Mshinga
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 3,532
- 1,126
- Thread starter
- #61
sayansi ipi isiyovutia watu kusoma unayoiongelea wewe?sayansi inataka kila kitu kiwe na mvuto ndio maana hata tafiti zinatangazwa ili kuvutia watu wazisome na wazijue kama zinawahusu,labda ungesema sayansi hairusu kudanganya hapo ningekubali na mimi nimeuzungumza ukweli ndani humu humu na taarifa yenyewe haijaongezwa hata chembe ya chumvi katika ukweli wake.Mshinga, Hapa ndipo ninaposema kunapokuwa kuna UPOTOSHAJI.
1. Kisayansi, Hatuvutii watu kusoma, bali ukweli ndio unaoongea...Mada kutopendwa haimaanishi UVUTIE KWA KUPINDISHA UKWELI, to make it palatable to some people DOESN'T MAKE IT TRUE, mkuu.
rudi juu usome kwenye topic namna maelezo mafupi yalivyowasilishwa na mtafiti2. Usemapo atumiaye dawa za ARV haambukizi virusi, na kisha kusema kwa asilimia chache bado inaleta MKANGANYIKO, na ndio maana hapa nikasema hebu na tuone statistics za wapi, na study hii ilifanywaje, zisije kuwa study za mtu mmoja , under sample size ya watu thelathini, then tuhitimishe kwa kusema hayo hapo juu.
Pili, dara validation ina umuhimu wake, tafiti zinapofanyika hutoa asilimia fulani kwa maana ya majibu, mfano confidence values/interval na hapa ndipo kwenye uzito wenyewe.
3. Uliposema hujaelewa, nikufafanulie..Unasema kuwa mgonjwa/muathirika akitumia ARV huwa katika hali ya kutoambukiza, nami nikauliza unapoongelea suala la utumiaji wa ARV na "kutosababisha maambukizi" unapaswa kutambua muda.
-Hapa namaanisha Muda wa Utumiaji dawa. Mf. magonjwa hutofautiana, na hata uwepo wa dawa katika mwili/mzunguko wa damu (Half life) hutofautiana.Yaani mgonjwa anapotumia dawa za malaria, si sawa na dawa za Kichocho.
Sasa unapokuja katika suala la UKIMWI picha ni tofauti, kwa sababu kitabibu kuna vitu viamuavyo/viashiriavyo hali ya uponaji wa mgonjwa kama.(Prognostic factors)
utofauti wa hawa utakuwa juu ya uimarikaji wa afya zao na si juu ya uwezekano wa kuzuia maambukizi mabao unategemea matumizi ya dawa tajwai. Muda wa mgonjwa kujitambua hadi kuanza kutumia dawa.
(aliyeathirika toka mwaka 1999 na kuanza kutumia dawa mwaka 2013 si sawa na aliyeathirika mwaka 1999 na kuanza kutumia dawa mwaka 2000)
mgonjwa akimeza dawa kuna mambo mawili ambayo ungeyaongelea ndo ningekuelewa na si swala la muda.ii. Muda mgonjwa aliyowisha tumia tiba.( Hapa namaanisha Muathirika aliyetumia dawa kwa Mwaka mmoja si sawa na aliyeanza kutumia dawa wiki mbili, ingawa wote ni waathirika).
1.mtu anameza dawa lakini kiwango cha dawa ile hata akipimwa hakionekani katika mzunguko wa damu maana mkusanyiko wa dawa ile haujakuwa mwingi katika damu (undetectable level)
2.mtu akimeza dawa kuna kiwango wakati ambapo akiwa anaendendelea kumeza dawa,dawa ile inakuwa imesambaa mwilini kiasi cha kuonekana moja kwa moja katika mzunguko wa damu (medicine at the detectable level), na hili swala halitegemei sana muda kama sababu pekee, bali linategemea dawa yenyewe na kiwango cha dawa
sikulenga watu wanaokiuka mashariti, nililenga wale wanaotumia dawa, nikimaanisha lazima utumiaji wa dawa uambatane na mashariti, sasa akiacha ni mambo mengineiii.Muathirika amekuwa akitumiaje dawa.
Hapa, kuna mengi sana ya kuongelewa, mara kadhaa wagonjwa huacha dawa wanapojisikia unafuu/au hali fulani ya kumudu kazi zao za kila siku. Pili kuna kipindi cha nyuma dawa zilikuwa za shida katika baadhi ya vituo hivyo kufanya kutopatikana kwa urahisi. Tatu, kutokana na baadhi ya madhara mfano, Ganzi, kuishiwa damu n.k waathirika wamekuwa wakisita kuzitumia.Sasa uwapo na wagonjwa wawili mmoja mwenye kutumia dawa kila siku na mwingine mwenye kuwa katika tiba anapojisikia, ni yupi mwenye kusema "hawezi kuambukiza"..au kwako wote hawa ni sawa?!!!
Ikumbukwe tunapoangalia Clinical, Immunological treatment faiure, IRIS, n k muda kama ambavyo nimekwisha sema hapo juu ni crucial.
hapa napo nilimaanisha kwa wale wanaopimwa mapema na kupata dawa mapema na nimeweka wazi katika maelezo ya awali kuwa labda kwa wale wasiopima na kupewa dawa,unaweza kurejea maelezo yangu, na kwa kuongezea , yote yanawezekana lakini utafiti ama ushahidi wa kisansi unahitajika kuthibitisha haya tofauti na inavyosemwa sasa katika maelezo hayo hayo ya kisansi4. Ninapingana na wewe kusema kwamba maginjwa nyemelezi hayapo, mkuu sijui uko maeneo gani au labda hospitali/ kituo gani cha afya ambako hakuna wagonjwa hawa! Lakini kwa uelewa wangu mdogo, ni kwamba magonjwa nyemelezi yapo sana, na hata kwa baadhi ya wagonjwa ambao wamekuwa wakitumia kinga (CTX prophylaxis).
Ikumbukwe, kuwa si vituo vyote vyenye dawa, si waathirika wite watumiao dawa inavyopaswa, si waathirika wote wenye kujijua!
fine,nimeweka maelezo yangu,japo kwa leo sina muda sana wa kupitia vitu vingi katika hayo maelezo unayosema,nitafanya hivyo5. Mwisho mkuu, tafiti ni nyingi, na ni vizuri kupata taarifa kupitia barua pepe kama ambavyo umesema hapo juu, Subsription ni jambo ambalo mtu yeyote anaweza kufanya na kupata taarifa hizo, ila cha muhimu ni VALIDITY ya taarifa. Muda wa tafiti zaidi ya mwaka mmoja ni mwanya/pengo kubwa kitabibu hasa kitafiti! Mfano tazama baadhi ya takwimu niliyoweka ya miezi miwili iliyopita ina tofauti kubwa na maelezo yako.