wale walio nao ila hawajapima na hawajijui so hawatumii ARV)

Inaelezwa kuwa upo uwezekano wa kuambukizwaukimwi kupitia denda,lakini mpaka sasa hakuna ushahidi hata wa mtu mmoja huko marekani aliyeambukizwa ukimwi kwa njia ya denda,uwezekao huo ni kama haupo, japo inawezekana na inatajwa hivyo ikitokea wote wawili muna vidonda mdomoni,lakini kwa ripoti iliyotoka mwaka jana mwishoni imeelezwa kuwa hakuna kabisa ushahidi hata wa mtu mmoja ulioonyesha mtu aliambukizwa kwa njia ya denda huko marekani mpaka sasa
 
Quite a lesson worth knowing. Thanks.
 
mada nzuri sana hii....sibanduki hapa...
 
Vip kuhusu sis wa uvinza? hatari ya maambukiz ikoje?
 
Je huyu mtu mwenye kinga imara ya mwili na tayari ameambukizwa akipima atapatikana na maambukizi? (Pamoja na kwamba hana dalili yoyote)

sorry nilikuelewa vibaya mwanzoni nilidhani unamaanisha wale ambao wana kinga imara isiyoruhusu maambukizi na ndio maana nikakujibu vile hapo mwanzo wa kujibu swali hili,maana sikuona sawasawa ulikuwa umeniquote kipi,majibu sawia kwa sawli lako hata mwenye kinga imara ya kuhimiri magonjwa nyemelezi kwa muda mrefu zaidi nae akipima anaonekana ana UKIMWI sawa na watu wengine
 
asante mkuu kwa ufafanuz wako, swali langu nilikuwa nataka kujua kuhusu tohara kwa wanaume kuwa kunasaidia kupunguza maambukiz kutoka kwa mwanamke mwenye vvu kwenda kwa mwanaume ambaye hajaathirika. Hili limekaaje mkuu naomba ufafanuz wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…